macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Waafrika na hasa watanzania tuna matatizo makubwa na ndio maana viongozi wanatuchezea sana. Hivi mtu alityekuwa hovyo na mpiga dili kama Jerry mnaona kweli yuko benchi kwa sababu rais ana kisasi nae na sio kwamba utendaji wake ulikuwa umejaa ufisadi na ubabaishaji? Kwanini umeamua ku-conclude kuwa tatizo ni ''kisasi'' na sio utendaji mbovu?JF kwa nondo hatari sana hii kitu ya 2012?
Safi sana, tumefahamu kwa nini Silaa bado yupo bench. Kumne kisa kilianza zaman eeh
Saint hilii n jipu ukiona anaogopa jue kuna mabango yamawahusu kiufupii wamepewa barua Leo NA hakika watajuta waliopokea helazao haojamaaSIKU moja baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kuamuru mabango yaondolewe barabarani, Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa amemtaka waziri huyo kuacha ubabe katika utekelezaji wa majukumu yake badala yake atumie vikao rasmi kutoa matamko yake.
Juzi wakati akizindua kituo cha daladala Mbezi, Dk Magufuli alitoa siku tano kwa wakala wa barabara (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam kuondoa wafanyabiashara na mabango yote yaliyojengwa pembezoni mwa barabara ili kukabiliana na msongamano.
Akizungumza ofisini kwake jana, Silaa alisema viko vikao vya bodi ya barabara na vya kamati ya ushauri ya mkoa ambavyo vyote vinaongozwa na mkuu wa mkoa na kwamba waziri huyo anaweza kuvitumia kupeleka hoja zake na kujadiliwa.
"Nchi hii siyo ya kwake na lazima atambue kuwa halmashauri zote ziko kisheria hivyo atumie vikao rasmi kutoa maagizo yake,"alisema Silaa. Alisema waziri huyo anatumia sheria ya barabara ya mwaka 2007 na kwamba kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo kulikuwapo na sheria nyingine ambazo hadi leo bado zinatumika hivyo anatakiwa aziheshimu.
Alisema miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini ni wenye mabango hivyo kutaka kuyaondoa ni sawa na kuhujumu maendeleo.Kwa mujibu wa meya huyo fedha za mabango zimekuwa zikitumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama shule, barabara na hospitali.
Alisema watu wenye mabango wana mikataba halali na halmashauri na wanaotangaza kwenye mabango hayo wana mikataba halali na wenye mabango hayo na kwamba kuyaondoa ni kusababisha usumbufu usiokuwa wa lazima katika mikataba hiyo.
Kuhusu suala la kutochaji ushuru katika kituo cha Mbezi, Meya huyo alisema suala hilo siyo sahihi kwani kuna gharama mbalimbali za uendeshaji ambazo zitatakiwa kulipwa.
Kwa mujibu wa meya huyo gharama hizo ni walinzi na uendeshaji wa choo ambao alisema zinaweza kulipwa na ushuru utakaokuwa unatozwa.
Katika hatua nyingine, halmashauri hiyo imesema itawashtaki wamiliki wa mabango ya biashara walioshindwa kulipa ushuru ambao unafikia Sh984 milioni. Silaa alisema karibu kampuni 20 zinadaiwa ushuru wa mabango na halmashauri hiyo zikiwamo kampuni ya simu za mkononi, kampuni ya vinywaji na kampuni zinazohusika kuweka mabango.
Alisema wameamua kuwashtaki baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na wamiliki hao ambao kila wanapofuatwa wamekuwa wakidai kuwa hawana fedha.
Mimi ni mpiga kura katika jimbo la Ukonga, hata angekuwa mgombea peke yake nisingempigia kura Jerry kwa sababu ninazozifahamu zingine zikiwa zimeishagusiwa hapa, lakini je, hoja aliyoitoa wakati ule bila kujali kama alikuwa ananufaika binafsi na mabango haikuwa na maana kweli?Huyu dogo mpiga dili sana...Siku ile walikesha na mwana wa mfalme kutaka kumrambisha mkwanja Waitara kule Ukonga,lkn Wakurya wauza mayai wa Kitunda walikuwa na panga viunoni wakimlinda Waitara kila anapooenda
Mpaka kunakucha vijana wa kijani hawaamini...Sogo Silaa aliupania sana Ubunge,alipotangazwa Waitara Dogo alilia kama kichanga kinatahiriwa...
Dogo alizidi dharau,anapiga kampeni Ukonga anaenda kulala Oystebay,muda wote wa Umeya haonekani Ukonga,
Kaiharibu Ilala,Round about zote kaweka maurembo ya mabati,unakuta badala ya kuweka bustani na maua halisi kupendezesha mji,kijikampuni chake kikachukua tender ya kuweka mamba wa madebe na mabati
Deal za kubeba takataka kupeleka Pugu akajigawia mwenyewe,matokeo yake Mitaa ikawa inanuka kwa uchafu maaana taka haziendi Pugu kwa wakati
Yeye na Antony Mavunde wakawa na ndoto za kuunda baraza jipya la Mawaziri,senzi kabisa kafisadi kasogo dogo haka!!Meya Ilala fukunyua wizi wa huyu mtu woooote
Haikuwa na maana zaidi ya kulinda maslahi yake kwenye pesa zitokanazo na mabangoMimi ni mpiga kura katika jimbo la Ukonga, hata angekuwa mgombea peke yake nisingempigia kura Jerry kwa sababu ninazozifahamu zingine zikiwa zimeishagusiwa hapa, lakini je, hoja aliyoitoa wakati ule bila kujali kama alikuwa ananufaika binafsi na mabango haikuwa na maana kweli?
....might b a reason to why,the man had nt selected him for dc appointment
Ni vizuri kutathimini tulikotoka. Je, Silaa anaweza kusema maneno yale leo? labda wakati ule, pamoja na mambo mengine, alikuwa na "kibri" cha "kubebwa" mahali fulani. Hata hivyo, ni kumkumbushia aliyekuwa waziri wa Ujenzi (ambaye sasa kapanda cheo kiofisi), KUSIMAMIA yaleambayo aliyaamini na "Akawekewa vingingi" na waliokuwa juu yake...Watu wana roho mbaya sana doo!! Mada ya 2012 leo 2016 ooophs