Jeshi la Polisi: Aliyedaiwa Kutekwa aliuza gari alilokodi Ili kulipa madeni ya harusi.Uchunguzi unaendelea kubaini Alikopotelea

Jeshi la Polisi: Aliyedaiwa Kutekwa aliuza gari alilokodi Ili kulipa madeni ya harusi.Uchunguzi unaendelea kubaini Alikopotelea

Unazijua taratibu za kuuza gari, na umewahi kuuza au Kununua gari kwa mtu? Na kusema wewe ni jirani na huyo Massawe unadhani itashawishi unavhokisema kiwe halali? Kwanini hujaandika habari za Massawe immediately baada ya kurepotiwa kutoonekana?
Gari kakutwa nayo mtu anadai aliuziwa na huyo massawe na alimpa milioni nane ili akimalizia milioni moja amkabidhi gari Mimi ni jirani na huyo massawe na mpaka polisi wanakuja kuchukua mkewe nilikuwepo.

Wewe unakataa gari halikuuzwa kivipi?
 
Gari kakutwa nayo mtu anadai aliuziwa na huyo massawe na alimpa milioni nane ili akimalizia milioni moja amkabidhi gari Mimi ni jirani na huyo massawe na mpaka polisi wanakuja kuchukua mkewe nilikuwepo.

Wewe unakataa gari halikuuzwa kivipi?
Swali la ziada kama alimpa hiyo milioni nane Ili akimaliza Moja amkabidhi gari, means Massawe alibaki na gari including the documents, sasa iweje tena polisi wakamate gari hiyo hiyo kwa mtu aliyeuziwa? Na isikutwe kwa Massawe?
 
Polisi wanaendelea na uchunguzi kufahamu kama Mtu aitwae Vincent Peter Massawe wa DSM amejipoteza mwenyewe kwa makusudi ama la, ikiwa ni siku kadhaa toka Ndugu zake watangaze kupotea kwake.

Taarifa ya Polisi imesema Jeshi hilo lilipokea taarifa za kupotea kwa Vincent siku chache baada ya harusi yake ambapo imebainika amekuwa akidaiwa zaidi ya Tsh. milioni 65 na Watu tofauti, hivyo wanachunguza kama amepotea kweli au amejipoteza sababu ya madeni.

“Kufuatia taarifa hii inayosambazwa katika Mitandao ya Kijamil, Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kulingana na ushahidi uliokusanywa kupitia kwa Watu mbalimbali na kupitia uchunguzi wa kisayansi uliokwisha fanyika hadi sasa, ni kweli taarifa za kupotea kwa Vincent Peter Massawe zilifikishwa Kituo cha Polisi Kigamboni Noveember 19,2024 na Mke wake” - Polisi.

“Upelelezi ulianza mara moja na kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwa na harusi November 16,2024 na baada ya harusi alitafuta gari ya kuwarejesha Ndugu zake na Wageni wengine Moshi Mkoani Kilimanjaro, ushahidi mwingine uliopatikana ni kwamba wakati wa maandalizi aliazima gari ( T 642 EGU Toyota Ractis) kutoka kwa Jamaa yake ili imsaidie katika shughuli za harusi lakini hakulirejesha gari hiyo kwa Mwenyewe na badala yake November 18,2024 ambayo inadaiwa alikuwa anafuatiliwa na gari ambayo alikuwa anaitilia mashaka ndiyo siku hiyohiyo aliuza gari hiyo kwa kiasi cha shilingi milioni 9 na akalipwa milioni 8 ikabaki milioni moja “

“Taarifa iliyopo inaonyesha kuwa siku hiyohiyo alimtumia Mke wake kiasi cha fedha ili alipe madeni mengine yaliyotokana na harusi ikiwepo Coaster aliyokodisha kuwarejesha Wageni wake Moshi, gari hilo aina ya Toyota Ractis limefuatiliwa na limekamtwa, ushahidi mwingine unaonyesha huyu Vincent Peter Massawe pia anadaiwa na Watu wengine wawili mmoja kiasi cha milioni 53 na mwingine milioni 16, ukweli wa tukio hili utafahamika muda si mrefu kama amejipoteza au laah kulingana na mtiririko wa ushahidi ulivyo na hili linategemea hasa tukipata ukweli kutoka kwa Mke wake kwani inadaiwa anao ufahamu mkubwa wa jambo hili, mwisho Umma utajulishwa taarifa zilizo sahihi kuhusu Peter Masawe” ——— Polisi.
....Hii ni Taarifa ya Kisayansi au Kiitelinjesia ya Polisi ??...
 
Gari kakutwa nayo mtu anadai aliuziwa na huyo massawe na alimpa milioni nane ili akimalizia milioni moja amkabidhi gari Mimi ni jirani na huyo massawe na mpaka polisi wanakuja kuchukua mkewe nilikuwepo.

Wewe unakataa gari halikuuzwa kivipi?
Mbona hii statement yako haielewki!? Gari kakutwa nayo mnunuzi ambae alikua akabidhiwe gari baada ya kumalizia M1 which is which!? Sasa kakabidhiwa vp bila kumalizia hiyo M1 anayo daiwa!!??
 
Kupenda sifa kunawagharimu wengi sana, sioni haja ya kufanya jambo kwa gharama ambazo zipo nje ya uwezo wako.
Umesioma taarifa ya Polisi halafu ukarelate na mazingira halisi? Yaani application.
Tufanye upo darasani, hiyo taarifa ni knowledge halafu tukio lenyewe ni context! Ukifanya application Kuna uhusiano? Mana yake inatakiwa uchukue taarifa na ulifanyie reflection katika ulimwengu halisi (real life situation)
Utaratibu wa kukodi gari upoje?
Ukikodi gari unapewa na dereva kama bwana harusi unakua hupewi dereva au unapewa?
Ukikodi gari Kuna masharti ya kukabidhiwa documents halisi za gari?
Unapouza gari je unauza gari bila Nyaraka halisi Kwa ajili ya kukamilisha taratibu za transfer of ownership?
Ukiangalia siku ni chache sana, je alijiandaa na kutafuta mteja wakati wa harusi na kabla hajakodi gari Ili kwamba baada tu ya harusi auiuze hiyo gari?
Je aioa Kwa sababu Gani kama lengo ni kufunga ndoa kuuza gari ya watu na kutokomea huku akiacha ndoa mbichi nyuma?
Polisi wanasema alimtumia mke kiasi Fulani Ili alipe madeni! Means polisi Wana uwezo wa Kuomba kibali na kuingilia taarifa za transaction za mke au Mume, kwanini waseme ni Kaisi Fulani na sio exact amount?
Kiutaratibu anayeandaa harusi ni bwana harusi, iweje mke ambaye hakushiriki au alishiriki kwenye kukopa ahueishwe kwenye kulipa madeni?
Kwa Hadi anayoonekana nayo bwana Harusi ni mfanya biashara, unadhani ni rahisi kwa yeye kukupa Kwa ajili ya harusi as per navyowajua wachaga linapokuja swala la harusi tena la mnama wao?
Polisi wanaelezaje hiyo harusi ilikua special namna Gani kutofautisha na nyengine?

Kulikua na haja Gani ya jamaa kutoa taarifa ya kufuatiliwa kama alikua na Nia ya kutoweka mazima? Alishindwa Nini kupotea kimya kimya?
Polisi wanajua nchi hii Ina mazuzu wengi wasiokua na uwezo wa kuhoji chochote na hivyo hupokea taarifa zao na kuzisambaza zilivyo.
Polisi wametoa taarifa ya Abdul Nondo mpaka sasa hivi?
Una taarifa za yule Mangi wa kiluvya na kinachoendelea mpaka sasa hivi
Una taarifa za abduction na execution ya Ali Kibao mpaka sasa hivi?

Huoni kwamba polisi Huwa wanakuja hadharani haraka hasa baadhi ya evidence zikitajwa mathalani namba za magari? Huoni wamekuja haraka na kire-position gari kama ilivyofanyika kwa Abdul Nondo?
Kama taifa Inabidi kuwanyoshea polisi kidole kwa kushindwa kutimiza wajibu wao na kugeuka state robers!
 
Ila mnunuzi ndiyo anakua kwenye hatari kubwa sana ya kupoteza maana utaratibu wa manunuzi haukufuatwa ipasavyo!!
Hakuna uuzaji Wala ununuzi wa gari Kwa muda mfupi namna hiyo!
Hata mtu akileta hoja ya kwamba gari ilikua inaenda kukatwa scraper! Lazima ujiulize, gari mpya inaenda kukatwa scrap?
Kama NDIYO Kuna taarifa yoyote ya mkodishaji kulalamika popote kutokurudishiwa gari yake as per Makubaliano ya mkataba wa kukodi? Au taarifa yoyote ya kutaka kuongezewa muda?
Dereva aliyepewa kupngozana na gari?
Kwanini isiwe kesi ya wizi wa kuaminika?
Kwanini isiwe kesi ya wizi wa gari?

Hii kwangu Bado ni cover story ya polisi.
 
Mbona hii statement yako haielewki!? Gari kakutwa nayo mnunuzi ambae alikua akabidhiwe gari baada ya kumalizia M1 which is which!? Sasa kakabidhiwa vp bila kumalizia hiyo M1 anayo daiwa!!??
Polisi wa Tanzania kwa mujibu wa Simbachawene ni form four failures ambao kimsingi uwezo wao wa kupangilia hoja Ili zisiache maswali nyuma ni mdogo sana. Hata wale waosomi wazuri wakiingia kwenye mfumo wa kusimamiwa na wanasiasa wajinga wanaowaza madaraka tu, usomi wao hukaa pembeni na kuwaza Kwa ujinga huo huo wa wanasiasa! Amri na utekelezaji tu!
 
Back
Top Bottom