Jenista Karibu Afya:; Fanya Haya Kwa NHIF

Ni waziri bora. Ana rekodi nzuri.
Naomba akomeshe/azuie utaratibu wa wastaafu kwenda kuhakikiwa mkoani.
Wengi ni wazee sana, wagonjwa, hatuna pesa na wengine ni walemavu.
Utaratibu wa sasa ni janga kwetu wastaafu.
Abuni namna bora ya kutuhakiki huku tuliko.
 
Hii wizara aliyopo kwa sasa inahusikaje na wastaafu?
 
Aisee management ya hospital nyingi za umma ni very very poor.
Jana nimeenda hospital ya Rufaa ya Mkoa et unapanga foleni kupewa control number kisha unapanga tena foleni kulipia huduma badae unapanga tena foleni kupewa listi ya malipo uliyofanya!!!
Huduma hizo zipo sehemu tofauti tofauti kibaya zaidi Pay point ni moja tu.
 
Sina hakika kama ataiweza Wizara hii! Bado mimi naona Ummy alifaa tu.
 
Hakuna mtu katili ktk serikali hii kama huyu mama! Kumbukeni huyu ndiye aliyeleta kikokotoo! Sasa subirini aimalizie hiyo NHIF
 
Tatizo laanzia CCM na wafanyakazi wa serikali wanalipa pesa ndogo sana
 
Wala sitoshangaa!

Naamini watendaji wazuri wapo nje ya mfumo wa kisiasa.

Hoja yangu ya kusema ni wakati wa sasa mawaziri watokane na merit tena isiwe kama Kenya wanakuwa nominated ndio wafanyiwe vetting bali watu wawe wanaapply ndio vetting ifuate.
ndio maana Katiba mpya ni jambo la muhimu, ama ni la lazima hakika!
 
TOTO AFYA irudishwe kwa umuhimu kabisa
 
Sina hakika kama ataiweza Wizara hii! Bado mimi naona Ummy alifaa tu.
Ummy hapana. Ame overstay kuanzia 2015 hadi 2019 wakati wa Magufuli. Kisha akarudi 2021-24 wakati wa Samia. Yeye ndiye chanzo cha mdororo huu mkubwa wa huduma.

Ame FISADI sana na ni super rich woman ndiyo maana naye akaingia kiburi cha kutaka Januari Makamba agonbee 2025 kwenye kura za CCM
 
Hakuna mtu katili ktk serikali hii kama huyu mama! Kumbukeni huyu ndiye aliyeleta kikokotoo! Sasa subirini aimalizie hiyo NHIF
Kikokotoo ni Magufuli mwenyewe wala usimsingizie Jenista
 
Pia kungetakiwa kuwe na bima za hospital binafsi na hospital za serikali
NHIF iko kwenye njia ya kwenda kaburini na actuarial study ilifanywa na serikali kuambiwa wasipojipanga NHIF inakufa ndani ya miaka 2-3 ijayo
🔴Serikali hailipi mamilioni ya hela ya NHIF waliyokopa kununua madege wakati wa Magufuli
🔴 Wastaafu wa umma wote wamepelekwa NHIF na serikali haipeleki michango yao lakini wanataka watibiwe na wanatibiwa bila seriukali kupeleka michango
🔴 Toto Afya Card na madudu mengine mengi yaliyoko NHIF pale ambayo CAG ilishasema mpaka kachoka...

NAMTAZAMA Jenesta Mhagama na aina yake ya majibu ya juu juu anayoyatoaga bungeni akikandikwa maswali halafu natazama anachokwenda kukutana nacho NHIF hasa nyakati hizi za uchaguzi NAMUONEA HURUMA SANA
 
Muhimu sana.

Hii ya waziri kutokana na wabunge ndio imeleta watu kama akina Nape zero brains kabisa mtu yuko wizarani halafu hajui kazi zake.
Ni kweli, naamini kwenye Katiba Mpya Mawaziri hawatatokana na wabunge. Bali watakuwa watu mahiri kwenye fani zao
 
Kwenye namba 5 umefuka mazima

Actually hizo packages ndizo zinafanya mfuko kusimama

It’s always the people in the apex who finance the pipeline in the base hauhitaji F tatu kujua hilo
 
Fake news
 
Nachofahamu anastashahada ya Elimu kutoka korogwe TTC hii imekaaje au alijiendeleza hatujui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…