Jerry Muro, wapi alipo?

Jerry Muro, wapi alipo?

Hana lolote badala ya ku deal na mafisadi papa anahangaika na polisi


Si bora hata yeye alikua na uthubutu wa ku deal na hao mapolisi? Wangapi wanaona uovu unatendeka na hawajali lolote kisa kuogopa huo upolisi wao? :israel:
 
Hivi watu wakiambiwa mahandsome wapite mbele jerry nae atakwenda!!! Mmhh, sasa itabidi nielimishwe upya maana ya neno handsome. Tatizo la huyo dogo ni ulimbukeni wa umaarufu! Alitaka apande chat kwa kutumia sensitive issues ambazo yeye alidhani ni za kawaida. Mimi simwombei mabaya lakini hilo liwe funzo kwake kwamba pamoja uhuru wa habari bado hekima na busara vinahitajika katika kuamua habari gani iwe aired na kwa namna gani au habari gani isubiri muda mwafaka au habari gani isitangazwe kabisa.

Hakuna mbaya duniani jamani; acha kashifa kijana:evil:
 
Wadau leo nimekaa nikajikuta namkumbuka kijana mtanashati Jerry Muro aliyeruka Mkojo akakanyaga nanihii!,

Siku hizi yupo wapi??.

sijui unamaanisha nini hapo kwenye red mkuu...

ila kijana MURO mi nilimfagilia coz ni mtu jasiri aliyeweza kuonyesha uozo wa baadhi ya sekta, hawa ndo waandishi tunao wataka sio wale wa kujipendekeza kwa kina RA, LA et al ili wapate mkate wa siku.. pumb**u zao
 
sijui unamaanisha nini hapo kwenye red mkuu...

ila kijana MURO mi nilimfagilia coz ni mtu jasiri aliyeweza kuonyesha uozo wa baadhi ya sekta, hawa ndo waandishi tunao wataka sio wale wa kujipendekeza kwa kina RA, LA et al ili wapate mkate wa siku.. pumb**u zao

Ulichoelewa nini??
 
hayo matatizo alonayo ingekuwa ni wewe na ukaona mtu ameanzisha thread kama hiyo ungejisikiaje?

Wewe siumekufa?! unatafuta nini JF au unataka Navy SEAL waibukie hapa??!..
 
Muro hakufanya mabaya,alijitahidi kufanya kazi yake ila jamii hakumuelewa,in one side anastahili pongeze and in another side alitakiwa kuwa na ubinadamu cos alidili na trafik waliokuwa wanakula rushwa za elf 3000 ingawa hakuna rushwa ndogo na kubwa,all in all kijana alifanya kazi yake kiuweledi matatizo yaliyomkuta ni changamoto ktk kazi haziepukiki
 
Dogo atakuwa amepiga issue nyingi tu na nadhani traffic walishindwa kumshikisha mlungula sasa akakutana na mjuzi zaidi yake hata ufanye vipi dogo ni fisadi tu hakuna rushwa kubwa wala ndogo wala hakuna mafisadi papa wala mafisadi kibua kama ana hatia wamshikishe adabu No Way.
 
Waungwana asubuhi hii nikiwa safarini tulisimamishwa na askari wa barabaran. Wakti huo dreva alikuwa alishaanda Sh 2000 za ki-TZ ili kumpa trafiki.. Aina ya gari ilikuwa Corolla hizi ndefu maarufu kama Bodaboda.Gari yenye uwezo wa kubeba abiria wanne na dreva wa 5 ilikuwa na watu wanane ndani. Ukweli ni kwamba 100% ya askari barabarani wanachukua rushwa. Lakini hata 95% ya madreva huwa wamejiandaa kutoa rushwa. Sababu hasa ni kuwa madreva wengi wa ki-TZ wanakuwa na makosa mengi sana..na wakti huo hawayarekebishi sababu wanajua pesa ndogo tu itasaidia. Alichojaribu Jerry Muro ni kitendo cha kutaka kubadili Utamaduni (Culture)wa Mtanzania na njia aliyopitia ni ya hatari sana. Sijui Jerry Muro ana khali gani sasa na anajishughulisha na nini maskini..lakini tujiulize ni watanzania wangapi wanaweza kujitolea kwa namna ile huku wakiona yanayomtokea Jerry Muro. Serikali yetu ni serikali ya Majambazi ambayo kwayo haki ni adui wao mkubwa. Maana …they only know dirty business… ili kujipatia hela. Tatizo la rushwa halitamalizwa kama hakutakuwa na mikakati itakayoanzia PRIMARY SCHOOLS ili kuwafanya hata kizazi kinachokuja kiione kama laana. Wakt tukiwa wadogo ilikuwa ukikojoa kitandani utatembezwa na watoto wenzio mtaa mzima ukipigiwa makopo, ile ilimjengea mtoto taswira ya kwamba kukojoa kitandani sio tu ni kosa litalopelekea wewe kuchapwa na mama lakini pia jambo la aibu ktk jamii. I.e. .. YOU LOOK SO LOW AND STUPID IN FRONT OF THE SOCIETY. Ilikuwa ni dawa iliyokuwa ikiingia moyoni na si machoni. Dawa ya Jerry ilikuwa inaingia machoni na kamwe isingesaidia kabisa. Sisemi Jerry hakufanya Jambo jema , la hasha At least he dared. Maisha ya mtanzania mwenzetu yameharibika sababu tu he tried to do the right thing. Matrafiki wote barabaran wanachukua rushwa na kama kuna mtanzania alishawahi kuona trafiki anakataa rushwa Tafadhali aseme. Hata angekuwa anatoka chuo leo.
Utamaduni wa masai kuvaa Lubega hauanzishwi akishamaliza shule anaanzishiwa akiwa mdogo na hukuwa akiona fahari ya kuvaa lubega. Hebu leo kamchukue dadngu Annelise mtoto wa kimasai aliyekulia Jijin Dar halafu umwambie avae lubega sababu yeye ni mumasai. Kama hatakutukana basi atanuna kuonyesha hajapendezwa. Hata kungetokea watu mia wote wakatumia mbinu ya Jerry Murro rushwa haitokwishwa. Maana ni utamaduni wetu. Ni watu wangapi leo wanaweza kusimama kidete kuipinga rushwa ambayo ingeweza kumtoa mdogo wako aliyekamatwa kimakosa kwa kesi ya kubaka. Je akienda kufungwa haki itapatikanaje? Rushwa haitokwisha kamwe kama tabia zetu watanzania hazitabadilishwa. Na tabia za taifa zima haziwezi kubadilika kama hakuna misingi thabiti iliyowekwa na Uongozi wa taifa. Baba wa taifa hili alianzisha shule za watu wenye vipaji maalum na mwanafunzi wa mkoa wa mtwara alikwenda kusoma Arusha. Lengo alitaka kufanya watnzania tuchanganikane tufahamiane ana tuwe na umoja wa kitaifa. Hili alianzisha toka mashuleni. Na hili likifanywa leo na nchi yetu ana hawa viongozi wetu wenye upeo mdogo still mambo yataenda vyema kabisa.
Sorry for daring…
 
Hivi watu wakiambiwa mahandsome wapite mbele jerry nae atakwenda!!! Mmhh, sasa itabidi nielimishwe upya maana ya neno handsome. Tatizo la huyo dogo ni ulimbukeni wa umaarufu! Alitaka apande chat kwa kutumia sensitive issues ambazo yeye alidhani ni za kawaida. Mimi simwombei mabaya lakini hilo liwe funzo kwake kwamba pamoja uhuru wa habari bado hekima na busara vinahitajika katika kuamua habari gani iwe aired na kwa namna gani au habari gani isubiri muda mwafaka au habari gani isitangazwe kabisa.
Mkuu naona umekosea kidogo. Tuseme Asange (Wikileaks) na yeye anatafuta umaarufu?. Jerry ni mwandishi aliyethubutu kutumia taaluma yake kufichua rushwa zilizokithiri ndani ya jamii ya watanzania.
 
jamani wana jamvi la JF kuna mtangazaji alikuwa anaitwa JERRY MURO hivi yupo wapi....????
 
Hivi ni kwa niñi wanaharakati wengi wa bongo wakiminywa kidogo wanatulia hata kubenea wa ----------- nae simsikii
 
Back
Top Bottom