Jeshi la Polisi kuongea na Waandishi wa Habari Septemba 13, 2024 kuhusu tamko la CHADEMA la Septemba 11, 2024

Jeshi la Polisi kuongea na Waandishi wa Habari Septemba 13, 2024 kuhusu tamko la CHADEMA la Septemba 11, 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1726172335524.png

Soma Pia: Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini
Screenshot_20240912-231931_1.jpg

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es Salaam atatoa tangazo zito kwa ajili ya tamasha

RC ALBERT CHALAMILA ATANGAZA TAMASHA KUBWA LA MAPISHI SIKU YA TAREHE 23 SEPTEMBER 2024 JIJINI DSM, ... RC CHALAMILA AHAIDI TSHS. 20,000 KWA WATAKAO WAHI JUKIANDIKISHA ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=_er2BeGdHTU

Mkuu wa mkoa awataka waje kwa wingi na watapata fedha hizo, ili hadi itapofika kesho aweze kupanga ni wapi watafanya tamasha hilo la nishati safi ... kwa...

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kuitisha usafi wa jiji kufanyika kwa kutumia wanajeshi wafangie barabara lakini mwishowe busara ilitumwa kwake kuwa kuwagombanisha askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ / TPDF na raia siyo jambo sahihi kulifanya ..

TOKA MAKTABA :
13 January 2024

kuelekea maandamano ya CHADEMA 23 January 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=d85tU2mvfa0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ametangaza kufanyika kwa zoezi la usafi katika Wilaya zote 5 kuanzia January 23 hadi 24 January 2024 zoezi ambalo litahusisha Wanajeshi zaidi ya 5000, Polisi zaidi ya 3000, FFU na Vyombo vingine vya dola.

RC Chalamila ameyasema hayo leo katika ibada ya kuwekwa Wakfu Mwangalizi wa Jimbo la Baptist la Dar es Salaam Tanzania, Makamu , Katibu, Katibu Msaidizi, Mhasibu na Mhasibu Msaidizi ambapo amewataka Wakazi wa Dar es Salaam kutokuwa na shaka watakapoviona Vyombo vya Dola vikifanya usafi....
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Anataka kujibizana na CHADEMA kuhusu shughuli zao za kisiasa...?

Yeye kama anataka kuongea na umma, waje na taarifa za uhakika kwa Watanzania kuwaambia ni kwanini wanateka watu, kuwatesa na kisha kuwaua...?

Na waliokwisha kuwateka, wamewaweka wapi? Tunawataka wananchi wenzetu waachiwe huru popote walikowaficha bila masharti yoyote..,

Kama wamewaua, tunataka maiti zao au watuoneneshe makaburi walikowazika, FULSTOP 🛑 🛑...!!
 
Mungu hajawahi kushindwa na shetani..

Kaini alipo muua ndugu yake akaulizwa umempeleka wapi nduguyo akajibu kwa jeuri mimi nimekuwa mlinzi wake?.. Mungu akatoa adhabu wote tunajua....

Uzuri ni kwamba kabla Mungu hajatoa hukumu yake anakuuliza kwanza..
Mfano Walipopotea bensaa8 azori tuliwauliza polisi hawa watu wapo wapi wakatujibu kwa jeuri...

T.lissu alipopigwa risasi tukawauliza wasiojulikana akina nani na ni nani anawatuma wakatupuuza?

Nadhani sote tunajua kilichotokea Yalikuwa ni majonzi kwa Taifa zima.. Mungu sio John..

Leo tuna watu wengi wametekwa na wengine wameuawa kama mbuzi wa supu kwa kumwagiwa Tindikali. Tumeuliza sana Mbona polisi mnafanya hivyo? Wametujibu kwa jeuri..

mtu akiwa na cheo bana anadhani ni moyo atakufa nao kumbe unapata cheo kwa muda na unaondoka muda wowote!! Sijui kama wenye vyeo mnalijua hilo

Wabunge tena tuliowapa dhamana kukaa sehemu takatifu ambapo vitabu vitakatifuna dua zinaanza kabla ya vikao. Tukawataka wajadili kuhusu kutekwa!! Aisee Yule Mama sipiiiika akajibu kwa jeuri, hawana huo muda machafu.. angepotea mwanaye angejibu vile?

Tukasema poa ngoja twende kwa pilato huko nako wakatupuuza!!! Jamani sisi tumewakosea nini? Au hawa ndugu zetu waliopotea hawana damu miili yao ina maji tu.?

Tukajipa Tumaini Mama ni mama!!
Huwezi amini Mama akasema kauli tata et ni drama .. jamani tumekuwa wagriki kwamba tunaigiza movie za ukweli..huku familia zao wanaomboleza?

Mama hivi kweli wanafanya drama za kijumwagia Tindikali na kupigwa risasi za kichwa?

Mama hata kama wamekosea adhabu wanazopewa ni kali na nzito sana Mama. Mama gani unakuwa katili kiasi hiki kwa kauli zako wakati mama ni faraja na tumaini kwa watoto na mme!!! Umetukosea na umemkosea Mungu wako.

Watoto na familia zao zinawalilia ukishindwa kujali hilo basi ebu kumbuka ule uchungu wa Leba mama!!!

wazazi wao wanavyoumia kuwakosa watoto wao, basi warudishiwe hata miili yao wapate kuomboleza mara ya mwisho!!!!

HATA KAMA MTU AMEKUKOSEA NAMNA GANI!! USICHUKUE UAMUZI WA KUMWAGA DAMU YAKE N.A. KUTOKA UHAI WAKE..hilo ni jukumu la Muumba wetu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi Nchini View attachment 3094509

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nani kawafanya kuwa wanyonge?
 
CHADEMA ,wanaakili sana polisi washaingia mkenge ,yaliyotamkwa na chadema yanaenda kuidhinishwa na mkutano mkuu,Yale yatakayoongelewa 13 napolisi ,yatajadiliwa nayo mkutano mkuu..nawao CHADEMA watatoa tamko...kazi inogile
 
Back
Top Bottom