Jerry Silaa: Magufuli acha ubabe!

Jerry Silaa: Magufuli acha ubabe!

JF kwa nondo hatari sana hii kitu ya 2012?

Safi sana, tumefahamu kwa nini Silaa bado yupo bench. Kumne kisa kilianza zaman eeh
Waafrika na hasa watanzania tuna matatizo makubwa na ndio maana viongozi wanatuchezea sana. Hivi mtu alityekuwa hovyo na mpiga dili kama Jerry mnaona kweli yuko benchi kwa sababu rais ana kisasi nae na sio kwamba utendaji wake ulikuwa umejaa ufisadi na ubabaishaji? Kwanini umeamua ku-conclude kuwa tatizo ni ''kisasi'' na sio utendaji mbovu?
 
Huyu dogo mpiga dili sana...Siku ile walikesha na mwana wa mfalme kutaka kumrambisha mkwanja Waitara kule Ukonga,lkn Wakurya wauza mayai wa Kitunda walikuwa na panga viunoni wakimlinda Waitara kila anapooenda
Mpaka kunakucha vijana wa kijani hawaamini...Sogo Silaa aliupania sana Ubunge,alipotangazwa Waitara Dogo alilia kama kichanga kinatahiriwa...

Dogo alizidi dharau,anapiga kampeni Ukonga anaenda kulala Oystebay,muda wote wa Umeya haonekani Ukonga,
Kaiharibu Ilala,Round about zote kaweka maurembo ya mabati,unakuta badala ya kuweka bustani na maua halisi kupendezesha mji,kijikampuni chake kikachukua tender ya kuweka mamba wa madebe na mabati

Deal za kubeba takataka kupeleka Pugu akajigawia mwenyewe,matokeo yake Mitaa ikawa inanuka kwa uchafu maaana taka haziendi Pugu kwa wakati

Yeye na Antony Mavunde wakawa na ndoto za kuunda baraza jipya la Mawaziri,senzi kabisa kafisadi kasogo dogo haka!!Meya Ilala fukunyua wizi wa huyu mtu woooote
 
SIKU moja baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kuamuru mabango yaondolewe barabarani, Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa amemtaka waziri huyo kuacha ubabe katika utekelezaji wa majukumu yake badala yake atumie vikao rasmi kutoa matamko yake.

Juzi wakati akizindua kituo cha daladala Mbezi, Dk Magufuli alitoa siku tano kwa wakala wa barabara (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam kuondoa wafanyabiashara na mabango yote yaliyojengwa pembezoni mwa barabara ili kukabiliana na msongamano.

Akizungumza ofisini kwake jana, Silaa alisema viko vikao vya bodi ya barabara na vya kamati ya ushauri ya mkoa ambavyo vyote vinaongozwa na mkuu wa mkoa na kwamba waziri huyo anaweza kuvitumia kupeleka hoja zake na kujadiliwa.

"Nchi hii siyo ya kwake na lazima atambue kuwa halmashauri zote ziko kisheria hivyo atumie vikao rasmi kutoa maagizo yake,"alisema Silaa. Alisema waziri huyo anatumia sheria ya barabara ya mwaka 2007 na kwamba kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo kulikuwapo na sheria nyingine ambazo hadi leo bado zinatumika hivyo anatakiwa aziheshimu.

Alisema miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini ni wenye mabango hivyo kutaka kuyaondoa ni sawa na kuhujumu maendeleo.Kwa mujibu wa meya huyo fedha za mabango zimekuwa zikitumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama shule, barabara na hospitali.

Alisema watu wenye mabango wana mikataba halali na halmashauri na wanaotangaza kwenye mabango hayo wana mikataba halali na wenye mabango hayo na kwamba kuyaondoa ni kusababisha usumbufu usiokuwa wa lazima katika mikataba hiyo.

Kuhusu suala la kutochaji ushuru katika kituo cha Mbezi, Meya huyo alisema suala hilo siyo sahihi kwani kuna gharama mbalimbali za uendeshaji ambazo zitatakiwa kulipwa.

Kwa mujibu wa meya huyo gharama hizo ni walinzi na uendeshaji wa choo ambao alisema zinaweza kulipwa na ushuru utakaokuwa unatozwa.

Katika hatua nyingine, halmashauri hiyo imesema itawashtaki wamiliki wa mabango ya biashara walioshindwa kulipa ushuru ambao unafikia Sh984 milioni. Silaa alisema karibu kampuni 20 zinadaiwa ushuru wa mabango na halmashauri hiyo zikiwamo kampuni ya simu za mkononi, kampuni ya vinywaji na kampuni zinazohusika kuweka mabango.

Alisema wameamua kuwashtaki baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu na wamiliki hao ambao kila wanapofuatwa wamekuwa wakidai kuwa hawana fedha.
Saint hilii n jipu ukiona anaogopa jue kuna mabango yamawahusu kiufupii wamepewa barua Leo NA hakika watajuta waliopokea helazao haojamaa
 
Huyu dogo mpiga dili sana...Siku ile walikesha na mwana wa mfalme kutaka kumrambisha mkwanja Waitara kule Ukonga,lkn Wakurya wauza mayai wa Kitunda walikuwa na panga viunoni wakimlinda Waitara kila anapooenda
Mpaka kunakucha vijana wa kijani hawaamini...Sogo Silaa aliupania sana Ubunge,alipotangazwa Waitara Dogo alilia kama kichanga kinatahiriwa...

Dogo alizidi dharau,anapiga kampeni Ukonga anaenda kulala Oystebay,muda wote wa Umeya haonekani Ukonga,
Kaiharibu Ilala,Round about zote kaweka maurembo ya mabati,unakuta badala ya kuweka bustani na maua halisi kupendezesha mji,kijikampuni chake kikachukua tender ya kuweka mamba wa madebe na mabati

Deal za kubeba takataka kupeleka Pugu akajigawia mwenyewe,matokeo yake Mitaa ikawa inanuka kwa uchafu maaana taka haziendi Pugu kwa wakati

Yeye na Antony Mavunde wakawa na ndoto za kuunda baraza jipya la Mawaziri,senzi kabisa kafisadi kasogo dogo haka!!Meya Ilala fukunyua wizi wa huyu mtu woooote
Mimi ni mpiga kura katika jimbo la Ukonga, hata angekuwa mgombea peke yake nisingempigia kura Jerry kwa sababu ninazozifahamu zingine zikiwa zimeishagusiwa hapa, lakini je, hoja aliyoitoa wakati ule bila kujali kama alikuwa ananufaika binafsi na mabango haikuwa na maana kweli?
 
Haikuwa na maana zaidi ya kulinda maslahi yake kwenye pesa zitokanazo na mabango
Kama sheria ilishabadirishwa,na wao kama Halmashauri iliwapasa wawe wamebadili sheria zao ndogo ndogo zinazoongosha Halmashauri ili ziendane na sheria ya Nchi ktk maswala ya uhifadhi wa barabara
Kutotambua tu umuhimu wa kubadili ili kuendana na sheria tajwa kama takwa na hitaji muhimu la kisheria na kosa la kwanza,lkn kuendele kutumia sheria ndogo ndogo zinazokinzana na sheria kubwa kwa dhumuni la kuendelea kula ushuru/kodi ya mapato ni kosa la pili la kurambwa makofi
Lkn cha tatu ni hilo la kubisha wakati yeye ndio hajafikia hitaji la kisheria ni kosa la tatu ambalo linamfanya asifikiliwe hata ubunge maalumu wa nafasi za Rais
 
Jerry alijawa na kiburi na dharau.

Ni kijana aliyejawa na tamaa na ni mwizi.
 
might b a reason to why,the man had nt selected him for dc appointment
 
"Nchi hii siyo ya kwake na lazima atambue kuwa halmashauri zote ziko kisheria hivyo atumie vikao rasmi kutoa maagizo yake,"alisema Silaa. Alisema waziri huyo anatumia sheria ya barabara ya mwaka 2007 na kwamba kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo kulikuwapo na sheria nyingine ambazo hadi leo bado zinatumika hivyo anatakiwa aziheshimu.

....weeeeita lete mubia kiu mingi sana
 
Naona hata account yake ya Instgram siku hizi imedoda
 
Tumbua jipu hilo...alikua anajiona mungu mtu siku hizi hata clouds fm hawamwaliki kwenye vipindi vyao
 
Hakujua mtu aliekuwa anamuongelea kuwa ndo Rais. sasa sijui now anajisikiaje! ndo maana hata ubunge aliukosa dadadeki...!!!!!
 
Watu wana roho mbaya sana doo!! Mada ya 2012 leo 2016 ooophs
 
Silaa kashaJITUMBUA mwenyewe. Angekuwepo...HIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII! Hata hivyo kabwe katumbuliwa kwa niaba ya UOZO woooote uliokuwa DCC.....
 
Watu wana roho mbaya sana doo!! Mada ya 2012 leo 2016 ooophs
Ni vizuri kutathimini tulikotoka. Je, Silaa anaweza kusema maneno yale leo? labda wakati ule, pamoja na mambo mengine, alikuwa na "kibri" cha "kubebwa" mahali fulani. Hata hivyo, ni kumkumbushia aliyekuwa waziri wa Ujenzi (ambaye sasa kapanda cheo kiofisi), KUSIMAMIA yaleambayo aliyaamini na "Akawekewa vingingi" na waliokuwa juu yake...
 
Back
Top Bottom