Tetesi: Jeshi la Polisi kuzuia kikao cha baraza kuu la CUF

Tetesi: Jeshi la Polisi kuzuia kikao cha baraza kuu la CUF

Status
Not open for further replies.
Ukishafanya review kwa lipumba ukajua alikotoka na alipo na mienendo ndipo utagundua mamluki ni wengi katika vyama vya siasa huko nchini. Twendeni na mtambo LISSU anatosha.
 
Alishika biblia mbele ya mamilioni ya Watanzania na wageni waalikwa toka nchi za jirani na kutamka haya, lakini kiapo alichokiapa mbele ya Mungu wake na matendo yake tofauti kabisa!

Hapa naona muhimili mmoja tayar ushatitia (bye bye bunge) huku tukusubir mahakama nayo ichukuliwe na mwewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ni kheri MTU kubaini wapi ulipokosea ili ujue mbinu za kusahihisha kosa kuliko kuhamishia kwa wengine, Aliyeshitaki polisi huhusu kikao haramu cha Zanzibar ni Mwenyekiti wao tena amesema mbele ya vyombo vya habari. Kuwa hajatoa maelekezo ya kuitishwa kwake, Yawezekana hamtaki kumtambua lakini ndyo hivyo sheria inamtambua na polisi wapo kuhakikisha sheria za nchi zinatekelezwa. Mkiambiwa rudini mezani mmalize matatizo yenu kila mmoja ananyonga sharubu, mtaja situka mmechoka kiakili msijue la kufanya.
 
Kinachoniumiza sana, kunisikitisha na kunishangaza ni kusikia miezi/miaka ya nyuma hawa akina Kikwete na Mkapa kwenda nchi za jirani kwenye bara letu kutafuta usuluhishi katika nchi hizo ili kusimamisha machafuko ambayo katika baadhi ya nchi yalisababisha umwagaji wa damu, lakini hapa kwetu wote hawa pamoja na SAS, Warioba, Mwinyi, Msekwa wameuchuna kimyaaa huku wakiona hali ya mshikamano inazidi kupungua na hivyo kutishia usalama wa nchi yetu. Viongozi wa dini nao kimyaaaa hata kukemea kinachoendelea nchini wameshindwa. Wahenga walisema mdharau mwiba.....
Hata sasa JK ni msuluhish wa Libya Saga

May Allah bless Me and You
 
IMG_20170728_063527.jpg

Haya maisha,huwez kujua kesho yako.
Leo Maalim na Lipumba hawakai meza moja.Na haya ndo maisha,hamuwez kukubaliana kila kitu

May Allah bless Me and You
 
Kwa nini watawala wa awamu ya tano wanaelekeza nguvu zote kunyamazisha ama kuua upinzani badala ya kujikita katika kutatua matatizo yanayolikabili taifa na wananchi kwa ujumla. Hivi msingi wa matatizo yanayoikabili Tanzania kwa sasa ni wapinzani ama yanatokana na mfumo pamoja na watawala wenyewe?.
 
Naomba mungu Cuf wasibugudhiwe ili japo nasi tujue kwamba wao wanakuja na point ipi ya msingi katika hili suala.kwani kama watadhuiliwa basi inaweza ikaleta kwikwi sana katika hali ya usalama wa demokrasia na amani kwa ujumla .nakumbuka nilipokuwa mtoto mama aliwahi kuniambia kuwa dawa nzuri ya kupunguza hasira ni kulia. Tunakuomba sana ewe muhimili wa nne 'maagizo kutoka juu' uwaruhusu hao wote wafanye kikao chao tafadhari ili watoe duku duku lao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata sasa JK ni msuluhish wa Libya Saga
May Allah bless Me and You
Unasuruhisha watu waliotayari kusuruhishwa, mtu asiyekubali suruhu kama maalimu unaanzaje? Mara ngapi ameshauriwa suruhu na michakato kuanza haipiti kitambo anakimbilia Dar kutangaza hataki suruhu? Wabobezi wa siasa wamemshauri kusuruhishwa na Mwenyekiti kwa afya ya CUF anakana katukatu hakai na msaliti. Lipumba anauliza, "Leo maalimu anakaa Meza moja na Sumaye aliyetekeleza mauaji ya wana CUF 60 ktk maandamano ya 2001 Mkapa na Maalim wakiwa ugaibuni lakini katu hataki kukaa meza moja na Mimi niliyekuwa front line?"
 
Ni dhahiri serikali ya ccm imeamua kuua upinzani na kulazimisha kufanay itakacho kwa maslahi ya watu watchache kwa kutumia mitutu. Huu ni ubabe ubabe.

Wakati CCM wakikutana ndani na nje kwa uhuru bila woga, na wanachokitafanya ni kampeni dhidi ya umoja wa nchi na matusi kwa Watanzania as if nchi ni yao peke yao, vyama vya upinzani ambavvyo ndivyo vina Watanzania wengi kuliko CCM, haviruhusiwi kufanya mikutano huru ya hadhara. Kwa nyongeza, hata mikutano ya ndani inazuliwa, na la ajabu, hata ya viongozi tu peke yao marufuku isipokuwa ile inayofanywa na vyama vyenye ubia na ccm kama ccm lipumba.

Wapinzani halisi ninaomba muende mbele zaidi. Acheni kulumbana na kufukuzana na maccm ambao kwao taifa si kitu isipokuwa maslahi yao. Hamwezi kuendelea kupigania taifa ikiwa mnaambiwa mikikutana mtauawa. Na mtauawa kweli. Kama si vitisho vya kuuliwa, bila shaka pasingekuwa na sababu ya kuwaweka kwenye targeti za mitutu ya bunduki. Bado ukombozi upo na hapo ndipo ccm itakufa kifo cha moja kwa moja kwa kuwa hakutakuwa na mtu wa kuwakubali kwa lolote. wakipoteza wameondoka na Tanzania itakuwa huru. Na hilo wanalijua.

USHAURI WANGU. FANYENI E-CONFERENCES, MUAZIMIE KILA MKITAKACHO NA HAKUNA BUNDUKI ITAPEKUA KILA NYUMBA KUANGALIA NANI YUKO KWENYE MKUTANO NA NANI. UKAWA MNA IT WAZURI, WATUMIENI HAO MTENGENEZE HII NAMNA YA KUONDOKANA NA MAKELELE YA KIBABE NA VITISHO VYA BUNDUKI.

MKAKATI HUU UFANYENI KATIKA NGAZI ZOTE. TECHNOLOJIA IKO JUU SANA KWA SASA KUZUIA WATU WASIKUTANE. WASILIANENI KWA NJIA YA MITANDAO. KUTANENI YA WANACHAMA WENU KWA NJIA HII. KUBALIANENI MIKAKATI KWA NJIA HII NA FANYENI SENSITIZATION NA RECRUITMENT YA WANACHAMA WAPYA, NA MPASHANE HABARI KWA NJIA HII.

KWA KUWA HAMRUSIWI KUKUTANA KWA WINGI, WALE WANAOBAHATIKA KUPATA AUDIENCE NA WATU, WAWASILISHE HOJA ZENU ZA NGUVU.

FANYENI TATHMINI YA MAMBO YENU KWA MTANDANO. HADI CCM WAIGE HAPA, WATAKUWA WALISHAPOTEZA UWEOZ WA KUONA.
Umeme utazimwa siku hiyo! Au mitandao itaamrishwa kuzima network
 
Unasuruhisha watu waliotayari kusuruhishwa, mtu asiyekubali suruhu kama maalimu unaanzaje? Mara ngapi ameshauriwa suruhu na michakato kuanza haipiti kitambo anakimbilia Dar kutangaza hataki suruhu? Wabobezi wa siasa wamemshauri kusuruhishwa na Mwenyekiti kwa afya ya CUF anakana katukatu hakai na msaliti. Lipumba anauliza, "Leo maalimu anakaa Meza moja na Sumaye aliyetekeleza mauaji ya wana CUF 60 ktk maandamano ya 2001 Mkapa na Maalim wakiwa ugaibuni lakini katu hataki kukaa meza moja na Mimi niliyekuwa front line?"
Leo hii unamwambia Seif hatak suluhu,kwani chanzo cha yote ni nini?
Haya sasa CUF imeshasplit,na kuna kila dalilk 2020 ikapoteza sana Udiwani na Ubunge kwa spidi kali sana

May Allah bless Me and You
 
sidhan kama watazuia maana kufanya hivyo ni sawa na kumzuia Mh Polepole kufanya mkutano kitu ambacho wanajua consequence zake...
 
CCM inalazimisha vita kwa udi na uvumba .
CUF, tulieni msumari wa moto uwaingie, chama kiliporwa kwa James Mapalala, tulieni chama kirudi tabora . huko pemba anzisheni chama chenu
 
Unasuruhisha watu waliotayari kusuruhishwa, mtu asiyekubali suruhu kama maalimu unaanzaje? Mara ngapi ameshauriwa suruhu na michakato kuanza haipiti kitambo anakimbilia Dar kutangaza hataki suruhu? Wabobezi wa siasa wamemshauri kusuruhishwa na Mwenyekiti kwa afya ya CUF anakana katukatu hakai na msaliti. Lipumba anauliza, "Leo maalimu anakaa Meza moja na Sumaye aliyetekeleza mauaji ya wana CUF 60 ktk maandamano ya 2001 Mkapa na Maalim wakiwa ugaibuni lakini katu hataki kukaa meza moja na Mimi niliyekuwa front line?"
Na Lipumba anakaa meza moja na JPM anaewaita wapinzani VILAZA na hatak wafanye mikutano[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

May Allah bless Me and You
 
Leo hii unamwambia Seif hatak suluhu,kwani chanzo cha yote ni nini?
Haya sasa CUF imeshasplit,na kuna kila dalilk 2020 ikapoteza sana Udiwani na Ubunge kwa spidi kali sana

May Allah bless Me and You
Chanzo cha yote haya ni udikteta wa Maalim kuzuia maombi ya baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Ubungo Plaza kutaka Lipumba ajieleze mbele ya wajumbe ili yatoke maamuzi sahihi na ya pamoja. Haya yote yasingetokea. Fitina na mabavu Siki zote hayajengi
 
Na Lipumba anakaa meza moja na JPM anaewaita wapinzani VILAZA na hatak wafanye mikutano[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

May Allah bless Me and You
Na hawaoni madhara ya misuguano isiyo na afya wataitwaje?
 
Umeme utazimwa siku hiyo! Au mitandao itaamrishwa kuzima network
++++++++++++++++++++++++
Nani atatangaza kwamba leo tuna E-Conference? Tukifanya usiku wa manane nani atazima nini? Kumbuka tunafanya kutoka sehemu mbali mbali duniani na tunatumiwa mitandao mbali mbali

Imekula kwa CCM hii!.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom