Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezuia mkutano wa waandishi wa habari wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Mnyika uliopangwa kufanyika leo Jumatatu 27/1/2025 saa tano asubuhi.
View attachment 3215420
Nje ya jengo la Makao Makuu hayo wapo askari wa jeshi la polisi kwa taarifa tulizonazo waandishi wa Jambo TV, Azam TV, Mwananchi wamezuiwa na kuondolewa eneo hilo.
View attachment 3215428
Aidha sababu zinazoelezwa juu ya kuzuiwa kwa mkutano huo inadaiwa ni uwepo wa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati (M300). Huku ikielezwa kuwa mkutano huo wa CHADEMA ungeweza kusogezwa mbele na kufanyika kuanzia tarehe 29.
View attachment 3215422
View attachment 3215487
Pia, Soma: Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika kuongea na Waadishi wa Habari Makao Makuu ya Chama, Mikocheni