Hakuna jipya zaidi ya waasi kuondoka.
Kipindi cha JK, hawa M23 walikuwa kama 600 kwa idadi ila walileta balaa zito. M23 wala sio wengi sana sababu Rwanda sio nchi tajiri kuweza kuwagharamia.
M23 ina silaha nzuri kwa sehemu sababu zinatoka Rwanda, ukijumrisha na mafunzo walopokea jeshini Rwanda ndo ikawa fimbo kwa Congo. Jeshi la Congo nidhamu hakuna kabisa, hata JKT ya kwetu ikipewa silaha inainyoosha vizuri tu Congo.
Kwahiyo Idadi yao kuwa chache, silaha pia walikuwa nazo kwa sehemu, ikapelekea SADC kuunda kikosi kipana zaidi kuelekea vita ile. SADC ikatoa Brigade moja, askari wasiopungua 3,000 wakipewa baraka zote na UN pia, wakaenda Goma. M23 hawakuweza kutumia silaha kali zaidi kwani ingezidi kudhihirisha wanapewa msaada na Kagame na kumbuka kipindi hiko Kagame ndo alikuwa mshukiwa namba 1 kufadhili genge hilo, mpaka UN ikamtaja Kagame ndio anawafadhili jamaa hao.
Sasa hapo endapo EAC ikaunda majeshi yake kwa idadi kubwa kama ya kwanza na silaha pia. M23 watakimbia kama walivyokimbia mara ya kwanza. Kipindi kile walipoona vita imekuwa ni nzito, hasa mizinga iliyokuwa inapigwa na JWTZ wakaamua waachie Goma, hasa ule mlima waliougeuza kuwa ngome yao. Hawapendi kufa, wanapoona wamezidiwa huwa wanakimbia, idadi ya vifo kwao sio kubwa sana, hawataki kufa sababu wakifa wanajua wanatia hasara kwa serikal ya kwao Rwanda.