GE2025 Jeshi la Polisi: Atakayethubutu kuvunja sheria Oktoba 29 asitulaumu kwa hatua itakayochukuliwa dhidi yake

GE2025 Jeshi la Polisi: Atakayethubutu kuvunja sheria Oktoba 29 asitulaumu kwa hatua itakayochukuliwa dhidi yake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nakamiwa na wanaume marijali nitakaokutana nao j5 road..!!
Nyie machawa mmelegea kwa kuimba mitano tena 😹
Hakuna Nyumbu anaetoka na nitakukamia hivyo hivyo Nyumbu we
 
Baada ya Lamomy Kuona hii taarifa alienda kukata ticket sahivi kapanda Kibomboi Express anaenda kwao Lushoto kujificha uvunguni hadi tarehe 29 ipite
Hatununui uoga, hio ndio kaulimbiu ya waandamanaji leteni mpaka vifaru barabarani magari na mabomu na risasi bunduki zimenunuliwa kwa kodi zetu
 
Hapa ni kama nishakufa kuliko kujinyonga Bora mniiue
 

Jeshi la Polisi linaendelea kuwahakikishia kuwa kuna usalama wa kutosha tunapoelekea kesho tarehe 29.10.2025 siku ya kupiga kura, kwani hakuna tishio lolote la kiusalama kama tulivyowahakikishia Oktoba 26, 2025.

Aidha, lingependa kuwa tahadharisha kuwa, kuna kikundi cha watu baada ya kuona wameshindwa kuvuruga amani ya nchi yetu wameunda kikundi cha vijana ambao wanaandaa picha mjongeo na taarifa mbalimbali za matukio yaliyotokea siku za nyuma ambayo yalishashughulikiwa na mengine ya kutunga ili wayasambaze kwenye mitandao ya kijamii yaonekane yametokea kipindi hiki au muda mfupi uliopita.

Mkiona taarifa kama hizo kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vingine vya habari vilivyo andaliwa na watu hao wenye nia ovu na amani ya taifa letu mtambue kuwa, ni za uongo, uzushi na za kutaka kutuchonganisha na kutugombanisha.

Wapo pia walioandaliwa kama ambavyo baadhi wamesha jitokeza kuzungumza na kutoa taarifa zenye tungo tata, zenye kutaka kuleta taharuki. Pia wanakusanya matukio ambayo yalitokea nchi zingine na kuyatengeneza kwa kuyawekea sauti zenye lafudhi ya kiswahili ili yaonekane yametokea nchini mwetu na wakati huu muhimu tunapoelekea kupiga kura kesho.

Pia, wamepanga kuchukuwa picha za baadhi ya viongozi na kuziwekea maneno na sauti zenye matamko ya upotoshaji ili ionekane wao ndiyo wanayazungumza au wanayatamka wakati si kweli.

Jeshi la Polisi wakati linaendelea kuwafuatilia ili wawatie nguvuni kwa mujibu wa sheria, linatoa rai kwa wananchi mtakapo ona au kutumiwa picha mjongeo na taarifa kama hizo au vipeperushi na mengine yanayofanana na hayo myapuuze kwani yameandaliwa kwa nia ovu ya kihalifu kwa lengo la kutaka kuleta taharuki kwa wananchi.

Aidha, mkitumiwa taarifa kama hizo msisambaze kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya makosa ya kimtandao badala yake mzifute. Mkumbuke taarifa sahihi zinazohusu jambo lolote zitatolewa na mamlaka zenye wajibu wa kufanya hivyo.


1761642523233.png

1761642536911.png
 

Attachments

  • 1761642300185.png
    1761642300185.png
    696.7 KB · Views: 25
Tarehe 29.10.2025 siku ya Jumatano ni siku muhimu sana katika Taifa letu, ambapo Watanzania watatekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Viongozi watakao waongoza katika nafasi ya Urais, Wabunge na Madiwani.

Jeshi la Polisi kupitia taarifa hii, lingependa kuwahakikishia wananchi na wageni watakao kuwa nchini mwetu kuwa hali ya usalama wa nchi ni shwari sana na hakuna tishio lolote la kiusalama linalo weza kufanya shughuli hiyo ya kupiga kura isifanyike kwa amani.

Pia wananchi mnahakikishiwa amani na usalama wa kutosha siku hiyo ya jumatano, hivyo mjitokeze kwa wingi kama mlivyojiandikisha kwenda kupiga kura bila hofu yeyote ile.

Aidha, lina wahakikishia limejipanga vizuri sana kumdhibiti yeyote yule kwa mujibu wa sheria atakaye jitokeza ama kwa makusudi au nia ovu kuvunja sheria za nchi ili kuhatarisha amani ya nchi kwa kisingizio chochote kile siku hiyo ya kupiga kura na baada ya kupiga kura.

Atakaye thubutu kuvunja sheria asilaumu kwa hatua zitakazo chukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi, kwani elimu imetolewa vya kutosha na kwa muda mrefu.

Hii taarifa yenu itawafikia je walengwa sasa? JF si imefungiwa? Au?
 
Tishio linaonekana hata kwa alie tahira. Wanafikiri watu kutekwa ovyo ovyo na kupotezwa sio tishio.. Hawa jamaa hamnazo kabisa
 
Huo upuuzi wao upite sasa ili tupumue. Tumechoshwa na hayo matamko yao yasiyokwisha.
 
Back
Top Bottom