DOKEZO Jengo la Walimu katika Shule ya Msingi Nsololo (Tabora) lililoezuliwa paa limetelekezwa mwezi wa pili sasa

DOKEZO Jengo la Walimu katika Shule ya Msingi Nsololo (Tabora) lililoezuliwa paa limetelekezwa mwezi wa pili sasa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
WhatsApp Image 2025-02-27 at 13.27.32_6dff24d8.jpg
Jengo la Shule ya Msingi Nsololo lililoezuliwa paa limetelekezwa Walimu wanakaa chini ya miti

Nimefika Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, kuna jambo limenisikitisha na baada ya kuwauliza Wenyeji, nguvu ndio zimeniisha kabisa.

Nimeambiwa huu sasa ni mwezi wa pili na nusu kuna jengo la Walimu katika Shule ya Msingi Nsololo halijarekebishwa baada ya paa lake kuezuliwa na mvua, hivyo Walimu kukosa sehemu ya kukaa.

Nilifika hapo kumtembelea ndugu yangu anayesoma katika shule hiyo na akanieleza kuwa Walimu wamekuwa wakikaa kwenye miti wakati wanaposubiri wenzao wamalize vipindi.

Nilipofuatilia zaidi nimebaini kuwa hakuna jitihada za msingi zilizofanywa licha ya kuwa Viongozi wa ngazi ya Wilaya wanajua kinachoendelea.

Hivi Ofisi ya Mkurugenzi wa Nachingwea haioni kinachoendelea? Vipi kuhusu kile kitengo cha maafa, nini kinaendelea? Hii sio sawa.
WhatsApp Image 2025-02-27 at 13.27.42_8e6749ed.jpg

WhatsApp Image 2025-02-27 at 13.27.40_e4a09c05.jpg

WhatsApp Image 2025-02-27 at 13.27.30_59b12643.jpg
 
Pesa zinatumika kutengeneza PR ya chai na vitumbua vya mama..
 
Back
Top Bottom