Jerry Silaa: Serikali iweke Tozo ya Tsh. 100 kwenye mafuta yanayonunuliwa Dar ili Kupata Pesa za Kujenga Barabara za Jiji

Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 kwa siku ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil. 130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Slaa amesema Tsh 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana, akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
amepiga hesabu kubwa sana. amejua kabisa kuwa wapiga kura wake walio wengi hawamiliki magari au pikipiki, hata akikosa kura zao atapita tu ubunge. amesahau kundi la bodaboda ambalo mpinzani wake atakuja kuwatumia wapige horn kwamba alitaka mafuta yapande kwenye pikipiki zao.subiri 2025
 
Tatzo hizo b.130/= zitaibiwa tena kama alivyosema mkaguzi.
Halafu hizi hela watu wanapga zinaenda wapi walete basi hata huku kitaa tuzungishie.
 
SINA GARI,SINA PIKPIKI NA WALA SIENDAGI KWETU KWA USAFIRI WA GARI,ILA NAJUA NA NINA UZOEFU KUONA KILA MAFUTA(PETROL)IKIPANDA BASI KILA BIDHAA INAPANDA BEI.SASA WEWEKWA SHIBE YAKO UNAKUWA MTU USIE NA SHUKURANI,USIEPENDA WATU WALIOKUPIGIA KURA JIMBONI UKONGA,USITAKA KUJUA UMASIKINI ULIOKITHIRI WA WANANCHI WALIOPO JIMBONI KWAKO,USIEPENDA HATA KUTEMBELEA SEHEMU DUNI UKAIONEA ADHA WANAZOPITANAZO NA MAPUNGUFU MENGI AMBAYO UNASIMANGWA NAYO KILA UCHAO,.SIE WATU WA MVUTI TUNAOTUMIA BARABARA YA MVUTI DONDWE TUNAKUTAHADHARISHA KWAMBA BRBR HII ITAKUHARIBIA KTK MABOX YA KURA KAMA HUJAAMBIWA NA WANAOJIFANYA UKO NAO KARIBU.SITAKI KUKUELEZEA NJIA ILIVYO WALA SIWEZI KUPIGA PICHA MANA NATUMIA KISWASWADU,TOKA HUKO ULIKO NA FANYA NI DHARULA LEO AMA KESHO WAKATI HUU WA MVUA UTAELEWA NINACHOKUELEZEA "NINA HAKIKA UTAJITOA KWENYE HUO UWAKILISHI WAKO WA WABUNGE WA DAR"WA KUTAKA KUTUKAMUA.
 
Kuanzia leo naacha kufuatilia mambo ya nchii hii. kila siku linaiibuka jambo jipya na linaniuumiza hadi natamani nihame nchi.

Ila one day mambo yangu yakikaa poa ntaihamisha familia yangu na kun’goa mizizi yangu na kwenda kuipanda ulaya huko.

STUPID GAVAMENTI
Wahaya bhana[emoji1787]
 
Pesa zimeibiwa Sasa zichukuliwe kutoka wapi? Jerry ana hoja kumbuka hiyo ni specific Kwa Dar tuu.

Pia Vyanzo vingine sio sustainable,kama Sumbawanga wananunua bei kubwa kuliko Dar Kwa nini Dar msinunie bei sawa na wao tena Kwa faida yenu?
Hizi ni hoja za kipigaji Mwigulu alituletea tozo na matunda yake hatujayaona hadi leo.
 
Akichangia mjadala wa Bajeti ya TAMISEMI, mbunge wa Ukonga Jerry Silaa kwa niaba ya Wabunge wa Dar es Salaam amependekeza kwa Serikali iweke Tozo ya Shilingi 100 kwa mafuta yanayonunuliwa Jijini humo ili kupata Fedha za kujenga Barabara za Jiji la Dar es Salaam.

Jerry Silaa amesema amesema Jiji la Dar es Salaam linatumia zaidi ya Lita milioni 3 kwa siku ambazo zinaweza kuwezesha Jiji la Dar kupata Bil. 130 Kwa mwaka ambazo zitatumika kujenga Miundombinu ya Barabara ndani ya Jiji Hilo.

Aidha Slaa amesema Tsh 100 itakayoongezwa italeta msawazo wa bei na maeneo mengine ya Nchi ambayo yananunua mafuta Kwa bei kubwa sana, akisema formula yake ataiwasilisha Kwa Waziri wa Tamisemi na Wizara ya Fedha.

My Take: Jerry Silaa ana Hoja ya msingi na asikilizwe, nimeipenda ubunifu wake sio Kila kitu kusubiria mikopo.
HOJA YA KIJINGA MNATEUA WEZI KWENYE TAASISI NA HALMASHAURI WANATUIBIA HSLAFU MNATAKA WANANCHI WALAZIMISHWE KULIPA TOZO
 
SINA GARI,SINA PIKPIKI NA WALA SIENDAGI KWETU KWA USAFIRI WA GARI,ILA NAJUA NA NINA UZOEFU KUONA KILA MAFUTA(PETROL)IKIPANDA BASI KILA BIDHAA INAPANDA BEI.SASA WEWEKWA SHIBE YAKO UNAKUWA MTU USIE NA SHUKURANI,USIEPENDA WATU WALIOKUPIGIA KURA JIMBONI UKONGA,USITAKA KUJUA UMASIKINI ULIOKITHIRI WA WANANCHI WALIOPO JIMBONI KWAKO,USIEPENDA HATA KUTEMBELEA SEHEMU DUNI UKAIONEA ADHA WANAZOPITANAZO NA MAPUNGUFU MENGI AMBAYO UNASIMANGWA NAYO KILA UCHAO,.SIE WATU WA MVUTI TUNAOTUMIA BARABARA YA MVUTI DONDWE TUNAKUTAHADHARISHA KWAMBA BRBR HII ITAKUHARIBIA KTK MABOX YA KURA KAMA HUJAAMBIWA NA WANAOJIFANYA UKO NAO KARIBU.SITAKI KUKUELEZEA NJIA ILIVYO WALA SIWEZI KUPIGA PICHA MANA NATUMIA KISWASWADU,TOKA HUKO ULIKO NA FANYA NI DHARULA LEO AMA KESHO WAKATI HUU WA MVUA UTAELEWA NINACHOKUELEZEA "NINA HAKIKA UTAJITOA KWENYE HUO UWAKILISHI WAKO WA WABUNGE WA DAR"WA KUTAKA KUTUKAMUA.
Hawa Wabunge inapaswa walipe kodi ndio akili zitawakaa sawa. Nipo tayari kuchangia hiyo mia Moja ila tubadilishe sheria na adhabu, kuwepo na adhabu kali kwa hawa nakandarasi Fake. chukulia mfano kuna barabara ya Kimara Bonyokwa ilivyojengwa kijjinga. Adhabu iwe hukumu ya kifo na hawa Wabunge kama akina Slaa walipe kodi kila malipo wanayolipwa.
 
Wabunge nyie ni watu wabaya sana sana na niwanafiki sana

Mnawaza kuongeza mzigo tena kwa wananchi wakati hamja isimamia serikali katika matumizi ya hovyo inayo yafanya pamoja na wizi wa fedha za umma?

Mnataka nini kije kitokee ndio mjue wananchi wana majeraha makubwa sana mioyoni mwao ?
 
Hizo wanazoiba hawajatosheka nazo? Tupumzishwe kidogo jamani.
 
Hoja muflisi kabisa mpaka serikali ilipoamua kutoa ruzuku kwenye mafuta means walitaka mafuta yawe bei nafuu.

Kwa taarifa yake alitakiwa aje na means ya kupunguza bei na sio kuongeza. Kupungua kwa bei ya mafuta kutapunguza cost ya usafirishaji na hivyo kuleta impact kwenye bei za mazao.
 
Kwani ukiongeza sh.100 ni lazima bei itaongezeka? Soko la Dunia likishuka yatapungua na mia hutoona impacts yeyote.
 
Jerry alipota na upepo WA magu TU 2025 hatumpiii
Ukonga akae akijua kabisaaa
 
Back
Top Bottom