Jeshi la Polisi kuongea na Waandishi wa Habari Septemba 13, 2024 kuhusu tamko la CHADEMA la Septemba 11, 2024

Jeshi la Polisi kuongea na Waandishi wa Habari Septemba 13, 2024 kuhusu tamko la CHADEMA la Septemba 11, 2024

Nchi yetu inakuwaga na mambo ya ajabu sana hasa hivi vyombo vya ulinzi na usalama. Zamani ilikuwa inasemekana Maalbino walikuwa wanapotea hawafi ikaja kugundulika huwa wanauwawa kutokana na imani za kishirikina tena baada ya miaka mingi kupita. Na vyombo vya Ulinzi kazi yao ni kulindana wao kwa wao na sio Wananchi ambao ndio walipa kodi na wanaowafanya wao walipwe mishahara minono. Miaka ya hivi karibuni yameanza kutokea mauaji hata kwa binadamu ambao sio Maalbino tena Sasa hivi wanakufa watu tena waziwazi. Hivi kuna ulazima gani kuwa na jeshi la polisi ambalo halitekelezi majukumu yake yaliyopo kikatiba? Kusema kweli inaleta simanzi na huzuni sana kwa haya yanayotokea nchini. Halafu kuna Wapuuzi na Wajinga jinga humu wanakuwa wanaleta mizaha na masikhara. Watanzania tuwe kitu kimoja na tulie na kuomboleza na wale wanaolia na kuomboleza.
 
Back
Top Bottom