Inatisha sana. Wanatudanganya Watanzania kwamba hawahusiki kumbe ni wao. Kelele za Watanzania nchi nzima zimewaogopesha hawa vinginevyo hawa nao wangepotea kabisa. Yule mwigulu anajibaraguza mitandaoni jana eti naye anashangazwa na kutekwa kwao kumbe yuko ndani ya himaya yake. Wamrudishe Bensaanane akiwa hai na mzima wa afya.
Anaandika Mzalendo Bollen Ngetti
SUALA la utekaji, utesaji na hata upotezaji wa watu huwa na sura mbili hususan katika tawala za Kiafrika. Suala hili ni la kawaidi katika nchi za Rwanda, Burundi, Ethiopia, Misri, Afrika Kusini na Angola. Hata Kenya hali ni hiyo hiyo.
Mara nyingi matukio haya hutendwa ama na vyombo vya dola kama Idara za Usalama au Jeshi la Polisi au vikundi vya kigaidi vyenye misukumo ya kisiasa.
Inapotokea Idara ya Usalama kumpoteza mtu lazima kuna kuwa ushahidi usio na chembe ya shaka kuwa mtu huyo anahatarisha usalama wa Taifa. Kwamba kuendelea kuwepo uraini ni hatari kwa uhai wa Taifa na hivyo ni salama zaidi akapotezwa ama kufungwa jela daima, kuuawa au kufichwa katika "dark sites" kwa mahojiano zaidi. Hapa Idara hii inalihakikishia Taifa usalama wake.
Wakati mwingine matukio haya hutendwa na Jeshi la Polisi wasio waaminifu kufuta ushahidi wa matendo yao maovu. Mathalan jambazi sugu amekamatwa akiwa hai na sheria inataka afikishwe kortini. Lakini kwa intelijensia ya polisi mtu huyu ni hatari zaidi. Polisi kuondoa "usumbufu" ni rahisi kummaliza huyu mtu na isiwepo kesi yoyote. Si haki lakini "hakuna namna" anauawa.
La tatu matendo haya hutendwa na vikundi vyenye misukumo ya kisiasa. Na mchezo huu kwa Tanzania imewahi kuchezwa sana na CHADEMA kwa kikosi chake cha Red Brigade al-maarufu MUNGIKI. Hapa lengo linakuwa ni kuwajengea wananchi mazingira ya kuamini Serikali yao ni katili na ndio inayoteka na kutesa watu na kuwapoteza. Hutumia mbinu hii kujaza umma hasira na chuki ili umma ikione chama hicho ndio kimbilio la wanyonge wenye huruma.
Hufanya kazi hii kwa akili ya hali ya juu. Unaweza kuonekana mtu anayemkosoa sana ama mkuu wa nchi au Serikali yake, basi kikundi hiki hutumia mbinu ya kumteka, kumpoteza ili ijengeke picha kuwa ametekwa na Serikali. Rejea kupotea kwa Ben Saanane na jinsi viongozi wa CHADEMA walivyolishughulikia kimtulinga. Hadi Leo ilitaka kuaminishwa umma eti katekwa na vyombo vya dola kwa kumkosoa Rais JPM kuhusu PhD yake. Hoja ambayo hata hivyo ilipeperuka na kupotea. Mimi bado nina amini viongozi wa CDM wanajua aliko Ben.
Roma Mkatoliki na wenzie wamechukuliwa na watu waliosadikika kuwa ni Polisi. Hapa pia "kusadika" inataka kuleta picha ya moja kwa moja kuwa ni Polisi walimteka. Na endapo atapotea mazima au kufa basi taswira iwe ni Jeshi la Polisi limehusika. Ninakataa tabia hii. Tunaijengea picha mbaya nchi yetu katika jumuiya za kimataifa. Tanzania hatujafika huko. Jeshi la Polisi limekiri kupokea taarifa za kupotea kwa wasanii hao na limeanza upelelezi. Povu la nini? Na kwa nini tuiharakishe jeshi hilo tunavyotaka? Wanaweza kutumia wiki kadhaa, siku kadhaa hata miaka kadhaa maana huwezi jua mtekaji alijipanga vipi na kwa muda gani. Tuache jeshi lifanye kazi.
Uongozi wa Mkoa umesema haitofika Jpili tayari ROMA atakuwa amepatikana. Tusubiri badala ya kuishutumu Serikali as if hii ni Serikali ya kigaidi. Nakataa maana watu kama ROMA hawana madhara yoyote kwa utawala wa nchi na usalama wa Taifa. Ni mbwembwe tu za mitandaoni na uhuru wa maoni.
Tumtafute Ben, tumtafute ROMA bila kusahau kujua "ajali" iliyomuua Chacha Wangwe ilisababishwa na nini (nani).
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]!