Mkuu, unadhani ni kwanini Roma Mkatoliki ametekwa na siyo kukamatwa na polisi au vikosi vya usalama?
Je, kama ametekwa unadhani ni kwasababu gani za kisiasa au kimuziki au kimaslahi na watu fulani?
Je, unadhani kuna mkonoi wa serikali kwenye hili tukio?
Ushauri wa kitaalam:
Taarifa za kuhusu gari ilotumika kumteka huyu kijana yaani picha ya gari, na namba zake ziwekwe mitandaoni.
Namba ya usajili itafutwe ijulikane ni nani mmiliki wa gari hili na kwanini limetumika kuwateka Roma na wenzake.
Kuitafuta namba ya usajili ni pamoja na kuuiuliza TRA kuhusu umiliki wa gari hii.
Haya yote yanapaswa kufanywa kwa kuwa polisi wamekana kuhusika na utekaji huu ingawa umetaka kuonyesha hivyo kwamba voymbo vya ulinzi na usalama Tanzania vinajihusisha na utekaji raia wake.
Pia waziri wa mambo ya ndani hajatoa maelezo yoyote kuhusiana na hili.