Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Mbunge Jesca Magufuli amesema mikopo pekee kwa vijana haitoshi, isipokuwa wanahitaji kujengewa uwezo ili wanufaike na mikopo hiyo.
ELimu kama ya utunzaji wa fedha na namna ya kuanzisha biashara ndio itawafanya wanufaike na mikopo hoyo
=====
Mbunge wa Viti Maalum, Jesca Magufuli, amesema kutegemea mikopo ya Serikali pekee hakutoshi kuwawezesha Vijana kiuchumi bila kuwepo kwa mfumo jumuishi wa ujasiriamali unaowaongezea ujuzi na uwezo wa kuzitumia fursa zilizopo.
Amesema hayo alipokuwa akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kwa mwaka wa fedha 2026/27, akisisitiza kuwa pamoja na jitihada za Serikali kutoa mikopo, bado kuna haja ya kuwekeza zaidi katika kuwajengea Vijana uwezo wa kujitegemea.
“Ni kweli Serikali inatoa mikopo kwa Vijana, lakini bado hatuwezi kutegemea mikopo tu, najua ni ukweli mchungu lakini lazima tuongee, hatuwezi kutegemea mikopo kuwawezesha Vijana hawa na mikopo hii ili Kijana aweze kunufaika kibiashara lazima tuwe na mfumo jumuishi wa ujasiriamali kwa Vijana wetu wa taifa hili la Tanzania na tunapozungumzia mfumo huu wa ujasiriamali, lazima tuwajengee uwezo Vijana hawa.” Jesca Magufuli.