Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Jeshi la Polisi Tanzania limewakamata Watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu wa kumbaka na kumlawiti Msichana na kusambaza video yake mitandaoni ambapo imebainika tukio lilifanyika Swaswa Dodoma mwezi May 2024.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa leo August 09,2024 imesema “Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson”

“Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe Mahakamani,
kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani”
View attachment 3065469
Maswali:-
Hao watuhumiwa wawili waliojificha ni akina nani? Majina yao kwa nini hayajatajwa? Kwa nini picha zao hao watuhumiwa hazijawekwa hadharani? Makazi yao hao watuhumiwa waliojificha ni wapi hasa?

Jeshi la Polisi naona linazidi kupoteza mwelekeo wake, kwa nini hasa wanaficha wahalifu???
 
Kwa maswali haya kuna kila dalili suala hili liko compromised na wenye vitambi
 
Acheni ujuaji raia, jeshi la polisi lipo vizuri kama huamini fanya uhalifu kimbia uone,
Mnaowatetea waliosambaza video mmeshindwa kujiuliza swali rahisi sana, video waliipata wapi hadi waanze kuisambaza? hapo ndipo polisi walipoanzia, hongera jeshi la polisi, hongera Mama Samia, tunaitaka Tanzania ya Amani.
GOD BLESS THE DEAD
 
Kesi kusikilizwa mfululizo! Hapo ni kuhukumiwa tu! Kwa hiyo ukitaka kesi yako isikilizwe haraka hakikisha tukio limerekodiwa ktk video na kurushwa mitandao ya jamii, victims wa ubakaji wapo wengi ila kesi zinachukua miaka mingi kusikilizwa sababu matukio hayakurekodiwa au kuvujishwa mitandaoni. Usawa mbele ta sheria uzingatiwe.
 
Back
Top Bottom