Jeshi la Polisi lakana kuhusika kutekwa kwa msanii Roma Mkatoliki

Jeshi la Polisi lakana kuhusika kutekwa kwa msanii Roma Mkatoliki

Polisi wetu wanafrahisha sana hivi ni nani anaepaswa kutoa taarifa kuhusu roma ni wananchi au ni wao baada ya kutowa utafiti wao.. au nini maana ya serikali ina mkono mrefu.?!
 
Jeshi la polisi Dar kupitia kwa kamanda Simon Sirro limekana kuhusika kwa lolote lile lililomtokea msanii Roma Mkatoliki na kwamba linafanya jitihada kumpata.

Jeshi hilo limeomba mtu mwenye taarifa zinazomhusu msanii huyo kupeleka taarifa kwao mara moja.

Msanii huyo alitekwa juzi jioni akiwa ndani ya studio za Tongwe records pamoja na wenzake na mpaka sasa hajulikani alipo na yupo katika hali gani.
@
Aidha upo uvumi unaoenezwa ndani ya mitandao na vijiweni kuwa huenda msanii huyo amefikwa na "mabaya" hali ambayo imezua taharuki kubwa miongoni mwa wasanii.
kikanuni jeshi la Polisi popote pale duniani haliteki watu (KIDNAPING) bali linakamata (ARRESTING) tena kwa arresting order au hata warrant, zoezi ambalo ni la wazi mtu anapokuwa arrested anahaki ya kuwasiliana na ndugu zake au hata wanasheria wake nk masuala ya kuteka mara nyingi hufanywa na vitengo 'SPECIAL UNITS' vya wanausalama wa michepuo ya kijasusi ktk nchi hawa ndio huwachukua watu kimyakimya wakati mwingine hata bila taarifa kwa mamalaka zingine kujua, hawa huwa hatari sana ktk utawala wa haki ktk Taifa, rejea utendaji wa The State Research Bureau huko Uganda wakati Idd Amin Regime.
 
Sasa wewe unataka wasemeje iwapo kama hawajawachukua. Mbona chama mfu wana vikundi vya ugaidi na utekaji
usiwe na siasa kila seheme kama lingetokea kwa mama ako au baba yako ukudhubutu kutoa kauli kama hizo za kisiasa za chama mfu kama huna chakuchangia usiharibu mb na chaji yako
 
Mengi yanazungumzwa kuhusiana na hili tukio la kutoweka kwa Hawa wenzetu, lawama ni nyingi Sana.

Lawama zimeelekezwa kwa RC Makonda, Jeshi la polisi, serikali, likihusishwa pia na siasa za nchi hii.

Mimi nashauri tuwe calm ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake.

Tukianza kuhalalisha hili tukio na baadhi ya watu flani, tutakua tunakosea na kuleta uhasama baina ya jamii bila ya sababu yoyote.

ROMA na mwenzie hawawezi patikana kwa kushutumiana.

Tuachie vyombo husika vifanye uchunguzi, Ndio vyenye dhamana hio
 
Ni mkolomije ndio anajua alipo. Anacheza chezo ili baadae aonekane HERO aandikwe tena kwenye magazeti ......anajua alipo ndio maana nimeshangaa mpoto nae yuko kwenye movement ya freeroma Snitch...wanacheza chezo na akina babu taleeent......na tushastuka. Warudisheni watoto wa watu. Msitafute sifa kwenye roho za watu
 
Msiingize hili tukio na mambo ya siasa. Akuna anae jua walitekwa na nani
 
Ndugu Daudi Bashite tafadhali mrudishe kijana wa watu ana familia na watt wadogo au sbb wewe bdo haujabarikiwa kupata mtt kwaiyo hauna uchungu? Tafadhali sana mrudishe kaka wa watu bado ana familia changa akamlee mtt wake tafadhali sana ndugu kkua na roho ya kibinadam kwa uliyoyafanya mpk leo basi inatooosha! Malipo ni hapaahapa duniani..Baba yako hatotawala milele!!
 
Ben nae ilikuwa hivi hivi, na sasa alianza kusahailika. Huenda kuna mtu au Kikundi cha watu kinahusika na matukio haya. Nchi iimarishe ulinzi la sivyo nchi hii haitakuwa mahala salama pa kuishi
 
bashite Mungu anakuona ujue hata wewe hautaishi milele
 
Ni kazi ya magamba.
Kinachonisikitisha ni kwamba vyombo vyetu vya usalama vinatumika vibaya.
 
Hata ikiwa serikali hakujihusisha Na Tukio la kutekwa na kupotea kwa msanii Roma serikali haitakwepa lawama hiyo. Kuna uwezekano kwa kikundi cha watu wametumia udhaifu wa serikali wa kutochukua hatua kwa vitendo vilivyotokea siku za nyuma kwa mfano ule uvamizi katika studio ya Clouds Fm na kile kitendo cha wale watu wasiojulikana waliomtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri Mheshimiwa Nape Nauye.
Serikali isiwe na double standard katika yanayohusu usalama wa nchi hii ni jukumu la serikali kulinda usalama wa raia wake. Nashindwa kujua kwanini serikali inashindwa kuelewa hawa vijana wapo wapi wakati baada ya familia kutoa ripoti simu zao zilikuwa hewani.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.
Usiseme serikali sema Bashite maana ndiyo Kageuka mariamungu wa Magu
 
Kuna siku mtachukuliwa wake zenu na wabazazi mtailaumu serikali ndio chanzo
Naomba unielewe sijasema serikali inahusika soma vizuri thread kabla hujatoa silly comments.
 
acheni kuishi kwa matukio...... kila kitu kikifanyika mnamwaga lawama kwa viongozii...." una uhakika gani serikali inahusika na upotevu wa huyo jamaa' siku nyingine uki post jaribu kuja na fact na si kuja na upotoshaji
 
Back
Top Bottom