Mgombea Ubunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Vijana, Jesca Magufuli (29), ameomba kura mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, akiwani nafasi mojawapo kati ya sita zinazogombewa upande wa Tanzania Bara.
Jesca ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Siasa na Utawala.
Amesema ana dhamira ya kweli ya kuwatetea vijana na kuwa sauti yao kupitia maono na mwelekeo alionao.
Mkutano huo Maalum wa UVCCM unafanyika leo, Agosti 1, 2025, jijini Dodoma kwa lengo la kuwachagua Wabunge wa Viti Maalum kundi la Vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia kundi hilo
View attachment 3427140