GE2025 Jesca Magufuli: Nitakuwa sauti ya vijana na kuwatetea

GE2025 Jesca Magufuli: Nitakuwa sauti ya vijana na kuwatetea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ndo maana alifanya interview na Millardayo ili asikike .

Uwezo mdogo kuanzia kichwani mpaka kujieleza MTU kapata four ya mwisho ya 37 then anataka ubunge. Ili akatunge Sheria.
Wivu huo mkuu,kupata four. O level haina maana mtu hana akili,vipi wale darasa la 7 waliolo bungeni na wanatunga sheria😁
Huyo Dada ana masters kwa sasa
 
Nas
She is very composed. Namshangaa kwa nini baba yake hakumpa nafasi ya uongozi mapema. Unaweza kuwa na uwezo lakini Kiongozi akawa anaogopa nepotism ndicho kilichomkumba huyu Binti alistahili kuwa bungeni siku nyingi
NAshangaa wengine wanamtukana
 
All the best Jesca Magufuli.
Tuna imani ana chembechembe ya uzalendo kama Baba yake.
 
Wivu tu 😂
Sio wivu.
Mh Balozi aliyejiuzuru ndugu Polepole ameweka wazi kwamba keki ya taifa ni ndogo sana hivyo ki busara haifai watu wa familia moja wakajikatia kipande chote wao peke yao. Asante
 
Mgombea Ubunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Vijana, Jesca Magufuli (29), ameomba kura mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, akiwani nafasi mojawapo kati ya sita zinazogombewa upande wa Tanzania Bara.

Jesca ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Siasa na Utawala.

Amesema ana dhamira ya kweli ya kuwatetea vijana na kuwa sauti yao kupitia maono na mwelekeo alionao.

Mkutano huo Maalum wa UVCCM unafanyika leo, Agosti 1, 2025, jijini Dodoma kwa lengo la kuwachagua Wabunge wa Viti Maalum kundi la Vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia kundi hilo


View attachment 3427140
Dah kafanana na Baba yake hadi kucheka
 
Itungwe sheria kali watoto wote wa viongozi wastaafu wa serikali, marufuku kugombea nafasi yoyote ya uongozi hadi ipite miaka 25.
Kwahyo viongozi wakatunge sheria ya kuwabania watoto wao wasiwe viongozi..!?? 😅😅

Hata ungekuwa ndio kiongozi ungetunga sheria hio..!??
 
Haya vijana sauti hiyo mnaletewa

Hivi peneza yuko wapi hajalaa shavu

Ova
 
Mgombea Ubunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Vijana, Jesca Magufuli (29), ameomba kura mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, akiwani nafasi mojawapo kati ya sita zinazogombewa upande wa Tanzania Bara.

Jesca ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Siasa na Utawala.

Amesema ana dhamira ya kweli ya kuwatetea vijana na kuwa sauti yao kupitia maono na mwelekeo alionao.

Mkutano huo Maalum wa UVCCM unafanyika leo, Agosti 1, 2025, jijini Dodoma kwa lengo la kuwachagua Wabunge wa Viti Maalum kundi la Vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia kundi hilo


View attachment 3427140
Nchi hii sasa imegeuka kuwa ya kifalme. Kila mtoto wa mtawala naye anatamani kutawala. Nchi ya kipuuzi sana hii.
 
She is very composed. Namshangaa kwa nini baba yake hakumpa nafasi ya uongozi mapema. Unaweza kuwa na uwezo lakini Kiongozi akawa anaogopa nepotism ndicho kilichomkumba huyu Binti alistahili kuwa bungeni siku nyingi
Awe bungeni kwa lipi mkuu? Huyu naye ni mpuuzi tu kama wapuuzi wengine. Unajua hayo maneno machache aliyosema hapo ametumia muda gani kuyakariri?
 
Kwahyo viongozi wakatunge sheria ya kuwabania watoto wao wasiwe viongozi..!?? 😅😅

Hata ungekuwa ndio kiongozi ungetunga sheria hio..!??
Upo uwezekano huo mkuu, kinachohitajika hapo ni political will. In fact wakiweka zuio hilo wanajiondolea maadui wa familia zao wasio wa lazima.
 
Back
Top Bottom