Jerry Muro ameiaibisha nchi, TFF, Yanga na Wanataaluma..ajiuzuru!

Jerry Muro ameiaibisha nchi, TFF, Yanga na Wanataaluma..ajiuzuru!

sasa wewe utaiweza nafasi ya jerry muro au unapiga kelele tu

Mimi naweza tu nikamfundisha vizuri kama Mkufunzi wa hayo masuala ili siku nyingine asije kujitia aibu na kuonekana kituko na mpuuzi mbele ya wenye ueledi wao na wana taaluma.
 
Mkuu si nimeshajinasibu kabisa hapo juu kuwa Mimi ni Yanga? au unataka nifanyeje ili uamini? Naipenda Yanga tena hasa Mchezaji wetu huyu mpya wa Zambia sijui Zimbabwe aitwae " Chura " kwani nasikia anapiga mpira wa kurukaruka kama chura mwenyewe vile.
Te te te bila shaka wewe ni Sinura Fc
 
Nikiwa kama Mwanachama wa Yanga nina haki ya kulalamika kwa Kiongozi wetu tuliyemchagua kwa njaa zetu na umasikini wa kiupeo unaotukabili " Gabachori " ili hatua stahiki zichukuliwe. Tena unatakiwa unipongeze Mimi mwana Yanga mwenzio badala ya kunilaumu. Uko wapi Mkuu kwa sasa? Kama vipi tukutane huku Chalinze kwa " Babu " tunapojitahidi kupunguza hizi goli saba au tisa ambazo nimethibitishiwa kuwa ndiyo tutafungwa na TP Mazembe tarehe 28 June 2016. Anahitajika mtu wa kujitoa muhanga ila bahati mbaya kila mtu anapenda bado kuishi.

Mbona nchi inaendeshwa kibabe babe husemi watu wajiuzulu?
 
Kumbe hadi nyumbani kwa wanaume wenzio unapajua?

Sasa kama 24/7 nakuja kukuchukulia Mkeo hapo hapo nitaacha kupajua? Halafu acha tabia yako ya kuanika chupi zako zilizotoboka dirishani Mkuu kwani unajichoresha sana na Mkeo huwa ananilalamikia sana hii kitu.
 
Sasa kama 24/7 nakuja kukuchukulia Mkeo hapo hapo nitaacha kupajua? Halafu acha tabia yako ya kuanika chupi zako zilizotoboka dirishani Mkuu kwani unajichoresha sana na Mkeo huwa ananilalamikia sana hii kitu.

Naona leo umeamua kuanika hekima zako zote hapa...hongera!
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na pia ni ya kusikitisha Shirikisho la Soka barani Africa ( CAF ) jana limesikitishwa na kitendo cha Idara ya Mawasiliano na Habari ya Klabu ya Yanga ( ambayo inaongozwa na Jerry Muro ) kwa kutokujua tararibu nzima za utoaji na upokeaji wa taarifa za Shirikisho hilo.

Kitendo ambacho CAF wamesikitika nacho ni baada ya kuona Klabu ya Yanga kupitia Idara yake hiyo ya Mawasiliano na Habari kuamua kujipangia wao siku, tarehe na muda wa mchezo wao dhidi ya TP Mazembe kinyume na taratibu za CAF ambazo hata hivyo zipo wazi na Mtu yoyote anaweza akazitafuta na kuziona.

Moja ya taratibu za CAF zinasema kuwa timu yoyote mwenyeji wa mchezo inatakiwa kutoa taarifa yake ya mechi siku tatu ( 3 ) baada ya kumaliza tu kucheza mchezo wake wa ugenini na si Siku ya nne ( 4 ) kama walivyofanya Yanga kupitia Msemaji wao Jerry Muro.

Kutokana na " upuuzi " huu wa Idara au Kurugenzi ya Mawasiliano na Habari Ya Klabu ya Yanga ambayo kwa 101% inaongozwa, kusimamiwa na kuratibiwa na Jerry Muro Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limekataa ombi la Yanga la kucheza mchezo wao huo tarehe 29 Siku ya Jumatano ijayo na Saa 1 usiku na badala yake CAF imesema mchezo huo utachezwa tarehe ile ile ( ambayo hata hivyo nasikia Mganga wa Yanga aliikataa kwani Kinyota inaonyesha Watafungwa magoli mengi ) ya 28 ambayo itakuwa ni Siku ya Jumanne na muda ni Saa 10 jioni.


Kwa haya yaliyoitokea Klabu ya Yanga ukiwa kama mtu mweledi na unayejua nini unafanya utagundua kuwa Msemaji wao Jerry Muro ametuaibisha sana Watanzania mbele ya CAF kwani kwa " upuuzi " wake hatoonekana ni yeye tu ndiye mwenye matatizo bali sasa tutaonekana Watanzania wote ni " mbayuwayu ". Vile vile kwa hicho kitendo Jerry Muro ameiabisha sana Klabu yetu / yangu ya Yanga na nashangaa kwanini mpaka sasa Viongozi wa Yanga bado wanamkodolea tu macho huyu Msemaji kwani amefanya Kosa kubwa sana tena la KIULEDI na KITAALUMA na hakupashwa hadi sasa hivi naandika hii taarifa kuendelea kuwepo Yanga.

Lakini kama haitoshi Jerry Muro amewakosea sana wenye TAALUMA yao ya Mawasiliano na Habari kwa hicho kitendo alichofanya kwani moja ya SIFA kubwa ya Mtu yoyote wa Mawasiliano na Habari ni muda wote kuwa na UFAHAMU mkubwa wa mambo, kufuatilia mambo kwa UMAKINI mkubwa na kuwa ni mtu mwenye MAARIFA huku muda mwingi akitakiwa KUJIONGEZA.

Nilichokigundua ni kwamba Msemaji wa Yanga Jerry Muro anatumia 99% ya Kazi zake katika KUJISIFU, kuisema SIMBA SPORTS CLUB, kujiita wa KIMATAIFA, kuzungumza tu kwa MIKOGO jinsi anavyopanda NDEGE na safari ya Ndege itakuwaje utadhani labda yeye ndiyo Rubani ( PILOT ) wa hiyo Ndege na kusema kuwa anaishi Mbezi Beach na ameoa Mke Mzungu na hiyo 1% tu iliyobaki ndiyo huitumia pekee katika kufanya Kazi muafaka za Yanga.

Nikiwa kama Mdau wa Michezo na Mwana Yanga tena wa KUFA KUFA kabisa naomba UONGOZI wa Yanga umwangalie huyu Msemaji wetu Jerry Muro kwa jicho la Tai ( Eagle ) kwani kwa makosa haya ya KIZEMBE kuna siku hakika atakuja kutugharimu sisi Wana Yanga na tutajuta mno. Uongozi wetu wa Yanga tafadhalini hebu tusaidieni kwani huu mchezo wetu na TP Mazembe isingekuwa UZEMBE wa huyu Msemaji wetu basi tungeucheza siku ile ile ambayo Mganga wetu wa PEMBA alitaka tuucheze ambapo tungeshinda goli 7 na sasa kwa kitendo cha Msemaji wetu kutokuwa na TAARIFA na UFAHAMU mkubwa wa KIMAWASILIANO na Watu wa CAF nina uhakika sasa kuwa hizo goli saba ( 7 ) sasa tutafungwa sisi hiyo Jumanne ijayo ya tarehe 28 huo muda wa Saa 10 jioni.

Jerry Muro muda ndiyo huu JIUZURU kwani bado hujachelewa!

Nawasilisha.


Nimecheka sana....umesema mengi lakini kumbuka jambo moja muhimu: WANACHAMA NA WAPENZI WENGI WA YANGA WANATAKA MTU WA AINA HIYO, NA WANAIPENDA MIPASHO HIYO. HATA SIMBA WAKO HIVYO HIVYO...HIZO NDIZO POLITICS ZA KLABU HIZI MBILI ZINAZOITWA KUBWA ZA YANGA NA SIMBA...
 
huyu ni shabiki wa simba damu aliwahi kutoa post moja akisema ana achana na simba hadi matatizo kadhaa yakitatuliwa pia alidai walisha wahi kuchinja hadi PAKA ili simba ishinde
 
Kwa hyo we shabiki wa KUFAKUFA, unaamini kabisa mambo ya giza kweny soka??
 
Halaf nimemshangaa sana, eti anasema wananyiwa mbinu.

yani timu za bongo ni pasua kichwa kweli, sasa CAF wanapanga njama gani wakati ratiba ipo tangu kitambo. yani walivozoea kuwapangia TFF wanadhani watawapangia na CAF.
yani nimemshangaa sana, eti figisu figusu kha
 
yeye ni msemaji wa yaliyoamuliwa lawama hizo tupoa uongozi
 
Back
Top Bottom