Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeipokea na unaifuatilia taarifa iliyotolewa na Wakili Dickson Matata tarehe 31 Agosti 2026 kuhusu kushikiliwa kwa Godlisten Malisa baada ya kuwasili katika mpaka wa Namanga. Malisa alikuwa akirejea nchini akitokea Marekani kupitia Nairobi, Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, Malisa aliwasil Namanga majira ya saa tisa alasiri na kuwasilisha hati yake ya kusafiria kwa maafisa wa Uhamiaji. Baada ya kusubiri kwa saa kadhaa, aliondolewa eneo hilo na kupelekwa Kituo cha Polisi Longido. Baadaye gari hilo liliondoka kuelekea Arusha, huku simu zake zikiwa hazipatikani. Hadi wakati wa kutoa taarifa hii, mamlaka husika hazijatoa uthibitisho rasmi wa mahali alipo wala sababu za kushikiliwa kwake.
THRDC imewasiliana na Wakili Matata, ambaye ameeleza kuwa yupo Arusha akifuatilia suala hilo. Malisa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gifted Heart Foundation (GH Foundation), shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi nchini Tanzania, ikiwemo katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na magonjwa yasiyoambukiza.
THRDC inatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kutoa mara moja taarifa rasmi kuhusu mahali Malisa anaposhikiliwa, sababu na msingi wa kisheria wa hatua hiyo. Aidha, mamlaka zihakikishe usalama wake na zimwezeshe kuwasiliana na familia yake pamoja na kuonana na mawakili wake bila kizuizi.
THRDC itaendelea kufuatilia suala hili na kuufahamisha umma kadri taarifa zaidi zitakapopatikana.