Tutu kalundji
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 532
- 1,287
Nimekuwa nikiandika makala nyingi sana kuhusu kuwepo kwa ongezeko la vijana katika magenge ya kihalifu wilaya ya bunda hasa kata ya bunda mjini.
Kwa kifupi kata ya bunda mjini inaundwa na mitaa ya nyerere,posta na sabasaba.Mitaa hii ipo katikati ya mjin wa bunda.
Hawa vijana wamejikita zaidi katika kupora wanawake na watoto hasa nyakati za usiku,kuharibu miundombinu ya mabomba na Kisha kuzipeleka kwa watu maalum ambao huziyeyusha na kupata dhahabu feki ambazo huziuza kwa wapita njia.Uhalifu mwingine ni kurusha mabulungutu feki
ya pesa maeneo ya vificho ambapo raia wasiyoielewa hiyo michezo huishia kutapeliwa na kuporwa.
Uhalifu huu umevutia kundi kubwa sana la watoto ambao wameamua kusitisha hata masomo ili wapate pesa.Wahalifu hawa wanaanzia miaka 12-50.
Wiki hii kundi kubwa sana la wanafunzi waliokuwa wakisafiri kwenda mashuleni kupitia stand ya bunda wamelizwa kwa kiasi kikubwa.
Jambo la kushangaza wahalifu hawa wanapofanya hii michezo wala hawakimbii,sielewi Kuna siri ipi katika huu ujasiri!
Nini kifanyike?
Jambo la kwanza Polisi washirikiane na viongozi wa mtaa kufanya sensa kubaini idadi ya vijana katika kila kaya na shughuli wafanyazo.Kijana asiyeeleweka shughuli zake atoe maelezo ya kina kuhusu namna anavyopata pesa!Hili lichukuliwe kwa u serious zaidi.
Jambo la pili ni kuwakamata wahusika wote na mitandao yao yote pasipo kuwaonea haya.Kuzidi kuwafumbia macho bunda inaenda kuwa maficho na eneo hatari zaidi kwa siku za baadae.
Mfano baadhi ya viongozi wa mitandao hii ni bwana mmoja aliyejiegesha kuwa na kimgahawa karibu na nyumba za kulala wageni zenye majina ya Butimbaru Guest,Sauti ya ng'ombe na TwigaGuest.Huyu Jamaa mgahawa wake upo karibu na hizo guest house anajulikana kwa jina maarufu la Baraka wasila.Huyu ndie master mind wa kutrain watoto wote jinsi ya kushughulika na hii biashara.Mara nyingi sana wahusika hukutana pale kwa ajili ya kupanga mipango yao miovu!
Maeneo mengine wanakoratibia mipango yao kikamilifu ni eneo la mama mmoja aitwae nyamagoma,huku mbali ya mipango ya wizi ndio kitovu cha michezo ya kamari ya Kila namna!
Jambo la kushangaza huyu Jamaa Baraka wasila mgahawa wake upo pia jirani kabisa na mwenyekiti wa mtaa wa posta pamoja na balozi wa mtaa wa nyerere.Ila ndio hivyo penye udhia penyeza rupia.Hali ni mbaya hawa vijana kwa siku za baadae ni hatari na hilo pia lilijidhihirisha trh 29.10.2025 walivyokuwa wanapora Mali za watu kwenye maduka.
Upande wa wahalifu naamini kabisa 90% ya vijana katika maeneo haya ni wezi,wakabaji,wauzaji wa bangi,dhahabu feki nk.Mbaya zaidi shughuli zao Zina mkono wa baraka kutoka kwa wazazi wao.Askari kata vikao unavyoitisha kuwa mkali na usipepese macho washakuzoea.Japo ombi langu Timu ya ocd ianze operation kali zaidi maeneo husika ili kuliokoa eneo kabla ya hali haijawa mbaya zaidi!Polisi kamateni hawa wezi ikiwezekana na wazazi wanaowalea ili usalama uwepo wa kutosha.
Jambo jingine ni kwa baadhi ya bodaboda wamekuwa wakipewa pesa kati ya 20000/- mpaka 30000/- kwa kutwa na kuwaachia pikipiki hawa wezi wakafanyie matukio ya kihalifu.Hawa bodaboda mnaweza kabisa kuwabaini kupitia vijiwe vyao na hata kuhoji wananchi wa maeneo husika maana Kila kitu wanashuhudia!Kuhusu bodaboda mnaweza kuwabana kwa kuwapa Sheria kali zaidi zitakazowaogopesha!
Itaendelea..........