inawezekana ikawa ni mass psychogenic illness (mass hysteria).
Lakini pia ni vizuri kuchunguza mazingira yao kiujumla ya hao wanafunzi:-
->Chakula na Maji wanayokunywa (ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa vitu visivyofaa katika chakula-maji)
->Hali ya hewa ya eneo.
->Magonjwa & Maambukizi - mlipuko wa magonjwa yanayoweza kuathiri Mishipa ya Fahamu au Mfumo wa Homoni.
->Mambo ya kisaikolojia ya umma (kwa this case could be, mfano mass stress sabb ya mitihani, adhabu kali zisizo na tija, stori-masimulizi ya hofu, n.k.
Kundi la wasichana wa umri huu likiwa pamoja ni rahisi kuathiriwa na msongo wa mawazo, na athari kuonekana kirahisi sabb wapo very sensitive kwa emotion compared to boys.
Kwa nini hutokea sana kwa shule za wasichana?
Tatafiti zinaonyesha hivi:-
Vijana (hasa wasichana wa umri wa sekondari) wako Sensitive zaidi kwa Stress za Kijamii, na ni rahisi kwao kuonesha matokeo ya hii psychological disturbance kuliko kundi la wavulana.
Athari huonekana dhahiri sabb ya uwingi wao katika eneo moja ambapo huambukizana kihisia.
Nini kifanyike.?
->Wanafunzi wapewe Counseling (ushauri nasaha).
->Wazazi/walezi na waalimu pia wapewe Counseling na namna ya kupambana na hii hali.
Lengo ni kupunguza Msongo wa mawazo wanafunzi, hivyo:-
->Bainisha vyanzo vyenye kuleta hofu.
->Toa watu hofu au boresha mazingira yoyote yanayoweza kuleta hofu katika kundi la wasichana wenye umri wa mwanzo wa ujana, Mfano uvumi hasi wenye kujaza hofu, au stori za kutisha zilizopo eneo husika, n.k..
->Promote & encourage Michezo & Burudani (michezo, sanaa [muziki, maigizo] n.k, husaidia akili kuwa fresh na ku-refresh mwili pia)
->Kufuta corporal punishment, adhabu ziendane na kosa, sio kukomoana.
->Kuchangamana na wanafunzi wa shule nyingine za jirani (mfano mara moja moja kufanya 'Debate', 'Sports' competitions na shule jirani, n.k.) ila kila kitu kwa kiasi.
->Mafundisho ya kidini yenye tija na sio yenye kutisha kwa kuharibu psychology (kila kundi kwa imani zao)
->Ratiba za shule pia ziwe rafiki, zibalance mambo, ili kupunguza unnecessary stress. Shule isiwe sehm ya mateso.
Msisitizo. 😎
Ukiwa na hoja au opinion yako, na wewe itoe pia hapa jamvini.