Jeshi la Polisi halina mbinu, limepoteza sifa ya kuitwa Polisi

Jeshi la Polisi halina mbinu, limepoteza sifa ya kuitwa Polisi

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Sasa ndio polisi wanatafuta balaa, hivi hamna mnaowafundisha kuchunguza ,polisi kupata habari wanategemea eti wananchi wawapelekee habari, mkiambiwa jeshi lipanguliwe mnapiga makelele ,jeshi letu limeishiwa mbinu za kufanya kazi kiuweledi wanalolijua ni kuwakamata wafuasi wa vyama vya siasa tu,hawana zaidi.

Kila mkuu wa polisi akipata fursa ya kuitikiwa na vyombo vya habari ,utawasikia sisi hatuwezi kukamilisha kazi zetu bila ya kusaidiana na nyinyi wananchi, hivi pana jeshi hapa wakifikia kusema hivyo? jeshi halina informers? kila mtaa au kijiji au kijiwe?

Ni wazi kuwa linajitenga na uhalisia kuwa wao ndio walinzi wa Wananchi na mali zao, eti wanawaomba wananchi ,na wananchi hao hao ikifika kumkamata muhalifu na kumpeleka Polisi siku ya pili unamkuta mhalifu yupo nje ,wala hana hofu. Halafu unamwambia mwananchi akupe habari za kijasusi wakati hio ni moja ya kazi kuu za polisi.

Polisi mnatuangusha sana nashindwa kujisifu kama nchi yetu ina jeshi la polisi lenye vipimo vya hali ya juu kabisa. Lipanguliwe tu? Maana wanaoliongoza wamefikia mwisho wa kufikiri, wanalolijua wao ni kumuua muhalifu ila wananchi wakiua wamejichukulia hatua mikononi . Lipanguliwe tu.hakuna msalie mtume,
 
Back
Top Bottom