Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Baada ya kuwepo kwa malalamiko na mashauri mengi kuhusu uhalali wa Jeshi La Polisi Tanzania kuzuia maandamano nchini hatimaye Jeshi hilo limeamua kutoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo.
Tamko hili la Jeshi La Polisi linakuja siku chache tangu Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam, Jumanne Muliro kukataza na kupiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, maandamano ambayo hata baada ya kuzuiwa yalifanyika.
Kwenye tamko lao, Jeshi La Polisi limefafanua kwamba, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa sura ya 258 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019 kifungu cha 11 (7) (c) wana mamlaka ya kulinda amani na usalama wa umma na kwamba wanaweza kuzuia maandamano endapo kutakuwa tishio la uvunjifu wa amani, na hivyo hatua wanazochukua ziko ndani ya uwezo wa kisheria.
Jeshi la Polisi pia limeeleza kwamba suala la maandamano linapaswa kufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa viongozi wa polisi kabla ya kufanyika kwa maandamano yoyote.
Soma pia: CHADEMA watoa tamko baada ya viongozi wake kukamatwa wakiandamana: "Polisi wametumia nguvu kupita kiasi"
Pia, tamko la Jeshi la Polisi linatoa mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusu haki zao za kisheria ikiwa polisi watazuia mikutano yao.
Jeshi la Polisi limedokeza kuwa kuwa chama cha siasa kinaweza kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi ikiwa watapinga uamuzi wa polisi pamoja na kuongeza jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wanaopanga au kuhamasisha vitendo vya vurugu.