Nimekuuliza swali moja je hao ni waalimu wa msingi au sekondari? Umeshindwa kujibu?
Kwa kuwa elimu yao ni darasa la saba basi ni waalimu wa shule za msingi. Na kama ni waalimu wa shule za msingi basi masuala yao ya ajira yanamalizwa na halmashauri za wilaya.
Na kama sheria inasema kuwa darasa la saba hana ajira, kwanini uyaite majibu ya waziri ni rahisi? Watu hawana sifa za kupewa ajira? Na kama wanasifa wapeleke nondo zao.
Mkuu naona labda ulipitwa vile vielelezo alivo vitoa Mhagama, wengine wamemaliza hadi kidato cha sita, na hao wengine kulingana na sheria aliyo inukuu Mhagama kwamba kama wamepitia kozi mbali mbali na experience sheria ina ruhusu kuwaajiri. Hata hivo myaka yote hiyo alishindwa nini kutoa ufafanuzi mpaka asubili kibano? Huwezi ona bado kwamba kuna sehemu hakuwajibika hivyo ni halali alivyo kumbushwa kama ilivyo ada?