Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kamanda wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua ameyasema hayo February 20,2026, Katika Kata ya Lengijave Mkoani Arusha, ambapo amesema kuwa upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani kwaajili ya hatua za kisheria.
Aidha, SACP Pasua amesema kuwa kutokana na Operesheni zinazofanywa na Kikosi hicho kote Nchini changamoto za usafirishaji wa Mifugo bila kibali zimepungua huku akiwataka Wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi hicho katika kutokomeza Uhalifu Dhidi ya Mifugo.
Naye Afisa Mifugo Kata ya Lengijave Bwana Hedson Kindia, amesema kuwa wamekuwa wakazingatia uhalali wa umiliki na usafirishaji wa Mifugo katika Kata hiyo wakati wote PAMOJA na kulinda haki za Mifugo katika umiliki na biashara.
Naye, Kalani Lukumai ambaye ni Mfugaji wa Kata hiyo, amelipongeza Jeshi la Polisi pamoja na Shirika hilo kwa kuendesha Operesheni huku akiwataka Wananchi kuwa walinzi wa mifugo hiyo katika kukuza ustawi wa Mifugo Nchini.