mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Kwani wewe unataka uongo au ukweli?Kwa maelezo yale unafikiri kutoa video yake si ni uzalilishaji!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani wewe unataka uongo au ukweli?Kwa maelezo yale unafikiri kutoa video yake si ni uzalilishaji!
ThibitishaMbowe alikataa cctv camera nyumbani kwake
Mambo ya PF3 ni ya kwake usimsemee hayo anatakiwa kujibu yeye na Joyce Mukya aliyempeleka hospital hayo hayahusu CCTV Wala wewe Ni yaoHapa una hoja za msingi kabisa na hata mimi nazikubali kwamba kwanini asipate Pf3. Kwakuwa anasema alishambuliwa nyumbani kwake basi tufunge ushahidi wa picha za CCTV ili Mbowe aumbuke. Kama hakuja hapo nyumbani CCTV hazitaonyesha akirudi, na kama alianguka tutaona alivyoanguka, na hata kama alikuwa na kakonyagi kadogo inawezekana kakaonekana, na kama alikuwa na mwanamke ataonekana pia.
Badala ya kusubiri kuingia madarakani kulifuta Jeshi la Polisi unaonaje tumshauri IGP wa Jeshi la Polisi naye aamrishe askari wake wajifungie kwa siku 14, kujipima maambukizi ya korona kama alivyofanya Kamanda wa Makanda wenu kwa Wabunge wake kususia bunge la bajeti!!!Sisi hatutahangaika na jeshi ambalo viongozi wake ni wanaccm , Mahita , Zerothe Steven na Chagonja ni mifano halisi bali tukiingia madarakani taasisi ya kwanza kuifutilia mbali ni polisi
MmmhMbona tulitegemea itakuwa hivyo tu
Huwezi kuwa na polisi duni kama hawa wanaoweza kutumwa na hata mjumbe wa shina wa ccm , lazima upate jeshi lenye weledi linaloelewa maana ya kutumikia wananchi , kwa bahati mbaya sana Ubalozi wa marekani unao ushahidi wa shambulizi la Mbowe , sasa hao polisi wako ni wa kuwahurumia tuKwahiyo mtakuwa na polisi wenu?
Majirani hawawezi kudanganya?Kwa hiyo ulitaka waseme kapigwa hata hajapigwa. Kama unahakika kapigwa unaweza kuthibitishia umma pia. Maana hao majirani hawawezi kudanganya.
Swali lako ni la kipuuzi na halielewekiBadala ya kusubiri kuingia madarakani kulifuta Jeshi la Polisi unaonaje tumshauri IGP wa Jeshi la Polisi naye aamrishe askari wake wajifungie kwa siku 14, kujipima maambukizi ya korona kama alivyofanya Kamanda wa Makanda wenu kwa Wabunge wake kususia bunge la bajeti!!!
Mwenyekiti ndo huyo wafuasi wake je ?????That is why sina chama. I never trust anyone. I never put my hope on someone. Konyagi vepeeee. The devil is a lie ,wallah. Yaani michepuko kila kona,sasa adhabu inayofuata ataanguka apasuke fuvu. Sipendi wanaume wanaocheat wake zao.Na ww ajuza leo naona unarusha mawe tu. Huna hoja lakini unaoongea utoto wa kiwango cha juu.
Chadema haiwezi kufa kwa upuuzi wa MurottoCCM ina mbinu nyingi, hii ni mbinu moja kati ya maelfu ya mbinu walizonazo ili kuhakikisha CHADEMA inakufa
Ndugu yangu hayo ni mambo ya ndani..Hivi Mbowe hanaga mke?
Huyu Joyce Mukya ni nani ,hawara ?
Hata logic ya nilichosema huelewi, kweli mpumbavu hata ukimtwanga na mpunga kwenye kinu mpunga uta koboka yeye atabaki alivyo.Umempa like
Kwani Like umeona jambo la maana
Ndio maana Mna Kurupuka kuropoka hovyo humu ili mpate like
Kwamba Nayo Kitu muhimu ktk maisha yenu et!!
Majirani hawawezi kudanganya?
Majirani walioshuhudia Tundu lisu anapigwa risasi, walisema nini?
Acha ufala wewe, cctv za tukio la Lisu zipo wapi?
Kwa matukio ya utekaji nyara ya wasiojurikana, nani anaweza kwenda kutoa ushahidi, na kwa taarifa yako ilo eneo lilipotokea tukio, sio kama manzese au kawe ambapo watu wanakesha, Dodoma, Daladala tu, zinabaki saa tatu usiku,
Muda wa saa saba usiku eneo la sengia /Area D, ni eneo kimya sana,
Tupia picha yake tuthaminishe
View attachment 1476358View attachment 1476359
USHAHIDI wa awali wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu madai ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe umeonesh kuwa siku hiyo ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakali na alizunguka kwenye kumbi mbalimbali za starehe zinazouza vileo ikiwemo ya Royal Village.
Pia ushahidi huo unaonesha mbali ya kuwa kwenye maeneo hayo ya starehe alikuwa nyumbani kwa mzazi mwenzake Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema na kwamba hata taarifa za kwamba ameshambuliwa zinatia shaka kwani mashahidi wote ambao wameojiwa hakuna anayethibitisha uwepo wa tukio hilo zaidi ya Mbowe mwenyewe na dereva wake.
Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Jeshi hilo David Misime amesema Juni 9 mwaka huu walitoa taarifa ya awali kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Mroto kuhusu tukio la lililoripotiwa kuwa Mbowe amelezwa jijini Dodoma kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa wakati anaingia nyumbani kwake .
Misime amesema baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ya awali wamekuwa wakipokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari wakitaka kufahamu matokeo ya uchunguzi kuhusu taarifa iliyofikishwa Kituo cha Polisi Kati Dodoma.
"Napenda kujulisha kuwa Jeshi la Polisi limeendelea kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa mhanga mwenyewe wa tukio ambaye alidai kuwa muda wa saa saba hivi usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa na anatoka kwa mzazi mwenzake aitwaye Joyce Nkya ambaye ni Mbunge wa Viti Maaluma Chadema anayeishi eneo la Medeli Mjini Ddoma alishambuliwa na kuumia kwenye mguu wa kulia.
"Mhanga wa tukio hilo alidai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kisha hospitali iliyoko takribani umbali wa kilometa tano nje ya Jiji la Dodoma pasipo umuhimu wa kutoa taarifa Polisi kabla ya kwenda kwa Joyce Nkya na Hospitali,"amesema Misime.
Ameongeza upelelezi wao umepata ushahidi kutoka kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa na uwezo wa kuona bila kizuizi kitendo cha kushambuliwa .
"Hata hivyo kwa mujibu wa wa mashahidi hawa hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele hizo au kuona mbowe akishambuliwa. Kwa mantikini hiyo ushahidi pekee unaozumngumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio(Mbowe) pamoja na dereva wake.
"Ambayo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake aitwaje James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake waliona umuhimu wa kumjulisha Jocye Nkya aliyekuwa mbali na eneo la tukio,"amesema.
Pia amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi nchini umethibitisha kuwa siku ya Juni 8 mwaka huu Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwepo ya Royal Village na kupata kinywaji.
"Hata hivyo alipofika hospitali alioneana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.Tunaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hili, hivyo tunaomba wananchi wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi huo wazilete kwetu. Tutaendelea kutoa taarifa kwenu kadri ushahidi utakavyopatikana,"amesema Misime kupitia taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari.
Pia soma
> News Alert: - Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana
> Freeman Mbowe na Joyce Mukya wamtumia Mjomba wa Mtoto kupata cheti cha kuzaliwa
> Mhe. Mbowe na Mhe. Joyce Mukya mtafanya hili suala kuwa siri mpaka lini?
> Joyce Mukya ni nani? Pamoja na kutokuwa active kwenye Siasa bado anapeta ubunge CHADEMA zaidi ya miaka 10