Jerry Silaa: Alex Msama ni tapeli namba 3 wa Viwanja, ajisalimishe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Promota wa Tamasha la Pasaka, Mtangazaji wa vipindi vya kwaya na Mgombea wa nafasi mbalimbali za uongozi huko CCM, Bwana Alex Msama ametajwa kuwemo kwenye 3 bora ya Matapeli Papa wa Viwanja DSM.

====


Your browser is not able to display this video.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amemtaka Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kujisalimisha kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es salaam akiwa na baadhi ya watu waliouziwa eneo la viwanja namba 1 kitalu 22 lililopo Kibada Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam ili kurejesha kwa wananchi eneo hilo lijengwa shule ya sekondari.

Silaa ametoa maagizo hayo alipofanya ziara katika eneo hilo Manispaa ya Kigamboni baada ya mgogoro huo kuwa wa muda mrefu kati ya wananchi wa eneo hilo na baadhi ya watu walionunua eneo la shule akiwemo Allex Msama.

Aidha, Waziri Silaa amemtaja Alex Msama kuwa ni tapeli namba 3 wa viwanja jijini Dar es salaam na tayari ameishaagiza baadhi ya maeneo anayoyamiliki kinyemela kunyang’anywa ikiwemo eneo la wazi na eneo la fukwe lililopo Mbweni Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

UPDATES
- Mfanyabiashara Alex Msama akamatwa kwa tuhuma za Utapeli wa Viwanja vya Tsh. Milioni 800
 
Mkimalizana nae katika hili Mamlaka nyingine imkamate kwa Kosa la Kudhulumu Mishahara na Stahiki za Wafanyakazi ( Waandishi wa Habari ) wa iliyokuwa Media ( hasa Gazeti ) akiongozwa na Marehemu Dada Yamola.
 
Kuna wana wanasema ooh rais muangalien jell slaa anaitia hasara serikarii,,, hahaha kumbe matapeli wenzao wanateteana oyaa jerry piga spanaa mdogo wangu japo kuwa umenizidi miaka 7 ila kaza hivyo hvy ukitoka hamia na kwa makonda mfuate huko huko pigaa spanaa
 
Jamaa ni tapeli mkubwa sana wa viwanja na amewashika watu wa ardhi wote hata huyo kamishna unaweza kukuta ni mtu wake so waziri akitaka kumkomesha msama adeal nae mwenyewe. Msama anaweza hadi kuiba viwanja vya serikali haogopi wanashirikiana na watu wa wizarani.

Ile wizara wangeifumua yite kuna majizi pale hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…