Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa taarifa kwa umma kufafanua utata wa kutoweka kwa Mohamed Bakari (28), mkazi wa Mbwanga Wilaya ya Dodoma mjini, ambaye aliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha mnamo Septemba 17, 2026, na kuzua hofu ya kutekwa.
Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa kijana huyo hakutekwa, bali alipatikana akiwa mzima wa afya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Sababu kuu iliyomfanya kuondoka nyumbani kwake na kukimbilia Kahama ni msukumo wa madeni yaliyokuwa yakimkabili na nia ya kwenda kutafuta unafuu wa maisha.
Akiwasilisha taarifa hiyo Septemba 23, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma alieleza kuwa hatua hizo za uchunguzi zilianza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mke wa Mohamed, Elizabert John (24), aliyeeleza kuwa mume wake aliaga kwenda kutafuta fedha za matumizi lakini hakurejea nyumbani.
Baada ya ufuatiliaji, taarifa zilizopatikana kutoka kwa ndugu zake zilithibitisha mahali alipo na sababu za kuondoka kwake. Jeshi la Polisi limewahakikishia wananchi ulinzi na usalama wa raia na mali zao, huku likiwataka kupuuza taarifa zisizo za ukweli zinazohusisha matukio ya utekaji na kuwataka kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
--------------
TAARIFA ZA AWALI ZA KUPOTEA
MOHAMEDI BAKARI HASSAN APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA DODOMA!
Mohamedi Bakari Hassani ni ndugu yangu wa damu. Alipotea usiku wa Ijumaa, 18 Septemba 2026 mpaka sasa hajaonekana, aliiacha familia yake majira ya saa 4 usiku. Alisema ninatoka kidogo nyie pumzikeni nitarudi. Toka usiku huo hakurudi na hakuonekana tena.
Alikuwa akijishughulisha na biashara ndogo ndogo na bodaboda. Ni nimuhitimu wa Chuo cha Mipango cha Dodoma. Baada ya kuhitimu chuo aliendeleea na utafutaji wake huko huko Dodoma na amepotea Dodoma. Tunaomba mtu yeyote atakayemuona toa taarifa kupitia namba hizi 0756290042 au 0797040042.
Asante mungu awabariki
Ni mimi,
Bakari Hassan; 20 Septemba 2026