Lissu alisema nini kuhusu katiba mpya na rule of law?Hili ni tatizo kubwa la Chadema. Tumeona kwa wale G55 ambao waliambiwa kuwa watapewa nafasi ya kujieleza lakini wakaishia kusimangwa. Tuliona jinsi Heche hakutaka kumsikiliza Sigrada na kumbeza baada ya kuumizwa na mlinzi wake. Chadema inaiga mambo ya CCM ( zidumu fikra sahihi za viongozi wetu n.k.) badala ya kujitofautisha nao. Sidhani kama kutakuwa na mabadiliko yeyote ya maana Chadema ikishika dola. Itakuwa ubabe ule ule. Na kwa vile kinajiona kuwa ndio chama pekee kinachostahili kuitwa upinzani, kitawaumiza wengi
Amandla...
Majizi ya CCM kama Mwigulu na Ridhiwani huyaoni?.fisadi heche anakataliwa kila kona ya nchi na wanachama wake 🐒
Tuliza mihemko na makasiriko jikite kwenye hoja mahususi mezani na itapendeza zaidi 🐒Majizi ya CCM kama Mwigulu na Ridhiwani huyaoni?.
VIpi kashfa kama za Richmond na EPA nazo huzioni wewe mpumbavu?
Sidhani. Anaipasua ili apate Nini?. Hawa ni wahuni wanatafuta stori.Mbowe ataipasuwa CDM kwa msaada wa CCM, wavaa ushungi wote wataenda na Mbowe.
Hawana msimamoMwanmke hastahili nafasi yoyote ya uongozi nipigeni Ban.
Ubabe upi?. Unataka watu wasikilizwe kwenye majungu?. Waliposikia watashtakiwa mahakamani wamekaa kimya.Hili ni tatizo kubwa la Chadema. Tumeona kwa wale G55 ambao waliambiwa kuwa watapewa nafasi ya kujieleza lakini wakaishia kusimangwa. Tuliona jinsi Heche hakutaka kumsikiliza Sigrada na kumbeza baada ya kuumizwa na mlinzi wake. Chadema inaiga mambo ya CCM ( zidumu fikra sahihi za viongozi wetu n.k.) badala ya kujitofautisha nao. Sidhani kama kutakuwa na mabadiliko yeyote ya maana Chadema ikishika dola. Itakuwa ubabe ule ule. Na kwa vile kinajiona kuwa ndio chama pekee kinachostahili kuitwa upinzani, kitawaumiza wengi
Amandla...
Unapoanza kwa kumuita mtu mropokaji ndio unapokosea. Haupo kwa ajili ya kuelimishana bali shari.Usiwe unaropoka usiyoyajua.
Wote tulisikia clip za mahojiano. Tulisikia akiomba asikilizwe. Sigrada na Rose walikuwa hawaelewani hivyo mkutano mzima walijazwa watu wa upande wake. Tofauti na unavyosema Rose ndie aliyekuwa anamchukia Sigrada kwa sababu waliamini alikuwa upande wa Mbowe. Na Sigrada alipomshukuru na kumsifia Mbowe mbele ya Lissu kwenye mkutano wa Bawacha akawa amejipigia msumari kwenye jeneza lake. Ni mbinu ya kawaida kuita shutuma yeyote usiyopenda kuwa ni majungu. Ni mbinu inayotumiwa sana na karibu vyama vyote vya siasa ikiwemo CCM.Sigrada alipewa muda mrefu sana wa kujieleza kwenye kikao, mbele ya wajumbe waliokuwa wanajua kila kitu juu ya chuki zake dhidi ya Tose Mayemba. Malalamiko yake yalijaa majungu matupu.
Wajumbe walikuwa wamepangwa. Na Sigrada alinyamazishwa kila alipotaka kujitetea. Badala ya kusikilizwa akatolewa nje ya mkutano. Wenye nia njema wasingemtoa nje ya kikao bila yeye kumaliza utetezi wake. Mwenyekiti makini angehakikisha pande zote zinasikilizwa. Kusema kuwa Heche hakujua kinachoendelea Njombe ni uongo maana bila shaka Rose kama mjumbe mwenzake wa Kamati Kuu alikuwa amemueleza upande wake. Kikao kilikuwa cha kumchinja Sigrada.Heche kwa kuwa hakuwa na uhakika na tuhuma zake, aliwauliza wajumbe. Kila mjumbe akazikataa tuhuma zake. Kila mjumbe aliposimama kutoa maoni yake, Sigrada alipoambiwa atulie hakutaka. Baadaye akaambiwa atoke nje, asubiri atakapoitwa.
Unajichanganya. Sigrada alitaka kurudi ndani baada ya kumuomba Heche. Na ni kweli alijaribu kuingia ndani baada ya mlinzi kumkatalia. Na ni kweli mlinzi alimsukumiza akaanguka. Heche angekuwa na nia ya dhati ya kumsikiliza angeamuru aruhusiwe kuingia. Ndivyo demokrasi ilivyo.Nje akaanza kulazimisha kurudi ndani. Akaanza kumdukuma mlinzi. Mlinzi naye alioomsukuma, Sigrada akaanguka.
Alizira nini? Unataka kusema baada ya kuanguka aliruhusiwa kuingia? Ulitegemea polisi wawalazimishe walinzi wa Chadema wamruhusu kuingia? Choice ya neno "kubugia" linaweka wazi bias yako. Kunywa bia sio kosa la jinai.Viongozi karibu wote wa Chadema ni wanywaji wazuri wa vilevi. Na mara nyingi huo unywaji wao wa vilevi umetumiwa na CCM kudai kuwa walikuwa wamelewa jambo lilipowakuta. Ulitaka aende akajikunyate kwake baada ya kutotendewa haki?Na hayo yalifanyika mbele y polisi ambao wlikuwa wakilinda kikao. Sigrada aliposimama, akazira na kwenda baa ambako alibugia bia mpaka sa 8 usiku alipodai kusikia kuumwa.
KTangu lini hilo limekuwa kosa? Kwa hiyo unakiri kuwa alihitaji matibabu? Hakuwa anajifanya.Hata alipoenda hospitali, ilishindikana kumpa baadhi ya matibabu kutokana na kiwango kikubwa cha pombe mwilini.
Unajichanganya. Kumsukumiza mtu ni assault. Mtu anaweza kupata athari kwenye kichwa bila hata ya kujitambua. Mara chungu mzima watu wameanguka, wakadhani kuwa wako okay lakini baadae wakagundulika kuwa walipata tatizo kwenye ubongo.Wewe unadhani kama mlinzi angekuwa alimpiga Sigrada, polisi wliokuwepo hapo wangeshindwa kumdhibiti huyo mlinzi?
Haibadilishi ukweli.Wewe ni mwongo mkubwa.
G55 waligundua kuwa kile kikao kilikuwa kimepangwa kwa ajili ya kuwasimanga. Badala ya kutafuta ukweli lengo lilikuwa ni kuwazika. Wao wakaona isiwe shida, wakaita press conference wakaelezea msimamo wao bila bughudha yeyote. Na ni kweli, tulishuhudia yaliyoendelea kwenye mkutano wa Chadema. Ni simango kwa kwenda mbele. G55 waliwastukia.Wale 55, waliitwa kwenye kikao ili watoe hoja zao, wakakubali, lakini siku ya kikao wakadai kuwa wao wana kikao na wanahabari.
Sasa hapa muongo ni nani? G55 walitangaza kutoka Chadema baada ya kuona kuwa hawana nafasi katika kile chama. Baadhi ya G55 waliwahi kuwa viongozi waandamizi ndani ya Chadema. Na, ndio, isingekuwa tatizo kwa baadhi ya viongozi wa Chadema kuongea nao mmoja mmoja faragha. Hasa kama ulikuwa na nia ya kuunganisha chama baada ya uchaguzi na kuthibitisha kuwa kila mtu ana nafasi ndani ya chama. Hilo la hongo halistahili jibu.Ulitaka CHADEMA ifanye nini? Imfuate kila mmoja nyumbani kwake kwenda kumhoji? Ukumbuke kuwa wale 55 baada ya kupokea hongo, hawakutaka kuhudhuria kikao chochote, wakaanza kutangaza kimakundi kuwa wanaenda CHAUMA.
Paranoia tupu. Waiue Chadema ili iwaje? Wangekuwa na nia mbaya na Chadema wangebakia ndani yake ili waichimbe na kuitilia fitna chini chini. Wao kwa uwazi kabisa walitoka na kuuachia uongozi mpya chama chao. Hiyo ndio demokrasi. Na wangekuwa na nia ya kuimaliza CDM wangejiunga na ACT-WAZALENDO badala ya chama kidogo kama Chaumma.Wale hawkuwa na haja ya kutaka kusikilizwa na yeyote kwa sababu mikakati yao waliyokuwa wamrpanga ilikuwa kuiua CHADEMA, na kutengeneza chama kingine.
Kushawishi wengine kuwaunga mkono ni siasa. Sidhani kama kuna mtu aliyeamini viongozi wengi wa Chadema waondoke nao. Unasema walidharauliwa na umma lakini haipiti siku bila kuwasikia Chadema waliisimanga Chaumma. Imefika mahali inaonekana kuwa Chadema ina uhasama mkubwa dhidi ya Chaumma kuliko iliyokuwa nayo dhidi ya CCM.Walikuwa busy kuwashawishi wanachama na viongozi mbalimbali ili wahame na kundi kubwa. Wanachama na wananchi kwa ujumla, wakawadharau.
Najua uta niambia.Lissu alisema nini kuhusu katiba mpya na rule of law?
Hizi ni platitudes tu. Ingekuwa kweli Chadema inaamini katika checks and balances wangeanza ku practice ndani ya CHADEMA. Badala yake tunaona waki vilify kila mmoja anaediriki kudai hizo checks. Hawaaminiki. Nao watakiuka hiyo Katiba kama ambavyo wenzao wanavyofanya.Ngoja nikukumbushe kama umesahau, alisema tupate katiba mpya, bora ambayo mamlaka zina check and balance, kusudi hata yeye Lissu akiwa Rais, akaboronga katiba hiyo hiyo itumike kumuwajibisha.
Ndio maana ni muhimu kuhakikisha kuwa vyama vilivyopo vinaishi kila wanacho hubiri. Uongozi na nchi bora itapatikana pale tu kila mwananchi atakuwa na haki ya kutofautiana na uongozi wake bila hofu yeyote. Kila mwananchi atakapo kuwa ana haki ya kuhoji kiongozi wake na kujibiwa kwa heshima anayo stahili. Na hii inawezekana kama jitihada za dhati zitafanyika ili kuwaunganisha hata wale wanaotofautiana ki mawazo. Unfortunately, hilo silioni katika Chadema ya leo.Hatuwezi kupata nchi bora kwa kutegemea utashi wa kiongozi mmoja mmoja.
Ninaelewa ndio maana siko tayari kudanganywa na maneno mazuri.Halafu we ni mtu unayeelewa sio ngumbaru acha kujitoa ufahamu.
Naweka msisitizoMwanmke hastahili nafasi yoyote ya uongozi nipigeni Ban.
Kiswahili nacho ni kigumu. Anayeomba msamaha ana msamaha gani tena wa kutoa moyoni? Mimi nilidhani anayeombwa msamaha ndiye anayeweza kutoa msamaha!