Yaani jeshi la Polisi hata kutunga hadithi nako ni shida.
1. Ukisoma utaona kuna majina mawili tofauti ya habari moja, Joyce Mukya na Joyce Nkya. Maana yake ni kuwa huu haukuwa uchunguzi bali utunzi
2. Jeshi la Polisi linasema Mbowe alipita sehemu zenye vileo. Kuonekana Bar hakuna maana mtu amekunywa.
Ulevi unaweza kupatikana katika restaurants, je ukionekana huko ina maana umelewa.
3. Aibu kubwa kwa jeshi ni pale inaposema Mbowe alilewa chakari. Jeshi la polisi halifanyi kazi kwa hisia. ''Ulevi chakari ni kitu gani katika vipimo''? Hakuna kitu kama hicho na huwezi kukitumia makalamani.
Jeshi la Polisi lilipaswa kutoa takwimu za vipimo kama hawana wakae kimya , wasijipake zaidi
4. Kwamba mtu hawezi kutamka maneno ni dalili ya ulevi.
Well, nani aliyesema hayo kutoka Hospitali?
Kwanini hawakutaja jina la Dk akliyethibitisha kutotamka vema maneno
Ukisoma habari yote ni aibu tu. Eti mashahidi hawakusikia, hivi Tundu Lisu aliposhambuliwa kulikuwa na mashahidi gani.
Mbona Jeshi la Polisi halielezi kwanini waliondolewa walinzi na kamera, eti leo limefanya uchunguzi
Jeshi la Polisi, kukaa kimya ni busara maana taarifa kama hii kwa wenye akili wanabaki wakicheka.
Hii tamthilia ni tamu sana, na dunia inazidi kutabasamu na kucheka.
Yaani taarifa inaiambia dunia nini kilitokea hakuhitajiki uchunguzi mwingine
Pascal Mayalla Mag3 JokaKuu