Jeshi la Polisi: Hakuna ushahidi kuwa Freeman Mbowe alishambuliwa. Alikuwa ametoka kwa Joyce Mukya. Alikuwa amelewa chakari

Pengine muda utasema.
 
Kuna mwanamama ni jirani yeke Mbowe na ni mbunge, anasema hakusikia lolote hadi asubuhi na alishangaa kusikia Mbowe kashmabuliwa na anasema siku hiyo alilala saa saba

Ni kweli kabisa, je CCTV footage Zinaweza kuonyesha huyo mama jirani yake wakati akiingia kwake? Uzuri wa CCTV haziwezi kupangwa zitoe maelezo ya kuokoa jahazi.
 


WATANZANIA HAWAAMINI JESHI LINALOENDESHWA KWA SIFA. Nasikitika sana
 
Hata Balozi za USA, UK, na EU walipokimbilia kutoa matamko kumbe tatizo ni ulevi na ufusika. Sasa sijui wataficha wapi sura zao. Shame on them!!
Zamani balozi hizo zikitoa statement unajua fika zimefanyiwa utafiti zikathitishwa independently na mashirika Yao ya kijasusi nk ndipo watoe statement Sasa hivi hamna kitu wakipitia jamii forums wakiona Kuna jungu wanalitolea tamko no verification no what?

Kuna kufeli Sana kwenye weledi kwa mashirika Yao ya kijasusi yaliyoko Tanzania yako incompetent hasa political security information hawako vizuri Wana produce wrong information kwenye nchi zao

Balozi ni mtu mkubwa wanamwangusha
 
Tangu juzi tumepata nakala ya uchunguzi wa polisi ambao umeandikwa bungeni , kila mtu mwema amelidharau kabisa jeshi la polisi .
Kwanini hukuweka hapa mapema?

Mbowe aache sana na ulevi oktoba imekaribia
 
Watoe na ya Lissu.

Kuna haja ya kulifuta jeshi la Polisi na kuanza upya
 
Yaani jeshi la Polisi hata kutunga hadithi nako ni shida.

1. Ukisoma utaona kuna majina mawili tofauti ya habari moja, Joyce Mukya na Joyce Nkya. Maana yake ni kuwa huu haukuwa uchunguzi bali utunzi

2. Jeshi la Polisi linasema Mbowe alipita sehemu zenye vileo. Kuonekana Bar hakuna maana mtu amekunywa.
Ulevi unaweza kupatikana katika restaurants, je ukionekana huko ina maana umelewa.

3. Aibu kubwa kwa jeshi ni pale inaposema Mbowe alilewa chakari. Jeshi la polisi halifanyi kazi kwa hisia. ''Ulevi chakari ni kitu gani katika vipimo''? Hakuna kitu kama hicho na huwezi kukitumia makalamani.
Jeshi la Polisi lilipaswa kutoa takwimu za vipimo kama hawana wakae kimya , wasijipake zaidi

4. Kwamba mtu hawezi kutamka maneno ni dalili ya ulevi.
Well, nani aliyesema hayo kutoka Hospitali?
Kwanini hawakutaja jina la Dk akliyethibitisha kutotamka vema maneno

Ukisoma habari yote ni aibu tu. Eti mashahidi hawakusikia, hivi Tundu Lisu aliposhambuliwa kulikuwa na mashahidi gani.
Mbona Jeshi la Polisi halielezi kwanini waliondolewa walinzi na kamera, eti leo limefanya uchunguzi

Jeshi la Polisi, kukaa kimya ni busara maana taarifa kama hii kwa wenye akili wanabaki wakicheka.
Hii tamthilia ni tamu sana, na dunia inazidi kutabasamu na kucheka.

Yaani taarifa inaiambia dunia nini kilitokea hakuhitajiki uchunguzi mwingine

Pascal Mayalla Mag3 JokaKuu
 
Kipindi hiki sijawasikia wakitaka wachunguzi toka nje kwa kujua kitakachotokea mwisho wa uchunguzi ni ripoti yenye aibu kubwa
Naona hakuna tena kelele.
Vipi hakuhitajiki uchunguzi huru toka ubalozi wa mmarekani au umoja wa ulaya!
 
Aibu kubwa sana kwa IGP
 
Sasa inakuwaje polisi nao wasingesema kabisa kwamba hakudondoka nyumbani kwake?
 
Yaani vipimo vya hospitali navyo visiaminike? Ni suala la kuchukuliwa vipimo upya kuthibitisha, maana majeraha, km kuvunjika mguu, hayafutiki siku moja.

Mkuu hivi tatizo liko wapi kwenye CCTV footage? Naona kila mtu anakwepa eneo hili. Na sing'ang' anii CCTV kwa bahati mbaya. Nimesema CCTV footage zitafanya kila mtu kuongea ukweli wake, kama Mbowe alikuwa na mwanamke ataonekana na atahukumiwa kwa hilo, kama alishambuliwa hatua zitaangukia kwa wahusika. X-ray zitaonyesha alivyovunja, na sio alivunjika kwenye mazingira gani.

Kwa hapa tulipo mimi naamini kabisa kutokana na maelezo ya Mbowe, na hali halisi ya tukio hata yeye kuna kitu anaficha, hasa hasa mwanamke, ila hata polisi na bunge wanaficha ukweli, na kupotosha ukweli respectively. Ndio maana tunasema msema kweli kwenye hilo ni CCTV Cameras tu. Mwengeso kwanini unakwenda hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…