Jenista Mhagama afika Mji wa London, azungumza na Watanzania waishio Uingereza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amekutana na wana-jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) katika mji wa London baada ya kuwasili Disemba 08, 2024 na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya nchini Tanzania.
Screenshot 2024-12-09 at 23-41-18 Instagram.png

Miongoni mwa mambo waliyojadiliana katika kikao hicho ni pamoja na dhana ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha uendelezaji wa wataalam katika ngazi ya bingwa na ubingwa bobezi na kufungua fursa za wataalam wa afya kupata ajira nje ya nchi.

"Vilevile tumejadiliana kuhusu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na dawa, kuimarisha huduma za mkoba nchini kwa kufanya kambi mbalimbali za huduma za kibingwa kwa kutumia madaktari kutoka Uingereza na maeneo mengine," amesema Waziri Mhagama.
Screenshot 2024-12-09 at 23-41-30 Instagram.png

Aidha, Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa wana Diaspora hao kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania.
Screenshot 2024-12-09 at 23-41-41 Instagram.png
Screenshot 2024-12-09 at 23-41-53 Instagram.png
Screenshot 2024-12-09 at 23-41-59 Instagram.png
 
Hahaha sasa hao wako London watakakikushaje tuna pata huduma bora sisi wadanganyika, nilisikia wameukana Uraia wao au hawa wao ni tofauti na diaspora tunaoambiwa wanatafutiwa haki maalumu?
 
Gafla tu nimekumbuka kile kingreza chake cha kushukuru kuchaguliwa kwa marehemu Dr Ndugulile kule Angola
 
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amekutana na wana-jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) katika mji wa London baada ya kuwasili Disemba 08, 2024 na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya nchini Tanzania.
View attachment 3173389
Miongoni mwa mambo waliyojadiliana katika kikao hicho ni pamoja na dhana ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha uendelezaji wa wataalam katika ngazi ya bingwa na ubingwa bobezi na kufungua fursa za wataalam wa afya kupata ajira nje ya nchi.

"Vilevile tumejadiliana kuhusu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na dawa, kuimarisha huduma za mkoba nchini kwa kufanya kambi mbalimbali za huduma za kibingwa kwa kutumia madaktari kutoka Uingereza na maeneo mengine," amesema Waziri Mhagama.
View attachment 3173390
Aidha, Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa wana Diaspora hao kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania.
View attachment 3173391View attachment 3173392View attachment 3173393
Asithubutu kuongea kwa English, atajidhalilisha. Mshaurini atumie Kiswahili tu
 
Hahaha sasa hao wako London watakakikushaje tuna pata huduma bora sisi wadanganyika, nilisikia wameukana Uraia wao au hawa wao ni tofauti na diaspora tunaoambiwa wanatafutiwa haki maalumu?
Taratibu taratibu tutakuja kuukubali urai pacha kama nchi nyingine ndani ya EAC walivyoukubali,kwani faida yake ni kubwa kuliko hasara zake.. Majirani zetu wako busy kuingia mikataba na nchi za ulaya na marekani ya kuwapeleka rais zao kufanya kazi nje ya nchi wakati kwetu kupata passport tu mpaka jasho likutoke. 😎
 
Yani wawapeleka nchi za ulaya kufanya kazi, sasa Tanzania wakitupeleka huko nani atalipa mikopo ya HESALB? Ukifika ulaya deni wanafuta?
 
Kwa faida yao bora wakawatafutia ajila vijana nje ya nchi kwani soko la ajila nchini ni dogo kulinganisha na wanaohitaji mfano angalia wahitimu wa vyuo vikuu pekee kwa mwaka hapa nchini ni wangapi?hata huo mkopo unalipaje na kazi huna?
 
Kazi nasikia wanatoa ukiwa uvcc, ni kujiongeza tu.
 
Wa ndio majuu huko

Waliohudhuria ni vidole vya mikononi, wengine bila viongozi wa wa Tizedi kwanini hawakufika!!! Viti tupu vya onyesha

Hawakualikwa au wameisusia?
 
Wametumia lugha gani?
Halafu huyo ajuza mimi toka nimezaliwa yeye ni waziri tu,hachoki?
 
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amekutana na wana-jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) katika mji wa London baada ya kuwasili Disemba 08, 2024 na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya nchini Tanzania.
View attachment 3173389
Miongoni mwa mambo waliyojadiliana katika kikao hicho ni pamoja na dhana ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha uendelezaji wa wataalam katika ngazi ya bingwa na ubingwa bobezi na kufungua fursa za wataalam wa afya kupata ajira nje ya nchi.

"Vilevile tumejadiliana kuhusu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na dawa, kuimarisha huduma za mkoba nchini kwa kufanya kambi mbalimbali za huduma za kibingwa kwa kutumia madaktari kutoka Uingereza na maeneo mengine," amesema Waziri Mhagama.
View attachment 3173390
Aidha, Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa wana Diaspora hao kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania.
View attachment 3173391View attachment 3173392View attachment 3173393
Per diem, uliwezalo leo lifanye usije ukalijutia baadae kwani siku ndizo hizo zinayoyoma.
 
Ni ziara ya kikazi au binafsi? Sioni tija ya hiyo safari kwa taifa.

Nikajua anakutana hata na waziri wa afya wa Uingereza kuona jinsi wanaweza kusaidia katika scholarship Watanzania kwenda kusoma masuala ya afya huko, mambo ya vifaa tiba, wataalamu wa afya kutoka Uingereza kuja kutoa training Tanzania, medical n.k
 
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amekutana na wana-jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uingereza (Diaspora) katika mji wa London baada ya kuwasili Disemba 08, 2024 na kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya nchini Tanzania.
View attachment 3173389
Miongoni mwa mambo waliyojadiliana katika kikao hicho ni pamoja na dhana ya umuhimu wa Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha uendelezaji wa wataalam katika ngazi ya bingwa na ubingwa bobezi na kufungua fursa za wataalam wa afya kupata ajira nje ya nchi.

"Vilevile tumejadiliana kuhusu kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na dawa, kuimarisha huduma za mkoba nchini kwa kufanya kambi mbalimbali za huduma za kibingwa kwa kutumia madaktari kutoka Uingereza na maeneo mengine," amesema Waziri Mhagama.
View attachment 3173390
Aidha, Waziri Mhagama amesisitiza umuhimu wa wana Diaspora hao kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania.
View attachment 3173391View attachment 3173392View attachment 3173393
Mungu anisamehe huyu huwa namuwazia kama huvutaga 😊😊😊👍👌❤😂🤣
 
Afadhali amekwenda kuzungumza na watanzania Kiswahili manake ingekuwa aibu kwa nchi kama angekwenda kuzungumza na wazungu. Arejee mapema nyumbani.
 
Back
Top Bottom