Chief Sanze
JF-Expert Member
- Jun 13, 2014
- 1,668
- 3,736
Yaani ulivyoenda kumuuliza ndiyo kakuongezea uongo mwingine na kukuhakikishia hoja ya Hussein kuwa ndiye mtume wa mashia! Kweli wewe kiazi.Shia ni swala tatu na siyo tano kama nyinyi na pia wanaamini Hussein ndo mtume wa mwenyezi Mungu kwa kizazi cha Waislam na si Muhammad, endelea kubisha.
Ni kwamba hakuna Muislamu anayeswali chini ya swala tano kwa siku,Wao Mashia wanachokifanya kuna baadhi ya swala wanaziunganisha mfano wakiswali swala ya adhuhuri wanaswali na swala ya alasiri na kuhusu Hussein si kama wao ndiyo wanaamini ndiye mtume badala ya mtume Muhammad isipokuwa wao wanaamini baada ya Mtume kufariki aliyestahili kuwa badala yake yaani kiongozi wa umma wa Waislamu(Khalifa) ni huyo Hussein mjukuu wa mtume kwa mtoto wake kipenzi Fatma lakini wengine waliona waliostahili kuchukua nafasi ya Mtume ni maswahaba wake kina Othman,Omar,Abubakar na wengineo, hivyo ndivyo ilivyo asikuongopee mtu.