Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenyekiti wa CUF si ni Ibrahim H. Lipumba? hakuna kibaya hapo kama hawakumshirikisha kufanya hicho kikao. Ni muhimu mamlaka iheshimiwe. Bila kuheshimu mamlaka hakuna maana ya siasa.
Kwani kuna tatizo gani si wakafanye nyumbani kwa maalim sefu?kulialia kwa nini?
Katiba ya CUF iko wazi kikao cha baraza kuu kinaitishwa na mwenyekiti,na mwenyekiti kasema hajaitisha kwa hiyo hicho ni kikao cha harusi tu
Licha ya majibu yako ya kibavicha ngoja nikujibu ifuatavyo.:-kikao kimeitishwa kama baraza kuu,ni mwenyekiti tu ambaye ni Lipumba anapaswa kuitisha hicho kikao,na ndio maana amesema hajaitisha kikao chochote huko zanzibar.Anaingiliaje kikao cha watu ambacho hakimuhusu/hajakiitisha yeye na hajui ni cha watu gani na wanajadiliana nini ?
Kwa mujibu wa chama cha CUF ya lipumba amboya ndiyo inatambuliwa kisheria kikao hicho si halalai, na sheria itachukulia kikao hicho kuwa batili. Anachofanya Prof. ni kujaribu kuuvuta umma utambue yeye bado mwenyekiti wa chama cha CUF, waache kusikiliza au kutilia maanani siasa za chama flani, hasa walioanzisha 'operation tokomeza usaliti'.Mimi nadhani kama kikao si halali maana yake chochote kitakachojadiliwa na maamuzi yatakayotolewa pia yatakuwa si halali !!
Shida na wasiwasi wa Propesa Lipumba ni nini hasa iwapo anajitambua kuwa yeye na kundi lake ndiyo viongozi halali wa CUF ? Si aachane na walio nyuma ya CUF Zanzibar na Maalim Seif S. Hamad kwa sbb kikao Chao kitakuwa kama cha harusi tu, au siyo bwana ?
mkuu nakumbuku kipindi cha nyuma kidogo,kabla ya uchaguzi,lipumba akiwa bega na maalim seif,kuna mtu mmoja wa makamo aliwahi kutuambia huyu jamaa anatumiwa na system,sote tulibaki kinywa wazi maana kwa nafasi ya yule mtu hawezi sema jambo lenye shaka,tangu kuanza kwa sakata ili sina chembe ya shaka yoyote na kauli ya yule mtuBREAKING NEWS USIKU HUU
Tuna taarifa rasmi kuwa, Jeshi la Polisi, kupitia kwa maelekezo kutoka JUU, limeelekezwa kuzingira Makao Makuu ya CUF, Vuga - Zanzibar. Ili kumzuia Katibu Mkuu wa CUF na Wajumbe halali wa Kikao Cha Baraza Kuu wasitekeleze wajibu wao.
Dola ya CCM inafahamu kuwa Kikao halali cha Baraza Kuu kikikutana kitaweka misimamo dhidi ya njama za DOLA na LIPUMBA na hivyo baadhi ya mabaya wanayotaka kuendelea kuitendea CUF kukwama.
Chanzo cha kuaminika kutoka Jeshi la Polisi kimeeleza kwamba Lipumba alielekezwa afanye mkutano na waandishi wa habari na atoe wito kwa vyombo vya dola vizuie Baraza Kuu hilo ili Polisi waweze kutekeleza hilo.
Hili litatekelezwa na Polisi kwa maagizo kutoka JUU pasina kujali kwamba kikao hicho kimeitishwa kwa kufuata masharti ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014), kifungu cha 80 (1), ambacho kinaipa uwezo Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.
Kutoka Uongozi wa CUF
Kwa mujibu wa chama cha CUF ya lipumba amboya ndiyo inatambuliwa kisheria kikao hicho si halalai, na sheria itachukulia kikao hicho kuwa batili. Anachofanya Prof. ni kujaribu kuuvuta umma utambue yeye bado mwenyekiti wa chama cha CUF, waache kusikiliza au kutilia maanani siasa za chama flani, hasa walioanzisha 'operation tokomeza usaliti'.
Mkuu mimi natofautiana na wewe kwa sdababu kadhaa.Kinachoniumiza sana, kunisikitisha na kunishangaza ni kusikia miezi/miaka ya nyuma hawa akina Kikwete na Mkapa kwenda nchi za jirani kwenye bara letu kutafuta usuluhishi katika nchi hizo ili kusimamisha machafuko ambayo katika baadhi ya nchi yalisababisha umwagaji wa damu, lakini hapa kwetu wote hawa pamoja na SAS, Warioba, Mwinyi, Msekwa wameuchuna kimyaaa huku wakiona hali ya mshikamano inazidi kupungua na hivyo kutishia usalama wa nchi yetu. Viongozi wa dini nao kimyaaaa hata kukemea kinachoendelea nchini wameshindwa. Wahenga walisema mdharau mwiba.....
Si Mungu huyo wa MtukufuWacha upumbavu wewe! Hivi ni Mungu yupi huyo mwenye kumtuma mtu apandikize chuki za kutisha hivyo na kutumia vitisho kila kukicha dhidi ya wanadamu wenzie!?
Mkuu mimi natofautiana na wewe kwa sdababu kadhaa.
1-Hivi katika Mgogoro wa CUF Maalim Seif hana kosa lolote?
2-Hivi katika mgogoro huu wa CUF Lipumba hana kosa lolote?
Kama wote wana makosa UFUMBUZI WA MATATIZO UTATULIWE KWA MARIDHIANO.
Kila mmoja akubali kupata na kukosa.
Kwangu mimi kosa Kubwa kwa Maalim ni KUFANYAKAZI KIMAZOEANA.
Maalim anawashauri wa kisheria wengi tu wazuri wangetafusiri katiba yao juu YA HITIMISHO LA KUJIUZULU mwenyekiti kikatiba ni DHAHIRI MAALIM ANGEITISHA KIKAO CHA BARAZA KUU KURIDHIA KUJIUZULU KWA MWENYEKITI.
KUTOKANA NA MAZOEA WOTE WALIPIGWA GANZI,HAWEAKUCHUKULWA HATUA.Gharama yake ni lazima wakae pamoja.Wamalize tofauti yao,na wasonge mbele.
Uchanguzi wa uongozi wa cuf haupo mbali,wakati ukifika na wapiga kura wakiridhia Lipumba Atatoka tu.
Hii ni kwa Maalim,UKAWA SIO CHAMA WALA HAWANA KATIBA WALA UONGOZI.
KWAKO,UKIIFANYA CUF KWANZA UKAWA BAADAE UTAFANYIKIWA.
UKIFANYA UKAWA KWANZA CUF BAADAE UTAHARIBIKIWA.AKILI YA KUAMBIWA UKICHANGANYA NA YAKO..........
Unatofautiana kwa sababu zako ambazo hazina kichwa wala miguu Mkuu. Huyu muhuni alijiuzulu na vikao halali vya chama vikamfuta uanachama. Hivi wahuni na mafisadi wa MACCM wangekubali aliyejiuzulu na kisha kufutwa uanachama awafanyie kama haya yanayofanywa na huyo mhuni!?
Mkuu bado msingi wa kutatua mgogoro ni maridhiano, kila mmoja WAO akubali kupata na kukosa.
Tukubali kuwa kuna tatizo,huo utakuwa ndio mwanzo wa ufumbuzi.
Lakini tukishabikia kwa vitu kama operation tokomeza msaliti,mgogoro huu utakuwa mgumu kufikia tamati.
Baraza za CUF linaitishwa na Mwenyekiti wa CUF siyo Katibu Mkuu na wala Makao Makuu ya CUF hayo Unguja yako Buguruni, Dar es Salaam. Wewe mbeba mabox huwezi jua ya TZ waachie wanaCUF wenyewe!!BREAKING NEWS USIKU HUU
Tuna taarifa rasmi kuwa, Jeshi la Polisi, kupitia kwa maelekezo kutoka JUU, limeelekezwa kuzingira Makao Makuu ya CUF, Vuga - Zanzibar. Ili kumzuia Katibu Mkuu wa CUF na Wajumbe halali wa Kikao Cha Baraza Kuu wasitekeleze wajibu wao.
Dola ya CCM inafahamu kuwa Kikao halali cha Baraza Kuu kikikutana kitaweka misimamo dhidi ya njama za DOLA na LIPUMBA na hivyo baadhi ya mabaya wanayotaka kuendelea kuitendea CUF kukwama.
Chanzo cha kuaminika kutoka Jeshi la Polisi kimeeleza kwamba Lipumba alielekezwa afanye mkutano na waandishi wa habari na atoe wito kwa vyombo vya dola vizuie Baraza Kuu hilo ili Polisi waweze kutekeleza hilo.
Hili litatekelezwa na Polisi kwa maagizo kutoka JUU pasina kujali kwamba kikao hicho kimeitishwa kwa kufuata masharti ya Katiba ya CUF ya mwaka 1992 (Toleo la 2014), kifungu cha 80 (1), ambacho kinaipa uwezo Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama kuitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.
Kutoka Uongozi wa CUF