Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Takriban kwa wiki tatu sasa jeshi la Israel limekuwa likipigana vita vikali vya mtaa kwa mtaa maeneo ya kaskazini ya Gaza.
Mwishowe jeshi hilo lilitanga hapo juzi kuwa limedhibiti kambi yote ya Jabalia ambayo imewapa shida kuishida tangu mwanzo wa vita.
Watu wengi walikufa kwenye mji huo na waliofukiwa chini ya vifusi haikuwa rahisi kuwaokoa kwani kwa kutumia helkopta maalum aina ya qudrapt jeshi la Israel liliwafukuza waliosogelea maeneo yaliyobomolewa.
Kwa mshangao leo tena jeshi hilo limeonekana kuachia maeneo hayo na kurudi nyuma huku wapalestina waliobaki hai wakionekana kusonga mbele kwenda kuwatafuta wenzao waliofukiwa
Hilo linatokea kabla ya jeshi hilo halijafanikiwa kuichukua mitaa ya Beit Zeitoun iliyotangaza kuwa na mpango wa kuidhibiti maeneo hayo hayo ya kaskazini ya Gaza.
Hali hii si ishara nzuri kwa Israel kwani kweli wanafanikiwa kuua na kubomoa majumba kutokana na kumiliki vifaa vya kisasa vya kivita, lakini kama ilivyotabiriwa mwanzoni hakuna uwezekano wa kutawala maeneo ya Palestina kama inavyokuwa kiutawala wa kawaida kwenye maeneo yanayokaliwa na nchi.
Kwa maana hiyo vita kati ya Israel na Palestina chini ya Hamas havitaweza kutangazwa kuwa vimemalizika.