Rwabugiri,
Maneni mazito sana Mkuu.
Mie sijali kama huyu Mhagama ana sifa gani na kafanya nini huko nyuma. Hawa viongozi wetu wamejiachia sana. Wakiwa wanatunguliwa namna hii walau wataanza kuwa makini. Si mnaona hata Masha sasa hatumsikii? Nafikiri kashashika adabu yake. Sidhani kama bado anakunywa ovyo Rose garden na kuropoka (iliandikwa humu JF). Viongozi wetu walijiachia/wamejiachia sana sana utafikiri akina dada wakishaolewa, kutunza miili yao inakuwa historia. Siku anaolewa mwembamba, hapo ongeza sasa azae, atajaa utafikiri anaenda kucheza Sumo (akina dada don't take it personal na hii si akina dada wote na nafahamu wengine huwa ni matatizo ya hormons).
Mama Mhagama, shambulia hawa wote. Na maadamu imeandikwa "achezae na upanga basi hufa na upanga", wapinzani wa Mhagama wameshapewa mfano wa jinsi ya kumkoma nyani. Kwani alikuwa wapi miaka yote nyuma? Na yeye atakomwa (na naombea akomwe) wakati wa uchaguzi. Hili joto likiwa kali, litatusaidia kujenga miiko ya viongozi kwani mtu ukimess up, wanakuondoa kwani utawapakazia wote.
Hongera CHADEMA na hasa Dr. Slaa na Zitto kwa kuleta huu mchezo wa Mabomu ingawa muasisi wa mabomu ndugu Mzindakaya ALIRUBUNIWA ki-siasa na Mkapa na akapata kitu kidogo na sasa mabomu yake kayafiata kabisaaa. Shame on you Mzindakaya na Mafisadi wote waliokuingiza kwenye Mduara wao.