Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi kuelezea tukio la Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Grayson Mahembe kujinyonga katika mahabusu alipokuwa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamisi, mkoani Mtwara.
Wamesema askari huyo baada ya kutoa maelezo alifungiwa mahabusu peke yake na askari wengine ambao ni watuhumiwa wenzake waliwekwa mahabusu nyingine za mikoani ili wasiharibu Ushahidi, ndipo alipochukua hatua ya kujinyonga.
Kwa suala la mazishi ya kijeshi polisi wamesema askari aliyejitoa uhai hazikiwi kijeshi kwa kuwa anahesabiwa hajafa kishujaa na hastahili heshima ya gwaride la mazishi linalochezwa na risasi na mabomu ya kishindo kupigwa.