Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wananchi wa tarafa ya Nyamiaga Kata ya Murukulazo Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera wameaswa kutokukichukulia sheria Mkononi na badala yake kuzifikisha changamoto zao katika mamlaka husika huku akiweka wazi kusakwa kwa wote walifanya mauaji ya mwanchi katani humo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ngara Mrakibu wa Polisi SP William Solla baada ya kukutana na wananchi wa kata hiyo lilipotokea tukio la mauaji ya mwananchi mmoja yaliyotokea Febuari 2025 katika kata hiyo.
Amesema kuwa kitendo hicho cha mauaji sio kizuri katika jamii ya watanzania hususani wakazi wa Ngara ambao hawana sifa hiyo.
SP Solla amewaomba wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ambapo amewaomba kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya mauaji wilayani humo huku akiwataka pia kutoa taarifa za watu wanaoficha wahamiaji haramu wilayani humo.