BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
BREAKING NEWS USIKU HUU
Tuna taarifa rasmi kuwa, Jeshi la Polisi, kupitia kwa maelekezo kutoka JUU, limeelekezwa kuzingira Makao Makuu ya CUF, Vuga - Zanzibar. Ili kumzuia Katibu Mkuu wa CUF na Wajumbe halali wa Kikao Cha Baraza Kuu wasitekeleze wajibu wao.
Dola ya CCM inafahamu kuwa Kikao halali cha Baraza Kuu kikikutana kitaweka misimamo dhidi ya njama za DOLA na LIPUMBA na hivyo baadhi ya mabaya wanayotaka kuendelea kuitendea CUF kukwama.
Chanzo cha kuaminika kutoka Jeshi la Polisi kimeeleza kwamba Lipumba alielekezwa afanye mkutano na waandishi wa habari na atoe wito kwa vyombo vya dola vizuie Baraza Kuu hilo ili Polisi waweze kutekeleza hilo.
Hili litatekelezwa na Polisi kwa maagizo kutoka JUU pasina kujali kwamba kikao hicho kimeitishwa kwa kufuata masharti ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014), kifungu cha 80 (1), ambacho kinaipa uwezo Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.
Kutoka Uongozi wa CUF
=======
Kikao kimefanyika vizuri bila tatizo, habari zaidi soma=>Maazimio ya baraza kuu la uongozi la Taifa la CUF kuhusiana na hujuma za dola dhidi ya chama