Pre GE2025 Jerry Silaa tunakuhitaji Ukonga kwa sababu zifuatazo

Pre GE2025 Jerry Silaa tunakuhitaji Ukonga kwa sababu zifuatazo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nikiwa kama Mwana Ukonga na mwananchi ninaejua siasa za Ukonga naomba nikiri kwa niaba ya wana Ukonga kuwa tunamuhitaji Jerry kuliko kitu chochote.

Hii ni kwa mustakabali wa maisha yetu, kubali kataa jimbo la ukonga ni miongoni mwa majimbo magumu ila sisi tuliozaliwa ukonga tunajua chanzo kiini na suluhu, ikumbukwe kuwa jambo la Ukonga lipo Wilaya ya Ilala, wilaya ambayo ni kubwa yaani inaanzia kariakoo mpaka chanika pia imepakana na kisarawe mkoa wa pwani kwa miaka yangu yote ambayo nimeishi ukonga nimegundua changamoto zifuatazo mosi ni miundo mbinu.

Tatizo la miundo mbinu ni kubwa kuliko tunavyofikiri kwani wakati wa masika watu hulazimika kupanga vyumba mjini kuepuka changamoto za usafiri ambapo huwa hakufikiki hapa naongelea maeneo kama mbondole,viwege, magole chakenke nk kwa watu wasio na akili lawama hizi huwa wanamtupia mbunge.

Bila kujua historia ya jambo husika wala kujua taratibu za serikali na michakato ya kumpata mzabuni nk, sababu ya kuwaelekeza wana ukonga kwamba tunamuhitaji Jerry ni kwamba huyu jamaa amekuwa jikoni kwa muda mrefu tangu akiwa Naibu Meya baada ya hapo amekuwa mjumbe kamati kuu ya chama.

Yaani jikoni kabisa hii imepelekea mpaka Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amiri jeshi mkuu kumuamini na kumpa uwaziri katika wizara nyeti sana ya ardhi, wana ukonga Mungu atupe nini tena ukizingatia maeneo yote niliyoyataja hapo juu yana migogoro ya ardhi mpaka kupelekea baadhi ya maeneo kuitwa maeneo ya uvamizi.

Mimi nashauri tuendelee kumng'ang'ania huyu home boy kwani yeye ndiye atatuvusha na kutupeleka nchi ya ahadi sababu ukonga anaijua vizuri na pia anaushawishi mkubwa hata kwa mkuu wa nchi na mamlaka zote, tusiache lulu hii ipotee.. kumbuka amepewa dhamana ya ardhi nchi nzima ya Tanzania.

Jimbo la Ukonga litakuwa tofauti baada ya muda mfupi sana.

Naomba kuwasilisha
Unapima upepo hatukutaki Wana ukonga kagombee KWENU unakoishi msasani
 
Labda kwa haraka haraka nikusaidie maeneo ya uvamizi, yenye kesi au hukumu imeshatoka tayari ukitoka pugu sekondari baada ya kupita reli mkononwa kushoto kama unaelekea viwege yale maeneo yana mgogoro kitamboo na hukumu ishatoka tayari ikifika njia nne mbondole kama unaelekea ofisi za serikali ya mtaa hukumu imetoka na waliovunjiwa walivunjiwa ving'ang'anizi walibaki kuna eneo linaitwa uvikiuta pia greda lilipita ila kuna wabishi bado wapo ambao ndiyo wanakuja na matusi humu kudaibwanataka barabara ukifika mbondole kuna kesi kubwa ambayo imezimwa kisiasa kwa kuwataka wamiliki wa sasa walipe fidia ila kiukweli hii kesi itaibuka muda siyo mrefu kwani mh Lukuvi alipokuwa waziri wa ardhi alimaliza kwa hekima zake hapantunazungumzia kaya elfu tatu...binafsi nina mchoro wa kutoka ardhi wa maeneo yote haya ambapo unakuta jitu limejenga kwenye let say pb (public building) halafu ndiye wa kwanza kutukana viongozi eti anataka barabara
Eneo la viwanda halihitaji barabara?
Hivi maendeleo yanafata watu au watu wafuate maendeleo.

Maeneo uliyoyataja ni machache kuwa yamevamiwa, ila kwa nini kusipo vamiwa napo hakuna miundombinu?

N.B Jimbo la ukonga limepakana na wilaya mbili za mkoa wa Pwani ambazo ni Kisarawe na Mkuranga.
 
Eneo la viwanda halihitaji barabara?
Hivi maendeleo yanafata watu au watu wafuate maendeleo.

Maeneo uliyoyataja ni machache kuwa yamevamiwa, ila kwa nini kusipo vamiwa napo hakuna miundombinu?

N.B Jimbo la ukonga limepakana na wilaya mbili za mkoa wa Pwani ambazo ni Kisarawe na Mkuranga.
Kama mmevamia industrial area maana yake hamna uhalali wa kulalamika pia hamjui wa kumlalamikia mnaenda kumsumbua mbunge ambaye Ana majukukumu tofauti kabisa..
 
Miye labda sijui, jukumu la mbunge ni kutengeneza barabara? Au ni jukumu la tarura? Barabara zinatengenezwa kwa fungu lipi? Labda tuanzie hapo kabla ya kuanza lawama ..binafsi naishi viwege kwa mpemba mwaka wa 13 sasa kabla ya hapo nilikuwa naishi mzambarauni kwa miaka 10 na ni muathirika mzuri tu wa hizi barabara huwa inanilazimu kupanga chumba mjini ili niwahi kibaruani lakini sijawahi kuona kosa la mbunge kwani huku nilihamia mwenyewe kwa utashi wangu...na nilipokuja kugundua haya maeneo mengi ni ya uvamizi huwa naomba tu Mungu huruma ya serikali kwa wananchi wake lakini mbunge hahusiki na lawama zozote
Uko sahihi. Mbunge kazi yake kubwa ni kupokea Posha na Mshahara. Akijitahidi sana abwabwaje na kuunga mkono hoja kwa 100% Bungeni. Baada ya miaka mitano tutapanga tena foleni kumchagua. Kero zetu hazimhusu asilani.
 
Nenda kaishi mbezi kuna lami kila mtaa...huwezi ukaja sehemu ukaanzisha mji kisha unamlaumu mbunge on a personal capacity kwani yeye ndiye alikwambia uhamie huko....
Alikujeje kuomba kura kwenye mji/makazi yalioanzishwa kiholelela??
 
Kama mmevamia industrial area maana yake hamna uhalali wa kulalamika pia hamjui wa kumlalamikia mnaenda kumsumbua mbunge ambaye Ana majukukumu tofauti kabisa..
Ilaumu Serikali kwa kuweka jimbo maeneo haramu na Mbunge kugombea maeneo haramu
 
Uko sahihi. Mbunge kazi yake kubwa ni kupokea Posha na Mshahara. Akijitahidi sana abwabwaje na kuunga mkono hoja kwa 100% Bungeni. Baada ya miaka mitano tutapanga tena foleni kumchagua. Kero zetu hazimhusu asilani.
Come clear chief tuache ushabiki tuache mihemko wajibu wa mbunge ni nini?
 
Maskio popo Jerry Slaa umeamua kuja kivingine hapa.

Wewe ni mbunge wa ovyo kuwahi kutokea katika historia ya bunge la tz.
 
Maskio popo Jerry Slaa umeamua kuja kivingine hapa.

Wewe ni mbunge wa ovyo kuwahi kutokea katika historia ya bunge la tz.
Jerry ni kama maji usipoyaoga utayanywa usipoyanywa utanawa huna namna aisee we jipendekeze tu usaidiwe
 
Kule ni temeke Jerry tena kutokea mjini ni karibu kupitia buza unakuja huku ukonga kutafuta nini?
Huu ni Ujinga sasa. Unadhani wote wameajiriwa? Kama una Biashara Banana au una Bucha Machinjio yako wapi??
 
Ni kutuwakikisha wapiga kura kuhusu changamoto za Kijamii zinazotusibu ikiwa ni pamoja na ubovu wa Miundombinu
Wanaitwa law makers, it is high level of illiteracy to blame a law maker in such a mess
 
Back
Top Bottom