Tetesi: Jeshi la Polisi kuzuia kikao cha baraza kuu la CUF

Tetesi: Jeshi la Polisi kuzuia kikao cha baraza kuu la CUF

Status
Not open for further replies.
Ana akili gani alikikimbia chama vitani!! Leo anaharibu kila walichovuna ktk hali ngumu ?!. Sasa hapo ana akili kweli ?!

Cairo's
Anazo akili coz ametumia mapungufu ambayo yapo kwenye katiba yao,Seif ndie mwenye kosa ilibidi amalize hili mapema xana kipindi ambacho jamaa anaondoka lakini ameshindwa na sasa anamhenyesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BREAKING NEWS USIKU HUU

Tuna taarifa rasmi kuwa, Jeshi la Polisi, kupitia kwa maelekezo kutoka JUU, limeelekezwa kuzingira Makao Makuu ya CUF, Vuga - Zanzibar. Ili kumzuia Katibu Mkuu wa CUF na Wajumbe halali wa Kikao Cha Baraza Kuu wasitekeleze wajibu wao.

Dola ya CCM inafahamu kuwa Kikao halali cha Baraza Kuu kikikutana kitaweka misimamo dhidi ya njama za DOLA na LIPUMBA na hivyo baadhi ya mabaya wanayotaka kuendelea kuitendea CUF kukwama.

Chanzo cha kuaminika kutoka Jeshi la Polisi kimeeleza kwamba Lipumba alielekezwa afanye mkutano na waandishi wa habari na atoe wito kwa vyombo vya dola vizuie Baraza Kuu hilo ili Polisi waweze kutekeleza hilo.

Hili litatekelezwa na Polisi kwa maagizo kutoka JUU pasina kujali kwamba kikao hicho kimeitishwa kwa kufuata masharti ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014), kifungu cha 80 (1), ambacho kinaipa uwezo Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Kutoka Uongozi wa CUF
Watumie GoToMeeting app. Dunia imebadilika sasa. Si lazima kila wakati mkutane ana kwa ana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inasikitisha mno kuona kura za watanzania walizopigia upinzani zikizimwa kwa nguvu kubwa ya dola,ni wazi kuwa vyombo vyetu vya usalama vinatumika kisiasa ,na upinzani unasukumwa kwenda ICUs,bila shaka siku kama ya leo mwakani sijui kama kutakuwa kilichobaki katika upinzani,very sad because any strong government need a strong oppositions to keep on check kama tunavyocheza chess,na hii inapelekea kupata good service deliveries kitu ambacho the poor of the poorest ndio anakihitaji.
 
Anazo akili coz ametumia mapungufu ambayo yapo kwenye katiba yao,Seif ndie mwenye kosa ilibidi amalize hili mapema xana kipindi ambacho jamaa anaondoka lakini ameshindwa na sasa anamhenyesha

Sent using Jamii Forums mobile app
Omba uhai CUF chini ya Lipumba huyu ambaye hawezi kupata hata ubunge kwao Tabora. Hawezi kupata wabunge na madiwani bara na visiwani. Na ndiyo itakuwa mwisho wa CUF. Ref NCCR mageuzi

Cairo's
 
Kinachoniumiza sana, kunisikitisha na kunishangaza ni kusikia miezi/miaka ya nyuma hawa akina Kikwete na Mkapa kwenda nchi za jirani kwenye bara letu kutafuta usuluhishi katika nchi hizo ili kusimamisha machafuko ambayo katika baadhi ya nchi yalisababisha umwagaji wa damu, lakini hapa kwetu wote hawa pamoja na SAS, Warioba, Mwinyi, Msekwa wameuchuna kimyaaa huku wakiona hali ya mshikamano inazidi kupungua na hivyo kutishia usalama wa nchi yetu. Viongozi wa dini nao kimyaaaa hata kukemea kinachoendelea nchini wameshindwa. Wahenga walisema mdharau mwiba.....
Wewe unashindwa nini kuchukua hatua ? au uwezo wako ndio huu wa kuja hapa kuongea majungu na mipasho? unatumia muda mwingi kutunga uwongo bila kuangalia athari zake, ulivo kuwa mweupe unashindwa ata kujitathmini umejaa chuki zakupitiliza kwa watawala, utaumia na kusikitika sana maana hamkutumwa mbadilishe magia yenu angani ni ujinga kuweza kuamini gia ikibadilishwa angani huwa haina madhara.
 
Serikali ikimpandikiza msaliti nawe wataka kila mtu afuate ETI ndio ufumbuzi. Wachekesha sana. Tz iliyozisaidia nchi zote kusini mwa Afrika kukataa ukoloni, ukaburu, ukandamizaji na vibaraka akina Muzorewa, Sithole, Urio Simango, Jonas Savimbi etc; ETI leo yashauriwa na Mtz iyakumbatie yaleyale. Nadhani kuna tatizo kubwa laja hapa NCHINI kwetu. Mungu tusaidie. AMEN.
Sidhani mfano wako unaswihi. Kwa taarifa yako hao wrote uliowataja hawakusaliti vyama vyao Bali nchi zao na pamoja na kutukia mabomu ma eisasi migogoro yao haikwisha mpaka walipokaa mezani sembuse Lipumba na Maalim?
 
CUF ya Seif ingalijikita na kukazana zaidi katika kesi ya msingi waliyoifungua mahakamani takribani mwaka mmoja uliopita inauyohusu msajili wa vyama vya siasa kumtambua Lipumba kama mwenyekiti halali wa CUF. Hili ndiyo la msingi kwani as long as Lipumba ndiye anayetambuliwa na mamlaka husika kwa mjibu wa sheria, cho chote watakachofanya kundi la Seif kinyume na matakwa ya Lipumba kitakuwa si halali na kinaweza kuhesabika ni kufanya fujo na hivyo kulazimisha FFU kufanya kazi yake.

Kwa nini akina Seif hawakazani na hiyo kesi ya msajili kumtambua Lipumba? Jee hawana namna ya kuilazimisha mahakama iharakishe kesi hiyo? Au kesi hiyo ilishafutiliwa mbali au ilishashindikana? Kama kesi hiyo ilishashindikana, basi inabidi wakubali tu kwamba Lipumba ndiye mwenyekiti wao na wanapaswa kushirikiana naye.
 
f0770f163cb0c0652ed20f0de34c6643.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom