Jeshi la Polisi latoa ufafanuzi juu ya tuhuma za baadhi ya Trafiki kuhusika na uchepushaji wa fedha

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
taarifa.jpg

Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoandikwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari zikisema "Wachepusha mfumo wa malipo".

Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi ikidai na kutaka kuaminisha umma kuwa askari wa Usalama barabarani wameingilia mfumo wa malipo ya fedha za serikali POS (Point of Sale) na kuchepusha fedha zilizotakiwa kuingia kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Kilichopo na kilichosahihi ni kwamba Jeshi la Polisi mbali na kuwa na mpango kazi na mikakati ya kutekeleza majukumu yake, hufanya usimamizi na ukaguzi wa namna Askari wanavyotekeleza majukumu yao ili kubaini ufanisi au ukiukwaji wowote ule.

Katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni ilibainika baadhi ya Askari walitumia mashine za kupima mwendokasi (,speed radar) kinyume na maelekezo ya Jeshi la Polisi. Baada ya kubainika walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa ambapo nane walishafukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo katika hatua za mwisho.

Hivyo mashine zilizotumiwa kinyume cha utaratibu kwa utashi na kwa manufaa binafsi ya hao askari ni za kupima mwendokasi na si zile zinazotumika kwa ajili ya malipo ya serikali (POS) kwani kuingilia mfumo huo si rahisi kama inavyoelezwa.

Mashine aina ya (POS) zinazotumika kwa malipo ya faini za barabarani hadi sasa uchunguzi haujabaini kwamba mfumo wa mashine hizo umeingiliwa na fedha kuchepushwa kama ilivyodaiwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kusisitiza kwa baadhi ya Waandishi wa Habari wanapoambiwa wasubiri ufuatiliaji unafanyika na taarifa sahihi itatolewa wawe na uelewa na subira kwani wasipofanya hivyo ipo hatari ya kutoa taarifa zenye kuleta taharuki kwa umma bila sababu yeyote ile.

Imetolewa na:

David A. Misime - DCP

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi

Dodoma, Tanzania
 
Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi ikidai na kutaka kuaminisha umma kuwa askari wa Usalama barabarani wameingilia
Polisi siku zote wamezoea kutufanya Watanganyika mazwazwa. Katika suala Hamza wa Ubalozi walitoa taarifa Hamza ni gaidi, katika suala la Aquelina wakatuaminisha risasi zilipigwa hewani. Kwenye suala la Mo Dewji wakasema gari ya south africa ilihusika kumteka.

Tangia matukio hayo sijawahi kuamini taarifa tata yoyote tena inayoitwa kutoa ufafanuzi inayotolewa na polisi.

Sawa, hao polisi walitumia mashine za kusoma speed kwa manufaa yao? How, walinufaikaje, mbona hamsemi?
Taarifa ya CAG inasema kuna POS zinaonekana zipo kazini lakini hazijawahi kufanya muamala, hili mbona hamjajibu?
 
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoandikwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari zikisema "Wachepusha mfumo wa malipo"...
Haya maelezo ya Polisi ni ya ubabaishaji, yanakwepa kueleza ukweli. Wanaweka lawama kwenye kutumia speed radar. Sasa hawa polisi walitumia speed radar kinyume cha taratibu ili iweje? Lazima walifanya kitu kinachohusiana na kutumia speed radar kwa namna ya kujinufaisha kifedha. Na kujinufaisha kifedha lazima waliingilia mfumo wa malipo kama watu wanavyosema, na lazima kwanza waanze na kutumia camera.

Wanachofanya hapa Polisi ni sawa na kumfukuza mwizi wa gari, halafu unapomkamata unasema kosa lake ni kuendesha gari kwa spidi kubwa wakati akifukuzwa na polisi, unaacha kutaja kosa la wizi wa gari.

Polisi hapa wanajaribu kuwatoa watu fikra toka ufisadi wa fedha uliokuwa unafanywa na kuonyesha kosa lilikuwa kwenye suala la camera. Huu ni upotoshaji wa makusudi, acheni upumbavu huu wa siku zote kutoa maelezo kwa manufaa yenu.
 
Hawa inaonekana wametumwa na kitu kinachoitwa serikali watoe ufafanuzi maana ni jambo la aibu mno kusikia mfumo wa CONTRLO NUMBER umeingiliwa. Watu wataogopa kufanya malipo ya serikali kwa kutumia CONTROL NUMBERS ni booooooom. Sasa wameambiwa wasafishe hapo.

Nimesikiliza taarifa ya habari ya saa 2 TBC Taifa, wamerudia na kusoma maelezo hayo hayo ya polisi. Kulikua na haja gani?
Wasituone sisi wajinga. Hawa wamefeli pakubwa.
 
Watu siku hizi hawana uoga tena. Iwe ulimpenda Magufuli au hukumpenda, lazima tukiri watu waliogopa kufanya wizi kama huu.

Lakini pia lazima tukiri kwamba suala la kuongezeka sana kwa wizi na ufisadi chini ya Samia linachangiwa na watu kuona kwamba kuanzia ofisi ya Raisi mwenyewe, mawaziri nk, ni wezi watupu. Sasa mtu anaona kama wao wanaiba, wamehalalishiwa kula kwa urefu wa kamba zao, mimi ni nani nijifanye muaminifu?

Kuna tetesi kwamba ndugu zake Samia, hata wale wa mbali, siku hizi wote ni mabilionea, sio Abdul peke yake! Sijui kama ni kweli, na kama ni kweli ni wazi ni ujumbe gani unafika kwa watu wenye dhamana ya fedha nchini.

Yale anayofunua Makonda ni tone dogo sana katika wizi unaofanyika nchini. Leo mpeleke Makonda Morogoro au Tanga nk, atakutana na yale yale anayoibua Arusha.

Tatizo ni kwamba tuna raisi dhaifu katika kusimamia nidhamu nchini, ambaye hakuna anaemuogopa katika kufanya ufisadi na kuiba, kwa sababu yeye binafsi watu hawamuamini kwenye mambo ya kujitajirisha na ndugu zake, wale wanaomzunguka kawaachia waibe waziwazi, na sasa kila mtu anaiba tu. Na labda pia ni asili ya Waafrika kutomwogopa mwanamke, hata akiwa raisi.

Kwa tunavyokwenda, nisingeshauri Samia aendelee kuwa raisi. Katika nidhamu ya kudhibiti ufisadi na wizi anafeli sana.
 
Kufuatia taarifa kuwa baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani wameingilia mfumo wa malipo ya fedha za Serikali POS (Point of Sale), Jeshi la Polisi limesema suala hilo si kweli bali linawahusu baadhi ya Askari waliotumia vibaya mashine za kupima mwendokasi (speed radar) kwa manufaa yao binafsi

Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime amesema baada ya ukaguzi wahusika walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa, Nane wameshafukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo katika hatua za mwisho

#KemeaRushwa #JFUwajibikaji #JamiiForums
 
Samahani, Nje ya mada..
"Mwenye Clip yoyote tangu voice recorder igunduliwe mwaka 1857 ya Jeshi la polisi futuhi Likikiri tuhuma?" Naiomba niingize kwenye historia ya safari channel.
 
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoandikwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari zikisema "Wachepusha mfumo wa malipo".

Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi ikidai na kutaka kuaminisha umma kuwa askari wa Usalama barabarani wameingilia mfumo wa malipo ya fedha za serikali POS (Point of Sale) na kuchepusha fedha zilizotakiwa kuingia kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Kilichopo na kilichosahihi ni kwamba Jeshi la Polisi mbali na kuwa na mpango kazi na mikakati ya kutekeleza majukumu yake, hufanya usimamizi na ukaguzi wa namna Askari wanavyotekeleza majukumu yao ili kubaini ufanisi au ukiukwaji wowote ule.

Katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni ilibainika baadhi ya Askari walitumia mashine za kupima mwendokasi (,speed radar) kinyume na maelekezo ya Jeshi la Polisi. Baada ya kubainika walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa ambapo nane walishafukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo katika hatua za mwisho.

Hivyo mashine zilizotumiwa kinyume cha utaratibu kwa utashi na kwa manufaa binafsi ya hao askari ni za kupima mwendokasi na si zile zinazotumika kwa ajili ya malipo ya serikali (POS) kwani kuingilia mfumo huo si rahisi kama inavyoelezwa.

Mashine aina ya (POS) zinazotumika kwa malipo ya faini za barabarani hadi sasa uchunguzi haujabaini kwamba mfumo wa mashine hizo umeingiliwa na fedha kuchepushwa kama ilivyodaiwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kusisitiza kwa baadhi ya Waandishi wa Habari wanapoambiwa wasubiri ufuatiliaji unafanyika na taarifa sahihi itatolewa wawe na uelewa na subira kwani wasipofanya hivyo ipo hatari ya kutoa taarifa zenye kuleta taharuki kwa umma bila sababu yeyote ile.

Imetolewa na:

David A. Misime - DCP

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi

Dodoma, Tanzania
Tangu lini Jeshi la Polisi la Tanzania limewahi kutoa taarifa ya ukweli????

Ni mtu mwendawazimu tu ndiye ambaye anaweza kuamini kwamba Jeshi la Polisi huwa linatoa taarifa za ukweli.
 
Maelezo bado hayajamaliza utata

Wiki 1 nyuma jamaa yangu kanisimulia, alipigwa cheti kisha akalipa, baada ya wiki kadhaa akadakwa, anaambiwa anadaiwa, jamaa akasema mbona kalipa, akawaonesha na meseji, polisi nao wakamuonesha kuwa hakijalipwa, ukitizama kwao bado deni, huku kalipa na control namba ni ile ile. Ikabidi alipe tu maana alikuwa na haraka zake.

Nikamuuliza imewezekanaje nae akaniambia alishangaa kama ambavyo mie nashangaa.
Sasa nimeona hii nikamkumbuka, huenda alicho iambia ni ukweli.
 
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoandikwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari zikisema "Wachepusha mfumo wa malipo".

Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi ikidai na kutaka kuaminisha umma kuwa askari wa Usalama barabarani wameingilia mfumo wa malipo ya fedha za serikali POS (Point of Sale) na kuchepusha fedha zilizotakiwa kuingia kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Kilichopo na kilichosahihi ni kwamba Jeshi la Polisi mbali na kuwa na mpango kazi na mikakati ya kutekeleza majukumu yake, hufanya usimamizi na ukaguzi wa namna Askari wanavyotekeleza majukumu yao ili kubaini ufanisi au ukiukwaji wowote ule.

Katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni ilibainika baadhi ya Askari walitumia mashine za kupima mwendokasi (,speed radar) kinyume na maelekezo ya Jeshi la Polisi. Baada ya kubainika walichukuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa ambapo nane walishafukuzwa kazi na kufutwa Jeshini na wengine kesi zao zipo katika hatua za mwisho.

Hivyo mashine zilizotumiwa kinyume cha utaratibu kwa utashi na kwa manufaa binafsi ya hao askari ni za kupima mwendokasi na si zile zinazotumika kwa ajili ya malipo ya serikali (POS) kwani kuingilia mfumo huo si rahisi kama inavyoelezwa.

Mashine aina ya (POS) zinazotumika kwa malipo ya faini za barabarani hadi sasa uchunguzi haujabaini kwamba mfumo wa mashine hizo umeingiliwa na fedha kuchepushwa kama ilivyodaiwa.

Jeshi la Polisi linaendelea kusisitiza kwa baadhi ya Waandishi wa Habari wanapoambiwa wasubiri ufuatiliaji unafanyika na taarifa sahihi itatolewa wawe na uelewa na subira kwani wasipofanya hivyo ipo hatari ya kutoa taarifa zenye kuleta taharuki kwa umma bila sababu yeyote ile.

Imetolewa na:

David A. Misime - DCP

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi

Dodoma, Tanzania
Alipaswa kuwashukuru watoa habari na si kuwalaumu kuwa wameripoti kimakosa.
 
Watu siku hizi hawana uoga tena. Iwe ulimpenda Magufuli au hukumpenda, lazima tukiri watu waliogopa kufanya wizi kama huu.

Lakini pia lazima tukiri kwamba suala la kuongezeka sana kwa wizi na ufisadi chini ya Samia linachangiwa na watu kuona kwamba kuanzia ofisi ya Raisi mwenyewe, mawaziri nk, ni wezi watupu. Sasa mtu anaona kama wao wanaiba, wamehalalishiwa kula kwa urefu wa kamba zao, mimi ni nani nijifanye muaminifu?

Kuna tetesi kwamba ndugu zake Samia, hata wale wa mbali, siku hizi wote ni mabilionea, sio Abdul peke yake! Sijui kama ni kweli, na kama ni kweli ni wazi ni ujumbe gani unafika kwa watu wenye dhamana ya fedha nchini.

Yale anayofunua Makonda ni tone dogo sana katika wizi unaofanyika nchini. Leo mpeleke Makonda Morogoro au Tanga nk, atakutana na yale yale anayoibua Arusha.

Tatizo ni kwamba tuna raisi dhaifu katika kusimamia nidhamu nchini, ambaye hakuna anaemuogopa katika kufanya ufisadi na kuiba, kwa sababu yeye binafsi watu hawamuamini kwenye mambo ya kujitajirisha na ndugu zake, wale wanaomzunguka kawaachia waibe waziwazi, na sasa kila mtu anaiba tu. Na labda pia ni asili ya Waafrika kutomwogopa mwanamke, hata akiwa raisi.

Kwa tunavyokwenda, nisingeshauri Samia aendelee kuwa raisi. Katika nidhamu ya kudhibiti ufisadi na wizi anafeli sana.
Nimerudia mara mbili kuangalia Avatar yako mkuu.

Ni kwa jinsi ulivyokuwa umetema madini matupu na nikahisi kuwa comment yako ilifaa ifungie mada.

Kuna nini tena, kuna mantiki gani zaidi ya maneno uliyoeleza hapa yenye ukweli tupu?
 
Asante Mkuu. Hivi vitu ukitafakari kwa makini utaona tatizo liko wapi kirahisi sana
 
Back
Top Bottom