Jeshi la Polisi laongeza muda wa maombi ya kazi baada ya Mfumo wa Mtandao wao kusumbua

Jeshi la Polisi laongeza muda wa maombi ya kazi baada ya Mfumo wa Mtandao wao kusumbua

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Polisi Kazi.jpg


TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUOMBA AJIRA
Mei 15, 2024 lilitolewa tangazo la kuongezwa kwa muda wa kuomba ajira na mwisho wa kutuma maombi hayo ilikuwa ni leo Mei 21, 2024.

Kutokana na changamoto ya mtandao iliyoendelea kujitokeza, mnatangaziwa kuwa vijana wenye sifa na nia ya kujiunga na Jeshi la Polisi zimeongezwa siku tano (5) za kuendelea kutuma maombi.

Hivyo, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kuomba ajira ni Mei 26, 2024 badala ya Mei 21, 2024.

Maombi yote yatumwe kupitia link: ajira.tpf.go.tz. Maelekezo mengine ni kama yanavyosomeka kwenye tangazo la Mei 9, 2024.

Imetolewa na: Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Makao Makuu ya Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA 21/05/2024

Malalamiko ya awali- Mfumo wa Ajira wa Jeshi la Polisi unasumbua, shida si mtandao ni mfumo wao wenyewe. Waweke njia mbadala ya kutuma maombi
 
Back
Top Bottom