Uchaguzi 2020 Jesca Kishoa Kafulila kuchukua fomu kugombea Ubunge CHADEMA Iramba ni kejeli na dharau kama si matusi kwa vijana wenzako

Mume wake ni RAS sidhani kama atadumu CDM, CDM watafute mtu mwingine tofauti ya huyu muda wowote ataunga mkono juhudi.
Na namna ni kumpitisha huko kwenye mchakato then CHUJIO limabakiza
 
Nakushauri utulie tulii mwacheni mama wa watu apiganie haki yake.

Ukitaka mbunge aliye yafanikisha yoote hayo uliyo muuliza mh Kishoa huwezi kumpata kamwe.
Haya maswali yaamhusu Jesca pekee..nitamuulizaje mtu mwingine!Tanzania Kuna tabia ya ajabu eti mwanasiasa wa upande wako akikisolewa ni nongwa !Nilichowasilisha kuhusu Hali kisiasa kuhusu Jimbo hili ni sahihi!
Ndio maana wengi mnaopinga hata Iramba hamuijui Bali mna mahaba na CHADEMA,...kama.mimi!Ila namkosoa Jesca kwa matendo take bila kificho wapa haya kwa maslahi ya Demokrasia!
Ndio maana si mfuasi wake au hata yeye anaweza kutia timu hapa kuja kujibu hoja chache nilizowasilisha!
 
Wew mnafki umetumwa na Mwigulu
Huyo mwigulu yeye kafanya nini kwa wana Iramba

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Mkuu acha mihemko....hapa hatumzungumzii Mwigulu....hivi shule mlienda kusomea Nini!
Hii ndio changamoto na ujinga tulio nao!
Akikisolewa Chadema tuna nuna....!
Nikikuambia Mwigulu huwa anashindaje utaona mantiki yangu!
Hivi unajua kuwa Jesca alifanya Kampeni takribani siku kumi tu!
Ni mahaba tu ya watu ndio yalimpa zile kura!
Nakuhakikishia Kama Jesca angeamua kurudi vijijini...kunywa mtukura,togwa,kuzika,kusali,kucheza ngoma,kufanya mijadala na wanafunzi,kuunda vikundi vya kina mama na bodaboda !Mwigulu angekuwa mwepesi mno!
Siasa na Sayansi....kihistoria Iramba ilikuwa na uchifu/mtemi usio na nguvu Sana ktk maisha ya watu!Hali hii bado ipo kwenye damu za wengi!
Unahitaji akili kubwa kuwapata watu Hawa!...Mwigulu anajua hili!
Afu ukome kuninasibisha na Mwigulu!
 
Hii ni barua kwenda kwa Jesca; hapa inafanya nini!
 
Jesca hana muda wa kujibishana na gamba moja fulani
 
Kama vile nakuelewa
 
Andishi lako lingenoga sana kama ungeainisha pia yafuatayo:
1. Wabunge wa Upinzani (Akiwepo Jesca) wamezuiwa kabisa kabisa kufanya siasa
2. Wabunge wa Upinzani (Akiwepo Jesca) wamekutwa wakishinda mahakamani kwa kesi ambazo hata wewe unaelewa kama ni za kubumba au za haki
3. Wabunge wa Upinzani wamekuwa wakibanwa sana bungeni
4. Jesca Kishoa Kafulila alipeleka michango na vitu jimboni Iramba alikataliwa na aliyekataza sio mpokeaji bali mamlaka
5. Jesca Kishoa ni MBUNGE WA MKOA WA SINGIDA sio MBUNGE WA Iramba na katika kutetea Wana Singida Jesca AMEONGOZA KWA MICHANGO MINGI BUNGENI kuliko hata Martha Mlata wa CCM mwenye title kama yake
6. Jesca ni miongoni mwa Wabunge walioshindwa KUNUNULIKA
7. Jesca katika kutetea HAKI na DEMOKRASIA alikuwa tayari hata ndoa yake itetereke. Thanks God hekima imetangulia ndoa angalau inaonekana ipo IMARA.
8. Jesca amefungua ofisi ya Mbunge Iramba na ameweka mtumishi anayesikiliza kero za wananchi kama wabunge wengi wanavyofanya
9. Jesca anasomesha watoto katika shule kadhaa nchini wanaotokea Singida.
10. Mume wa Jesca pamoja na uanaume wake alikubali kuingia 'KINGI' (Rejea alichokisema Nasari kwenye Ile flash aliyonayo ya wanachadema wanaohamia CCM) lakini Mtoto wa Kike 'kakomaa' na Upinzani. ANAPASWA APONGEZWE angalau kwa UJASIRI tu kuliko kutengeneza threads za MAJUNGU kama hizi.
 
Ahsante Sana Kabwela.....amini usiamini Jesca angeweza kufanya zaidi ya hayo na kujijenga mno....ndani ya udikteta wa awamu ya Yesu! lakini alikosa nia,dhamira Kama so weledi!
Lakini maadam anagombea na Shetani ,wacha Mungu tutajua tutafanyaje!
Hata hivyo Kabwela Mimi sijaandika majungu....huu Ni ukweli...Ni lazima tuiishi!
Jesca anajua wazi na hawezi inuka kukanusha haya....ndio maana nimeandika mwishoni kuwa kwa heshima ya Demokrasia na Chama tumueleze hayo ajifunze!
Mimi kimsingi sikudhani Kama Jesca atarudi Iramba!
 
Sijaelewa huyu jeska yupo chadema au CCM na je ndio mme wa tumbili?
 
Mwendo mdundo dadangu!! As long as wana CDM wanakukubali na chama kimeshakubali hayo maneno hata kwenye khanga yapo!!
 
Jesca Kishoa na wafuasi wako bado mnao huu Waraka!
Najua mliutupa sasa nawakumbusha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…