Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Mara baada ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amelielekeza Jeshi la hilo kuhakikisha linaendelea kusimamia kikamilifu usalama katika Ziwa Tanganyika akisisitiza boti hiyo itumike kwa shughuli zilizokusudiwa huku akiwaomba wananchi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji Tanzania, SACP Moshi Sokoro, amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ununuzi wa boti hizo akisema jumla ya boti 11 za kisasa zimenunuliwa na tayari zimegawiwa katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Mkoa wa Katavi.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani, amesema boti hiyo itasaidia kuimarisha doria na misako mbalimbali katika ziwa hilo, sambamba na kufikisha elimu ya polisi jamii kwa wananchi, hususan wavuvi wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa Kata ya Karema pamoja na wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali kwa hatua hiyo, wakieleza kuwa boti hiyo itasaidia kukabiliana na changamoto ya matukio ya unyang'anyi, hususan wa vifaa vya uvuvi, ambayo yamekuwa yakiwasumbua wavuvi katika Ziwa Tanganyika.