Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Soma pia:

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.

Screenshot_20250222-153220_1.jpg

Soma: Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa video mjongeo iliyokuwa ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa.

View attachment 3245354
So ndio michezo yao hiyo? Wataaminikaje kulingana matukio simalar to hayo?

What if video isingechukuliwa?
 
Is that a way of handling a criminal? Askari anapaswa kufanya kazi kwa weledi na kwa uangalifu sana.

Ukamataji ulifanyika kienyeji bila kuonesha ujuzi wa kitaaluma.
Ilikuwa ni purukushani za kishamba zilizodhaniwa kufanywa na watu wasio na ujuzi wa kazi za kiusalama.

Imagine raia wangeamua kuingilia kati varangati ingekuwaje?

Askari hata akiwa kiraia ( askari kanzu) Kuna picha na ujumbe lazima auneshe na kuutuma kwa hadhira Ili kujibu sintofahamu.

Wajifunze kuwa smart katika kazi zao.
 
Jeshi halina credibility ya kuaminika. Kwa nini wasingewatuliza wananchi kisha wakawatoa wasiwasi pamoja na kudhibitisha kwamba ni polisi na tunampeleka kituo fulani?
Embu acha utoto wako hapa. Yaani wewe kila siku unaunga mkono uovu tu Utafikiri na wewe ni mhalifu. Kwanini usiulize sababu ya yule wa pikipiki aliyekuwa anakamatwa kutokutii Amri?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa video mjongeo iliyokuwa ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa.

View attachment 3245354
Hakukuwa na namna sahihi ya kumkamata hadi watumie njia ile
 
Ujinga ni mzigo ndugu yangu. Kulikuwa na ubaya gani, polisi mmoja anawatangazia wananchi kuwa, "Ndugu wananchi sisi ni polisi msiwe na wasiwasi tunamkamata huyu ni mtuhumiwa" Halafu anatoa kitambulisho kuna ubaya gani?
Jeshi halina credibility ya kuaminika. Kwa nini wasingewatuliza wananchi kisha wakawatoa wasiwasi pamoja na kudhibitisha kwamba ni polisi na tunampeleka kituo fulani?
 
Back
Top Bottom