Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Jeshi la polisi latolea ufafanuzi tukio la bodaboda kusemekana kutekwa, wasema ni mhalifu aliyekuwa anatafutwa muda mrefu na polisi

Tena huyo mhalifu wamemsamehe sana maana alikuwa anakimbia na kukataa kutii amri hata pale alipoonyeshwa vitambulisho vyote. Inatakiwa wamfinye sanaa ili ataje na wenzake na kurudisha vitu alivyoiba kwa watu.
Hujajibu swali mhalifu ndio anakamatwa hivyo?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Jeshi letu la Polisi Nchini limetoa ufafanuzi wa kina juu ya video mjongeo iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikionyesha dereva bodaboda au mtu mwenye pikipiki akikamatwa na watu waliovaa kiraia nakisha baadaye kupakizwa kwenye gari nyeusi na kuondoka naye.

Jeshi letu la polisi limesema tukio hilo lilifanywa na askari wetu kwa mtu huyo ambaye alikuwa ni mhalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji kwa kutumia pikipiki.

Kwa hiyo watanzania tuache mihemuko na lawama na kutupa maneno yasiyo na ukweli. Tuwe watu wa subira na kushirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi kupata taarifa rasmi.

View attachment 3245354

Soma: Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha
Choko wewe,angekuwa mhalifu sugu angekuwa nje kwa dhamana??umesikia alichoongea baada ya kuachiwa?shoga weww
 
Tena huyo mhalifu wamemsamehe sana maana alikuwa anakimbia na kukataa kutii amri hata pale alipoonyeshwa vitambulisho vyote. Inatakiwa wamfinye sanaa ili ataje na wenzake na kurudisha vitu alivyoiba kwa watu.
Wewe kidampa hopeless kabisa sikiliza hapa kijana anaeleza mkasa mzima na vile huwa huna internet ya uhakika nakupa summary kuwa hao watu walikuwa wakimfuatilia ili wamgonge sasa ndio ukamataji huo?

Hata licha ya kuwa wamemkamata wamempiga akiwa ndani ya gari hadi alipofikishwa kituoni wameendelea kumpiga , sasa huo ndio utaratibu wa wapi kumpiga mtu aliyefungwa pingu?


View: https://youtu.be/4upFAaJHGvg
 
Ni rahisi kwa mpumbavu kukurupuka na kulaumu jeshi la polisi kwa kuwa uhalifu huu haujamgusa yeye binafsi au familia, lakini mwenye hekima angeweza pengine kulishukuru jeshi la Polisi kwa majukumu wanayoyafanya kupamabana na uhalifu nchini.
Nakuunga mkono kabisa.
 
Huna akili wewe dada, hakuna anayesema wahalifu wasikamatwe tuna hoji kwanini wakikamata mtu wasitoe taarifa kwa uongozi wa mtaa au kwa watu waliokuwa karibu? huna maana kabisa. Husikii matukio ya utekaji? jinga sn ww mama
Hatukubali utekaji but wengi ni watu wa matukio ule wake za watu,uibe mali za watu unaachalwaje hai kwa mfano unajua madhara ya hivyo vitendo
 
Wewe kidampa hopeless kabisa sikiliza hapa kijana anaeleza mkasa mzima na vile huwa huna internet ya uhakika nakupa summary kuwa hao watu walikuwa wakimfuatilia ili wamgonge sasa ndio ukamataji huo?

Hata licha ya kuwa wamemkamata wamempiga akiwa ndani ya gari hadi alipofikishwa kituoni wameendelea kumpiga , sasa huo ndio utaratibu wa wapi kumpiga mtu aliyefungwa pingu?


View: https://youtu.be/4upFAaJHGvg

Jee ni mhalifu au ni mtuhumiwa tu?
Mtihani mzito
 
Jee ni mhalifu au ni mtuhumiwa tu?
Mtihani mzito
Huyo bado ni mtuhumiwa.

The presumption of innocence until proven guilty ndio hatua aliyopo, hao waliomkata wanatakiwa kuja na evidence beyond reasonable doubt kuonyesha sasa ni mhalifu.
 
Jee ni mhalifu au ni mtuhumiwa tu?
Mtihani mzito
Kuna pande mbili mfano wewe wakili
Jambazi kakukata mapanga na mashoka akaiba vitu vyote ndani ya nyumba na gari akashikwa na polisi wa doria kabla kuondoka na sura unamtambua uko hoi na madonda mkono na mguu umekatwa unaugulia ICU kwako wewe huyo ni mtuhumiwa? Utamchukulia mtuhumiwa wakati mia kwa mia ulioma live akikuta kata na mapanga na mashoka askari wakakuokoa asiendelee kukuchalanga mapanga na mashoka
Polisi mfano wamemdaka huyo jambazi akikukata kata na mapanga na mashoks
Kwako binafsi ni mhalifu asilimia 100

Ukiulizwa mfano na BBC kuwa wewe kama.wakili nguli huyo aliyedakwa live akikucharanga mapanga na mashoka ni mhalifu au sio mhalifu hadi iwe proved mahakamani kuwa yeye mhalifu vinginevyo kwa sasa sio mhalifu ni mtuhumiwa ndivyo utajibu wewe wakili nguli?

Na kuwa Polisi waache ujinga wamchukulie tu huyo kama mtuhumiwa sio mhalifu wasubiri mahakama ithibitishe kwa sasa wao ni innocent na dhamana wapewe
 
Tanzania hatuna ukabila ila hizi itikad za kisiasa zimetuadict kuliko hizo heroin na cocain.
Yaani akili za kawaida kama mtz neutral hazitakiwi kbsaa kwamb lazima usifu usipo sifu basi wew ni mhalifu au mpinzani.
Anyway kwakuw hili jamvi liko mubashara tunaamin wahusika wamo(polisi) humu.
Ni hivi kama kweli mmeridhika na taswira yenu kuwa na utata kwenye jamii au kwamba hiyo ndo only,last and best option bhasi kila la kheri.
 
Sasa mbona wamemuachis, nikisikiliza maelezi yake baada ya kiachiwa....!

Naona Police wa ngazi za juu, Huwa wanadanganywa sana....!
 
Tii Sheria bila shuruti mambo kama haya hayakupati,uibe,uibe wake za watu unategemea nini
Mkuu naona leo wew na Lucas M mmekuwa ndege wafananao. Nkwel hatuwez fanan mawazo lakin mjitahid msiwe mnasaliti mnachokiamin mioyon mwenu, otherwise uelewa wenu ndo huohuo wa comments zenu.
 
Back
Top Bottom